kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,779
- 4,982
Canada imechukua hatua ya kujitenga na Marekani baada ya Rais Donald Trump kuwekea ushuru wa 25% kwa bidhaa kutoka Canada na Mexico, pamoja na ushuru wa 10% kwa bidhaa kutoka china .Viongozi wa Canada, wakiongozwa na Waziri Mkuu Justin Trudeau, wameamua kuachana na Marekani kabisa. Mark Carney, ambaye anasadikiwa kuchukua nafasi ya Justin Trudeau kuanzia Machi, amesema kwamba hawezi kujibembeleza kwa Marekani. Aliongeza kwamba ni bora Canada ikateseka kiuchumi kuliko kuendelea kuwa na urafiki na nchi inayojionyesha kama mnafiki. Canada itakutana na changamoto hizi kwa umoja, na watarudi wakiwa imara zaidi