Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,925
- Nilizaliwa kabla Tanganyika haijapata uhuru.
- Nilikuwa na akili zangu na kutambua vizuri siku Tanzania ilipopata uhuru.
- Niliouona muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
- Niliona kuanzishwa kwa Azimio la Arusha.
- Nilishiriki kuchagua jina la chama kipya, ambacho hatimaye kilijulikana kama CCM. Nilikuwa mwanachama wa CCM.
- Nilikwenda Jeshi la kujenga Taifa.
Cancer huanza ndani ya mwili na ikiendelea hujitokeza juu. Cancer ya ufisadi na rushwa iliyoendelezwa na CCM imesambaa sana na sasa imeibuka na kujionyesha wakati huu. Je bado tunataka watu kama hawa waongoze nchi yetu?
Baadhi ya viongozi wa tawi la CCM Mburahati Barafu, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Kilie Mhovile (kushoto), Katibu wa Jumuiya ya Wazazi na mjumbe wa kamati ya siasa, Shani Omary (wa 2 kushoto) na kulia ni mjumbe wa shina 31, Mahmoud Mwinyi, wakionyesha leja feki zilizokamatwa na Umoja wa Vijana wa tawi hilo. Leja hizo ambazo zilikutwa nje ya ofisi ya tawi hilo jana, zinadaiwa kuwa na majina ya watu waliofariki dunia.
CCM walizana rafu
Wakati matokeo zaidi ya kura za maoni kupitia CCM yakiendelea kutolewa na wakongwe wakizidi kubwagwa, yamezua fadhaa kubwa miongoni mwa wagombea walioangushwa na wafuasi wao na sasa wanayapinga Habari Kamili