Elections 2010 Campaign ads

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Hivi CHADEMA wamejiandaaje kuhusiana na kutengeneza matangazo mafupi mafupi ya kampeni ambayo yatarushwa na vituo vya televisheni na redio?

Ningependa kujua kama kuna wanaojua.
 
wanahitaji mchango kwa ajili ya hayo matangazo,tehe tehe tehe.
Vp mzee mtaalam nn wa Ads tuletee kama ya GOP .........................................utani bana subiri wenye majibu watakupatia Nyani.
 
wanahitaji mchango kwa ajili ya hayo matangazo,tehe tehe tehe.
Vp mzee mtaalam nn wa Ads tuletee kama ya GOP .........................................utani bana subiri wenye majibu watakupatia Nyani.

Kikwete ana gaffes nyingi sana kiasi kwamba amerahisisha kazi ya kum-swift boat.....hiyo kama akipatikana mtengenezaji mzuri wa matangazo na kama vyombo vya habari havitaogopa kuyarusha.
 
Ngabu
Sidhani kama watakosa matangazo, ila dubwasha limeshachukua almost mitaa yote jijini kwa matangazo yao, unadhani CHADEMA wataonekana kweli bila hata billboard moja?
 
Kikwete ana gaffes nyingi sana kiasi kwamba amerahisisha kazi ya kum-swift boat.....hiyo kama akipatikana mtengenezaji mzuri wa matangazo na kama vyombo vya habari havitaogopa kuyarusha.

Tatizo hivyo vyombo vya habari pia
 
Ngabu
Sidhani kama watakosa matangazo, ila dubwasha limeshachukua almost mitaa yote jijini kwa matangazo yao, unadhani CHADEMA wataonekana kweli bila hata billboard moja?

CCM is not playing....they are going all out despite having the upper hand. And If CHADEMA wants to give them a run for their money then they need to out work and out campaign them.
 
Nyani Ngabu,
Mkuu hili muhimu sana na sijui kama Chadema wameshalifanyia kazi. Tena kwa vijana kama nyie mlioko majuu nadhani mnajua jinsi ya kuchora picha hizi kwa kuzingatia WATU wanaopelekewa ujumbe na bila shaka mchango wenu unatakiwa sana ingawa ndio huishia hapa JF.

Ingekuwa bora sana kama kila mbunge wao angekuwa na siku au dakika za kuhutubia moja kwa moja kupitia TV au kuweka Ad zao ktk vipindi mbalimbali hasa vile vinavyosikilizwa sana. hakuna kitu kama matangazo (ads) pamoja na kwamba yana gharama kubwa lakini mwisho wa siku malipo yake ni makubwa.

Kwa mfano zikichukuliwa hotuba za JK akitoa ahadi kisha inakatwa na kuuliza haya ya kweli?.. kisha inaonyeshwa hali halisi.
JK akwaahidi wafanyakazi inakatwa na kisha kurudisha hotuba yake kwa wazee wa jiji la Dar. yaani kila kitu kilichosema na CCM kipewe picha ya madhambi yaliyofanyika. Hii ni katika kuongeza hasira za wananchi na kumalizia Uchaguzi ni wenu wananchi kama wanataka kuendelea kudanganywa kwa Tshirt na khanga basi na waendelee kuichagua CCM lakini kama wanataka mabadiliko ya kweli wachague Chadema..
 
Nadhani ads the billboards ndizo zita wafikia watu wengi zaidi na kwa urahisi zaidi. Kwa mfano ukiweka billboards kadhaa mitaa ya Mwenge mpaka Posta hile ni barabara ya wafanyakazi kwa hiyo watu wataziona karibia kila siku mara mbili. Pia billboards hazina muda maalumu kama t.v. na radio muda wowote zipo na kila anaye pita ata ziona. Ukienda kwenye makampuni mazuri ya hizi billboard ads una fanyiwa project moja nzuri tu.
 
Yaani Bob wee acha tu.....kuna ammunition za kutosha kabisa kuwashambulia CCM. Kwa mfano hiyo ya inayodaiwa Kikwete kusema hataki kura za wafanyakazi...kama kuna tape yake ni kiasi cha kuhariri tu na kuongeza mengine mawili matatu kitu na boksi
 
I'm talking about an all out effort here. Halafu siku hizi Tanzania kuna TV na redio kila kona. Sio kama ilivyokuwa zamani. Hata kwetu Ikungulyabashashi kuna TV.....

Kwa hiyo mabango, placards, flyers, etc. etc. yote pouwa tu....wanaweza hata kukodi magari yenye picha za mgombea wao na yakawa yanazunguka kwenye sehemu mbalimbali kumtangaza.
 
nchi inavyoendeshwa na wanafiki hii ...........tv wataambiwa air time yote imeshauzwa, hakuna slot.
 
Mwaka huu umekosa kabisa shamrashamra za kampeni. Hata mabandiko huko njiani ni machache sana. Nadhani takukuru nao wamechangia
 
nchi inavyoendeshwa na wanafiki hii ...........tv wataambiwa air time yote imeshauzwa, hakuna slot.

Kama ndio havyo basi kuna umuhimu wa kuwa na angalau sheria inayofanana na 'equal time rule'.....(hii kama hatuna sheria ya hivyo)

Hivyo kama kukosa wakose wote na si wengine wapate halafu wengine wawekewe vizingiti vya kusingizia
 
kwa vyombo vya habari vya umma nafikiri kuna muongozo kama si sheria inayovitaka vitoe nafasi sawa kwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki kwenye uchaguzi.

lakini sidhani kama kuna sheria inayovibana vyombo vya habari vya binafsi

uongozi wa chadema uje utupe mwanga kwenye hli
 
Mwaka huu umekosa kabisa shamrashamra za kampeni. Hata mabandiko huko njiani ni machache sana. Nadhani takukuru nao wamechangia

Takukuru wanachangiaje? sherehesha
 
Hivi CHADEMA wamejiandaaje kuhusiana na kutengeneza matangazo mafupi mafupi ya kampeni ambayo yatarushwa na vituo vya televisheni na redio?

Ningependa kujua kama kuna wanaojua.

Hey dude I was thinking on the same, hasa the ads kwa maneno yao wenyewe kama jamaa zako wa faux (In their own words).............. Mfano ni hiyo ya kura za wafanyakazi, Tambwe akitokea anapigwa na ile ya akihamia CCM alale na mama yake, Makamba akionekana tu anapigwa na zile gaffes zake alipokuwa natetea mafisadi.

The simplest one could be haya masuala ya shule......... Ukitoka nje ya Dar just some 50kms kuna shule kwenye jimbo la muungwana zimeezekwa nyasi, hazina vyoo wala madirisha......... Sasa kama huyu jamaa alikuwa mbunge huko for more than 15yrs, Waziri na pia raisi kwa miaka mitano hizo shule anazosema na kutamba wamejenga ziko wapi?

Kuna ile ya muungwana kumpa hela mtoto mdogo, unamuibulia picha ya watoto ombaomba hapo Dar na kuuliza amefanya nini for the last five yrs kutatua tatizo hilo.

Unampiga na nyingine kwa style ya faux, kama mwenyekiti ameanguka hadharani zaidi ya mara tatu je si wakati muafaka watanzania kuelezwa ukweli kuhusu afya ya mgombea wa CCM? uNACHOMBEZA NA mAKAMBA KUSEMA NI sWAUMU halafu baadae Kinana kusema upungufu wa sukari.

They are just endless.

Ofcourse hata kama TV na redio wanadengua kurusha matangazo haya YouTube can do us better in the beginning
 
..mimi nangependa matangazo yenye vibwagizo "hatudanganyiki" na "ashindwe na alegee."

..kuna maeneo ametoa ahadi ambazo hajazitekeleza, sasa hapo mnamuweka kwenye "kideo" kabisa, mwisho wa tangazo mnamaliza na kibwagizo "hatudanganyiki."

..lingine unaweza kuweka zile gaffes zinazochukiza kama aliposema mimba za wanafunzi zinatokana na viherehere vyao. mwisho wa tangazo kama hilo unamaliza na "KIKWETE ashindwe alegee," simultaneously unaonyesha kideo cha kulegea na kuanguka pale jangwani.

..wa-Tanzania hawana muda na ma-detail na uchambuzi kwa hiyo inawezekana kabisa ushauri wa Ngabu wa kuwa-swift boat CCM unaweza kufanya kazi. political adds zikiwa nzuri na wananchi waka-relate nazo zinaweza kufanya kazi nzuri kuliko hata hotuba.
 
Hahaha JokaKuu umeniacha hoi. Ila hiyo ya kushindwa na kuelegea is a bit too much coz the guy is clearly not well and it wouldn't be right to use his illness for political advantage....

Ila umenichekesha
 
Kama ndio havyo basi kuna umuhimu wa kuwa na angalau sheria inayofanana na 'equal time rule'.....(hii kama hatuna sheria ya hivyo)

Hivyo kama kukosa wakose wote na si wengine wapate halafu wengine wawekewe vizingiti vya kusingizia

Sheria ya uchaguzi inasema hivyo ila nani kakwambia Tanzania watu wanafuata sheria..! Umesahau Kikwete mwenyewe alibariki rushwa kwa kusema utaenda Kilimanjaro kuongea na wazee bila kitochi cha Pombe.?? Tukaambiwa alikua anatania tu..!
 
Ngabu said:
Hahaha JokaKuu umeniacha hoi. Ila hiyo ya kushindwa na kuelegea is a bit too much coz the guy is clearly not well and it wouldn't be right to use his illness for political advantage....

Ila umenichekesha

Nyani Ngabu,

..lakini JK mwenyewe amejichekesha chekesha na kudai tatizo lake lilikuwa na swaumu tu. hivyo baada ya kugida glasi ya maji akaendelea kudunda.

..mtengeneza tangazo anaweza kujitetea kwa ku-play fool kwamba JK hana matatizo yoyote serious ya kiafya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…