Kwa muda wa zaidi ya mwezi sasa hapa JF kumekuwa na matangazao ya CallTanzania.com yakiashiria kuwa bei ya simu kuita Tanzania (nadhani kutokea marekani) ni senti 13 tu kwa dakika. Swali langu siyo kuhusu huduma zenyewe bali wamiliki wa biashara ile; je ni watanzania?
Utafiti wa haraka haraka umeonyesha kuwa kampuni hii CallTanzania.com inamilikiwa na Miron Enterprises LLC, ambayo pia inamiliki keepCalling.com na PeruTel.com. Miron Enterprises LLC yenyewe inamilikiwa na mtu ajulikanaye kama Florin Miron, na imesajiliwa huko Americus, Georgia. Lakini CallTanzania.com, KeepCalling.com na PeruTel.com zote zinaendesha biashara zake kutokea address moja ya Bellingham, Washington State.
Kama kuna anayemjua huyu bwana Miron kwa zaidi namwomba anisaidie kujua kama jamaa huyo ni Mtanzania. Nina dukuduku tu kwa vile tangazo lake linayoonyesha utanzania sana. Nafahamau wakenya kadhaa ambao wana makampuni ya simu na wanafanya vizuri kwa sitashangaa kusikia kuwa kuna watanzania pia wameshaingia kwenye biashara hiyo ambayo inalipa sana.