najua watu wanaamini utalii. lakini wanaokuja kwetu hawatumii pesa za hapa. anakuja na ndege ya kigeni, anapokewa na magari yanayomilikiwa na wageni, anafikia hotel zinazomilikiwa watu wa nje haohao, anachukua charter zao na kurudi kwao. halafu baada ya hapo hao foreigners wanarudisha faida hizo kwao. pesa tutakayopata ni ya vinyago na fees ndogondogo. ufaransa mtalii anatumia 70% ya gharama zote hapo. tanzania mtalii anatumia asilimia tano. biashara kichaa. yaliyokea kwenye almasi yatatokea kwenye uranium na gesi. wala tusijipe matumaini. tunahitaji mtazamo mpya.