Calcutations (Maisha ndani ya Dar)

Mlachake

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
4,437
Reaction score
4,618
What is more Expensive? Living in your own house at Mbezi Mwisho(Morogoro Road) while working at The city centre, Or living in a rented house in Sinza and Renting your house to simeone else?
 
it depends on your calculations and conveniences. To me Some places in Sinza are overcrowded and the value for money in those ares are not convincing me to rent.
 
Unataka kusema tuwafurumushe wahindi wote kule uhindini(Upanga, kivukoni, kariakoo,kisutu etc) ili nasi tufaidi matunda ya uhuru wetu. Maana wanakaa kwenye magorofa yetu kwa rent sawa na bei ya njiwa while sisis tunakaa madongo kuinama na kuwa tortured na long cues.
 
Bora kupanga sinza ukapangisha nyumba yako mbezi
 

Hapa ndipo Naichoka Nchi yetu.
 
it depends on your calculations and conveniences. To me Some places in Sinza are overcrowded and the value for money in those ares are not convincing me to rent.

Well said mkuu.
ila hii habari ya kutoka ofisini saa kumi na moja unafika nyumbani saa nne ya usiku, Unakunywa zaidi ya Tshs. 10,000 kwenye foleni kila siku unaionaje?
 
What is more Expensive? Living in your own house at Mbezi Mwisho(Morogoro Road) while working at The city centre, Or living in a rented house in Sinza and Renting your house to simeone else?

Mkuu, Kama Mbezi unaenda kuulaza mwili wako tu, bora pangisha nyumba nawe Upange Sinza/Mwenge.

Ila kama una vikuku,vibata, vimbuzi, ving'ombe na vilimao na vichungwa.....bora tu uteseke na mifoleni, labda iko siko Maisha bora kwa mtanzania inaweza ikawa kweli.
 
hakuna bora kati ya hayo uliyoyataja...bora zaidi ya hayo ni kuhama nchi au kungoa uongozi wa nchii uliyopelekea kuwa na miundombinu na mifumo mibovu sana ya maisha...kukaa kwenye foleni more than 2 hours ni tatizo la kitaifa na hata ukikaa sinza trafik jam ni ishue...achilia mbali mafuriko ya mvua za dar...huwezi jua wapi ni bondeni na wapi ni milimani....
 
Bora kupanga sinza ukapangisha nyumba yako mbezi

Nimeishi sinza miaka7 katika nyumba ya kupanga nasasa naishi mivumoni(ni karibu sawa na mbezi mwisho) kwenye nyumba yangu nimegundua ni bora kuishi mivumini kwangu, kwasababu gani? ghalama za kupanga Sinza kwa nyumba yenye huduma kama ya kwangu ni zaidi ya 400,000 kwa mwezi. Nikitaka kupangisha ya kwangu naweza kupata 150,000 au laki2 kwa mwezi. Hapa kinachojadiliwa nadhani ni ghalama za kusafiri kutoka Sinza kwenda kazini(City centre) na kutoka Mbezi mpaka kazini(City centre). Kwa uzoefu nilioupata ghalama za maisha kwa ujumla zimepungua. sitarijadiri suala la conviniency maana inategemea na nature ya kazi ya mtu

Yaliyojitokeza.
1. Ghalama za mafuta kwa mwezi hazijaongezeka sana kwasababu siyo kila siku ninakwenda kazini kumbuka kuna week ends, sikukuu na likizo. nikiwa Sinza nilikuwa natumia mafuta wastani wa Tshs 10,000 kwa siku ambayo ni Tshs300,000 kwa mwezi kwasasa natumia wastani wa Tshs20,000 kwa siku ambayo ni 600,000 kwa mwezi. Ukichukua Pango400,000 + mafuta300,000=700,000
wakati kwa mivumoni natumia mafuta600,000+pango150,000(technically 150,000 is revenue to me)=750,000 tofauti ni 50,000 ambazo zinajifuta na yafuatayo.
2. Ghalama za vyakula mivumoni(hata mbezi) kidogo zipo chini kwa mfano bei ya mhogo au mchicha mivumoni/mbezi haifanani na sinza.
3. Impulse buying(Manunuzi yasiyopangwa) mivumoni(hata mbezi) ipo chini ukifananisha na sinza

Haya ni machache sana kati ya manufaa ninayoyapata kutokana na kuishi kwenye nyumba yangu mivumoni. usisahau kuishi kwenye nyumba yako kunakufanya ukopesheke kirahisi hata madukani mambo yakikaa vibaya
 

Kumbe weye jirani yangu, itabidi nikutafute tukapige bia.
 
am sorry unasema???!!!!kazi kwelikweli lakini tutafika!
 
Mkuu Gama hata hivyo zile nyumba nyingi zilikuwa za kwao zikataifishwa tu-refer arusha declaration 1967
 

Mkuu, well said!

Kwa kuongezea tu Mivumoni unaweza kujilimia vimchicha na vipilipili vyako......bado gharama zinapungua hapo....lakini sinza labda mchicha uupande kwenye ndoo.
Pia mivumoni waweza kujifugia vikuku vyako na vibata kadhaa wakati Sinza utatafuta kugombana na majirani tu.
 

Maisha ya kuviziana usiku mtu anakuja kutupa takataka karibu na mlango wako kisa hana mahala pa kuchimba jalala na hana pesa za kumlipa mtu wa kubeba taka siyataki tena.
 
Binafsi naamini tunahitaji kufanya analysis ya kina zaidi kuweza kujua wapi pana cost saving. Pia ni muhimu kutofautisha financial saving na convinience zingine ambazo ni ngumu kuziweka kwenye monetary terms e.g. hewa nzuri, kukopesheka madukani e.t.c.

Binafsi nina nyumba Mbweni Mpiji about 50 km kwenda na kurudi toka city centre, nimeamua kupangisha hiyo nyumba kwa pango dogo kabisa la 170,000 na kupanga Tabata Bima ambapo ni 20 km kwenda na kurudi toka city centre kwa kodi ya sh. 300,000.

Faida za Tabata
1. Mafuta ya gari sh. 200,000 kwa mwezi
2. Napata usingizi wa kutosha na kupumzika tayari kwa siku nyingine
3. Napata muda mrefu wa kukaa na familia yangu na mama totoo
4. Napata muda wa kukagua na kufuatilia maendeleo ya watoto wangu on daily basis
5. Nikiwa naenda kazini napata muda wa kuwa drop watoto shuleni kulingana na muda ninaoondoka
6. Kutokana na kuendesha kilometa fupi fupi, inanichukua zaidi ya miezi 3 kufanya service ya gari na tyre kuisha faster



Hasara za kuishi Tabata so far zijaziona, kumbuka cost ya maisha ni karibu sawa sawa in terms of food prices

Faida za kukaa Mbweni
1. Hewa nzuri
2. Raha ya kukaa nyumbani kwako (obviously nyumba yako ina raha zaidi ya kupanga kisaikolojia)


Hasara za kuishi Mbweni
1. Kuamka saa 10 usiku na kurudi home saa 5 usiku monday to friday
2. Magonjwa ya kisaikolojia yanayoambatana na kukaa muda mrefu kwenye foleni
3.Car maintanance cost is relatively higher interms of fuel and service
4. The longer you drive in terms of kilometa na speed the higher the possibility of getting involved in accidents
5. Huna muda wa kukaa na watoto na mkeo/mmeo
6. Hata mkeo anaweza kuchepuka kirahisi kwa sababu anajua mpaka ufike home utakuwa umechoka na utachelewa. kwa hiyo mkeo anaweza kushawishika kupata cha chap chap teh teh teh

So ni bora kupanga eneo la karibu na ofisi yako kuliko mbali especially kama tofauti ya distance ni kubwa na kuna foleni.
 
Jamani njooni mikoano kuna unafuu mkubwa,kwani lazima wote mkae dar?mimi kwa mfano nipo moshi mjini,6km kutoka ofcn kwangu natumia lita 1 tu kwa siku,yaani elfu 2.2 hakuna foleni wala nini

Duh, kweli una raha yaani 1 lita kwa siku? mimi kila siku ni km 168 sawa na Moshi - Arusha. Yote life.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…