Captain Geogre Bantu kurithi usukani kuliongoza jahazi bila Captain Mkuu Gardner G. Habash

humu JF kuna kila taaluma kuanzia wabashiri, wambea, waganga wa kizungu na wa jadi n.k. Sasa mtuambie mapema na huyu apewe muda gani kabla hajakaa naye?
 
Sisi wengi wakongwe tunakumbuka historia ya Captain Gardner nguli wa vipindi vya redio, alianza kama muuza cassette (Kanda) za audio na video pale jijini mwanza kama mtu wa masoko,
Kweli kabisa. Nakumbuka miaka hiyo hasa 1998 kila nilipokuwa nikifika Mwanza ilikuwa ni lazima niingie FM Studio jirani na Mwanza hotel kununua audio cassete na nilikuwa namkuta Gardner hapo studio kama muuzaji. Na baadae kwa muda fulani alihamia duka fulani la kuuza TV lililokuwa jirani kabisa na hiyo FM Studio. Kama sikosei mmiliki wa hilo duka alikuwa anaitwa Mushi.
 
....Wamrudishe Mussa Hussen kwenye kipind cha Jahaz....Bantu wakiwa na Mussa kipindi hakitatetereka sana maana Musa Pia wanaendana na Bantu na hata kipind Gadnar Yupo Musa alionekana Ku fit...Gadner, Bantu na Mussa Hussein ilikua Combination Poa
 
Kwa nini mnawaza arudishwe nani, sijui nani akae na nani? Mi naona ni wakati wa kukipa kizazi kipya nafasi. Wawekwe hawa watoto ili watangazie watoto wenzao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…