Cameroon: Kanisa Katoliki latoa wito wa Haki na Amani

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Kanisa Katoliki nchini Cameroon limetoa wito wa utulivu huku kukiwa na hofu ya kutokea machafuko, wakati nchi hiyo ikisubiri matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 12, 2025. Kanisa hilo limesema matarajio yao ni kwamba matokeo yatakuwa na uwiano na maoni ya wapiga kura.

​
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na Radio France Internationale (RFI) leo Oktoba 21, 2025, ikinukuu taarifa ya Baraza la Maaskofu wa Katoliki wa Cameroon (NECC), maaskofu hao wamehimiza utulivu na amani, wakitoa wito kwa wahusika wote wa kisiasa kujiepusha na maamuzi yenye madhara kwa taifa.

"Tunatumai kwamba matokeo rasmi yataakisi matarajio ya wapiga kura, na kwamba hakuna kitakachobadilishwa na mamlaka yoyote inayohusika katika mchakato huu," wamesema maaskofu hao.

Kanisa Katoliki, ambalo ni mojawapo ya taasisi zenye ushawishi mkubwa na kuheshimika zaidi nchini humo, limekuwa likichukuliwa kama sauti ya maadili katika masuala ya kijamii na kisiasa.

Hali ya taharuki imeongezeka baada ya mgombea wa upinzani na msemaji wa zamani wa serikali, Issa Tchiroma Bakary, kujitangaza kuwa mshindi wa uchaguzi huo. Tchiroma anadai kuwa amemshinda Rais Paul Biya, mwenye umri wa miaka 92, ambaye anatafuta kuongeza muda wa utawala wake wa miaka 43 kwa kipindi kingine cha miaka saba.

Kujitangaza huko kumeibua upinzani mkali kutoka kwa Serikali na Chama tawala cha Cameroon People's Democratic Movement (CPDM), huku maafisa kadhaa wakieleza kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria na ni cha kichochezi.

Tume ya uchaguzi ya taifa hilo (ELECAM) bado haijatangaza matokeo rasmi, na ina muda hadi Oktoba 27, 2025, kutangaza mshindi wa uchaguzi huo.

Hata hivyo, msimamo wa Tchiroma kwamba “atatetea ushindi wake” umewatia hofu wachambuzi wa siasa na wananchi, wakihofia kwamba tangazo la matokeo linaweza kuchochea ghasia au machafuko katika taifa hilo la Afrika ya Kati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…