Calcutations (Maisha ndani ya Dar)





Kazi kweli kweli!!!! ila mzee kwa mbezi na Sinza the difference is negligible na nazani kwa issue ya foleni sometimes hata sinza inakuwa balaa !

Mwanamke kugongwa hiyo ni tabia yake na ni kama unakula chips kila siku kana kwamba huwezi kuwa na energy ya kutosha kumsatisfy unaporudi na kama ni issue ya foleni sidhan kama kutoka Dar kwenda Mbeni it can take u mpaka saa 5 Ucku otherwise u have otherbussines to do, cdhani kama ni foleni hiyo mkuu!
 

Very nice reasoning Buddy. Nikuta sholae?
 
Sisi tunakaa Tandale, kazi Manzese natembea kwa miguu tu kutoka nyumbani kwenda kazini
 
Kwako ni Kwako Tu ........na Sikuzote Kwako Hakujawahi na Haitakaa itokee Kwako Kukawa Mbali

Knyama, Sinza , M/ nyamala Nyumba sasa hv ni Tzs 350,000 - kwa mwezi kwenda juu, Na hiyo ni nyumba ya Vyumba 2 tuuuuuuuuuu.

Jenga Ukae Kwako achana na mawazi Mgando
 

Ninasishi Mbezi mwisho,nami nilijuwa mmoja wa wanaoumia na foleni ya Morogoro roads,lakini faida ya kukaa nyumbani kwangu ni kubwa millions tines ya kupanga,kwanza nina eneo la kutosha kwangu na familia yangu,hewa safi sana,Vikuu,vimchicha flesh nk.
Isitoshe kwa wale wanaokaa mbezi mwisho kuna njia mbadala ya kukwepa foleni ya morogoro road asubuhi na jioni.Nifuatishe kama ifuatavyo...Through Chuo kikuu kuelekea Changanyikeni,moja kwa moja mpaka karibu mita 200 na geti la JESHI,kuna njia inacvhepuka kulia pana kibao cha ASSEMBLIES OF GOD CHANGANYIKENI fuata hiyo njia ya kuelekea kanisa la TAG,nenda moja kwa moja ukizingatia kulia kama kuna njia inachepuka kwani kushoto kwako ni kuelekea eneo la jeshi kama kms 3 unakua umemaliza eneo la jeshi unaungana na barabara ya Makongo juu,Baada ya kama mita 200 toka kumaliza msitu wa kejeshi na kuungana na barabara ya makongo juu kuna barabara inashuka bondeni upande wa kushoto,ifuate ukizingatia kushoto hadi kwenye daraja linalojengwa la mto mbezi pana diversion,fuata hiyo njia moja kwa moja hadi Goba,unapinda kushoto kuelekea mbezi mwisho,Goba na mbezi mwisho ni 10KM.hakuna foleni kabisa. Inanichukua 30min.toka mlimani city hadi home mbezi mwisho. Jumla ni 16KMS toka mlimani city. Try it you will enjoy,Kuishi kwenye mji wako kuna raha zake,USIPIME BWANA
 
Jamani,kukaa zaidi ya 30KM kutoka kazini,na foleni za Dar.hayo ni mateso makubwa kisaikologia na kifedha pia.tumeshindwa kuishi mbezi na familia yangu kwa sababu ya foleni na usalama mdogo uliopo ktk maeneo ya kando ya Dar.

Nashauri kama hujajenga ,nenda ukajenge kigamboni,huko kutakuwa nafuu ya foleni pia siyo mbali na city center.
vinginevyo karibuni sana kinonondoni,kijitonyama,mwenge,sinza na ukiweza upanga 🙂
Maisha ndio haya haya ,sasa kutumia zidi ya saa 6 barabarani uhuo ni upungufu wa kutafakari na kuchukua hatua.ni heri ukiwa unapenda kuishi ktk nyumba yako ya mbezi/kibamba /bunju etc basi bora ufungue duka huko huko ujiajiri or weka mazingira ufanye kazi yako karibu na unapoishi.
 

Goba Mwisho na Mbezi ni Kilometa Tisa Taslimu na kwa sasa barabara nimeipita inaonekana hiko bomba sana.
 

Mzalendo Mpya:

Inategemea na njia unazopita. Kama wewe unasema kwenda mbezi ukuchukua wastani wa masaa sita yaonyesha ya kwamba wewe huwa unafuata nyororo kuanzia 'Faya'; Manzese; Ubungo Mataa; Mbezi Mwisho etc lakini wanaojua njia za mkato hiyo si issue kabisa. Sinza et al ni full mabaa na gesti bubuz. Hivi watoto wako pamoja na mama changa kuwapitisha hiyo barabara ya Shekilango na Urafiki mida ya 'Sungu Sungu' kazini unawafundisha nini? Maadili sehemu hizo ni sawa na sufuri. Wajanja woote uenda Sinza et al kula maisha lakini familia ziko nje ya mji zinakula 'real life'
 
Mimi nilipo natumia baiskeli tu dk 2 kazini.Gari kwa J1 na j2 tu.Ndo raha ya Mkoani bwana.
 
True said, kuishi sinza kuna challenges za maadili ya watoto etc,nazungumzia maeneo ya karibu na city center,kwa familiy person sinza hapafai kabisa,ila tabata,kigamboni bado ni pazuri na travelling time ni fupi sana,

kuna aliyezungumzia kupita shortcuts and panya route,embu tafakari familiy members wako ambao usafiri wao ni Daladala na hawana option zaidi ya bodaboda.
 
Hapo na mimi nakuunga mkono.
Wingi wa magari Dar ukichangiwa na ufinyu wa barabara unaleta foleni sana.
Maana hata ukikaa Sinza, Mwenge, Mikocheni, etc, foleni bado ni kero tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…