Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
Kweli REDET wamebobea kwa uongo, kwa akili ndogo tu hivi kweli Daily News linaongoza kwa kusomwa sana na watu,vijijini au mijini? hapa tu inadhihirisha kuwa utafiti umefanyika maofisini hasa ofisi za serikali na hii inanifanya nitilie mashaka utafiti wao kama ni wa kweli au wa kubuni na kufurahisha watu wao.Kwa vyombo vya habari na jinsi vinavyotoa elimu ya uraia, asilimia 42.7 ya wahojiwa waliridhika na utendaji wake ambapo redio ziliongoza kwa asilimia 73.7, televisheni asilimia 41.6 na magazeti asilimia 27.4 na upande wa magazeti gazeti la Daily News liliongoza kwa kusomwa sana kwa asilimia 25.6, Mwananchi asilimia 17.1 na Nipashe asilimia 12.4.
Utafiti unatakiwa uendane na hali halisi iliyopo huwezi kusema utendaji wa serikali unaendelea vizuri wakati huohuo unasema 2/3 ya wabunge wao ambao ndio wanaunda serikali wameonekana hawatarudi maana yake hawafai, I believe in research but I dont trust every research.