Captain Malik ''encyclopedia'' ya historia ya mpira Tanzania

Captain Malik ''encyclopedia'' ya historia ya mpira Tanzania

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074

Captain Malik

Jina lake ni Captain Malik. Captain Malik ni mtu maarufu sana kwa watu wa Dar es Salaam hasa wa kizazi cha miaka ya 1950 nyuma kidogo na mbele kidogo ya hapo. Captain Malik sasa anaweza kuwa anakaribia miaka 80 na kupita kidogo. Captain Malik yuko katika orodha yangu ya watu ambao nimefahamiana nao na wamenishangaza kwa akili zao nyingi walizojaaiwa na Allah kiasi kuwa unapozungumza nao haukuchukui muda kutambua kuwa huyu si mtu wa kawaida ambae unaekutana nae Karikaoo kila uchao. Mara moja akili yako inatambua kuwa huyu ni mtu mwenye kipaji ambacho si cha kawaida.

Katika orodha hii yangu nitawataja wachache na nawataja kwa kuwa tayari wameshatangulia mbele ya haki – Peter Colmore, Jim Bailey, hawa ni Wazungu Colmore ni Mkenya mwenye asili ya Uingereza, na Bailey ni Kaburu wa Afrika Kusini na mwingine ni Sheikh Ali Muhsin Barwani, Mzanzibari. Kaka yangu Captain Malik yuko ndani ya orodha yangu hii.

Captain Malik katika ujana wake miaka ya mwishoni 1950 na kuanzia 1960 alikuwa akicheza mpira Young Africans ya Dar es Salaam akiwa nahodha na hapo ndipo alipopata jina lake hili la ‘’Captain,’’ ambalo limemganda hadi leo. Captain Malik ananiitikadi mimi kama mdogo wake nami siku zote amekuwa kaka yangu na kwa kweli si mimi tu, sisi wengi tuliokulia Kariakoo tunamuheshimu Captain Malik kama kaka yetu.

Jana nimemkuta Capatain Malik katika kizingiti cha Msikiti wa Manyema baada ya Sala ya Alasiri anavaa viatu aondoke. Baada ya mazungumzo nikamuomba nimpige picha na akanikubalia na ndiyo hiyo picha hapo juu. Captain Malik Allah amempa kile Wazungu wanakiita, ‘’Photographic Memory,’’ yaani kipaji cha kukumbuka kwa usahihi kabisa kila kile ambacho jicho lake limeona kuanzia tarehe, majina, mahali na yote yaliyokuwapo kwa wakati ule.

Kushoto Athmani Kilambo katika utu uzima 2010 na Abubakar Shariff mchezaji

wa Cosmopilitan

Athmani Kilambo alikuwa mchezaji wa Yanga na pia timu ya taifa ya miaka ya mwanzoni 1960 akicheza nafasi yoyote ya ulinzi na alitokea Bagamoyo akiwa kijana mdogo labda miaka 20 hivi. Captain Malik ndiye aliyempokea Yanga na kumkabidhi jezi kucheza mechi yake ya kwanza Ilala Stadium. Huu ukaja kupelekea usuhuba mkubwa baina yao uliodumu nusu karne hadi alipokufa Kilambo. Mimi nimemfahamu Kilambo tayari keshakuwa mchezaji maarufu kabisa akijulikana ndani na nje ya Tanganyika wakati ule, mchezaji mwenye umbo kubwa lakini mwepesi na hodari wa ‘’sliding tackles,’ kiasi akiwamudu vilivyo wachezaji wakali wa enzi zile. Kilambo alipatapo kunambia siku moja kuwa yeye wagomvi wake walikuwa wachezaji wa Kenya hasa Wajaluo kwa kuwa wakitumia nguvu sana katika uchezaji wao. Kilambo anasema Kocha wao wa timu ya taifa ya Tanganyika Myugoslavia Celebic akijua mchezo wa Kenya wa kutumia nguvu na alikuwa katika Gossage Cup akimpanga Kilambo beki wa kulia na Mohamed Chuma beki wa kushoto na hawa wote walikuwa, ‘’hard tacklers,’’ wana uwezo mkubwa sana wa kupambanisha chuma kwa chuma. Kilambo anasema washambuliaji wa Kenya wakiwaogopa sana wao.

TIMU YA BANDARI 1960s MWISHONI

Nyuma waliosimama kulia Maulidi Dilunga, Hassan Gobbos, Athmani Kilambo, Kitwana Manara, Abdulrahman Lukongo,

Kitenge ''Askari'' Baraka, Joseph Anthony.

Waliochutama kulia Mohamed Chuma, (pass), Jamil ''Denis Law,'' (pass), Mbaraka Salum, Abdulrahman ''Bwana Fedha'' Juma (pass) Mohamed Msomali

Turudi kwa Captain Malik.

Captain Malik siku moja kaanichekesha sana kiasi cha kutokwa na machozi. Anasema siku hizo Kilambo mgeni Dar es Salaam na Yanga bado hajawa, ‘’senior player,’’ bahati mbaya timu imeingia uwanjani Ilala Stadium yeye kachelewa na alipofika lango kuu askari wakakataa kumpitisha ingawa aliwaambia kuwa yeye ni mchezaji wa Yanga. Ikabidi Captain Malik afatwe ndani ili aje langu kuu kumtambua Kilambo na kumuingiza ndani awahi kuvaa jezi na kuingia uwanjani. Captain Malik anasema kamkuta Kilambo nje pembeni katoa macho kajikunyata hajui nini la kufanya.

Captain Malik ni ‘’Encyclopedia,’’ ya historia ya mpira Afrika ya Mashariki na hasa Tanzania. Ana hazina kubwa sana ya historia na matokeo muhimu ya mchezo huu ndani ya Yanga, Simba wakati ule ikiitwa Sunderland, Cosmopolitan na club ndogo za mjini kama African Temeke Good Hope, Liverpool, Kahe Republic, Rover Fire na nyingine nyingi za mitaani. Itafaa sana kama Tanzania Football Federation (TFF) watatafuta muda wazungumze na Captain Malik wapate historia za viongozi wa mpira waliopita kama marehemu Kitwana Ibrahim kiongozi wa Yanga maarufu sana Kondo Kipata, Patron wa Simba Habib Segumba akijulikana kama ‘’Underline,’’ au manahodha waliopita wa timu ya taifa kama Captain Ayub Mohamed, au ‘’strikers’’ wa kutisha kama Yusuf Mwamba au wachezaji waliocheza timu ya taifa katika umri mdogo sana kama Hemed Mzee, mchawi wa chenga, Mbwana Abushiri akijulikana kama ‘’Director,’’ wapigaji penalty na ‘’free kicks,’’kama Hemed Seif waliokuwa wakiogopewa, magolikipa hodari wa ‘’diving,’’ kama Kitwana ‘’Popat’’ kabla hajaacha kuecheza golini na kwenda kucheza mbele na kuwa mshambuliaji hodari. Captain Malik ataeleza vipi Kiwana alipomkosesha goli la wazi Enos Bondo katika mechi ya Tanganyika na Kenya Kombe la Gossage pale Kitwana alipochomoka golini wakati Enos Bondo keshawatoka mabeki wote anakabilina na goli na Kitwana akaruka juu na kuangukia kwenye miguu ya Bondo na kuokoa hatari ile na Kitwana Popat akatolewa nje kwa machela ameuia bega vibayasana. Picha hii Kitwana yuko hewani ilipigwa na ikatoka katika magazeti yote. Ilikuwa picha nzuri sana ya ‘’action.’’ Captain Malik anayajua yote haya na katika uhodari wake atakupangia timu yote ya Kenya na Tanganyika kutoka kichwani. TFF mtafuteni Captain Malik atawarithisha hazina yake na faida kubwa sana ya kumbukumbu itahifadhiwa.

Timu ya Tanganyika iliyochukua Kombe la Gossage 1965 waliochutma kulia ni Kitwana ''Popat'' Manara, Sembwana, Mohamed Chuma, Abeid Maulid, Mbaraka Salum, Abdallah Aziz

Nyuma waliosimama kulia Kitwana Ibrahim, Hemed Seif, Sharif Salim (Captain), Mwalimu Julius Nyerere, Kocha Celebic, Hamisi Kilomoni

Mstari wa nyuma ya Mwalimu Nyerere kulia Mathias Kissa, mwisho kushoto Mohamed Msomali, Emil Kondo, John Limo, Abdulrahman Lukongo, Hamisi Fikirini na Rashid Seif mdogo wake Hemed Seif

Hemed Seif katika utu uzima 2007

Captain Malik ana mengi katika suala la uchawi katika mpira na ''politics,'' za kupata wachezaji wazuri katika enzi zao, ‘’Benchi la Ufundi,’’ na atakupa na majina ya mafundi wenyewe na walikokuwa wakiwatoa na nini walikuwa wakifanya. Captain Malik atakupa na majina ya vijana waliokuwa wakitumwa kufanikisha mambo haya kabla ya mechi kubwa ya Simba na Yanga labda jana yake usiku wa kuamkia mechi na siku ya mechi wakati timu zinajitayarisha kuingia uwanjani. Miaka ile Kariakoo walikuwa wakiishi wenyewe wenyeji, bado hawajahama kuyapisha maghorofa. Siku ya meshi ya Yanga na Simba pale Mnadani. Mtaa wa Mafia na Msimbazi washabiki wa timu hizi watawasha vitezo na kuchoma ubani toka asubuhi na bendera zinakuwa zimepandisshwa za yanga na Simba zikipigwa na moshi wa ubani. Hali ya mji inakuwa imebadilika toka asubuhi washabiki wa Mnadani wanashambuliana kwa maneno makali makali ya kuvunjana nguvu kuwa nani atatoka mshindi jioni ile. Wkati ule mechi hizi zinachezwa Ilala Stadium. Kwa leo ukitazama unajiuliza watu wailiweza vipi kuenea uwanja mdogo kama ule. Captain Malik kayashuhudia haya yote kwa macho yake na si kama mchezea pembeni.

Katika ''politics'' za kuwaleta wachezaji utastaajabu kujua kuwa Yanga walikuwa na mapenzi makubwa na baadhi ya wachezaji wa Sunderland wakitana sana kuwachukua kuja kuongeza nguvu Yanga. Viongozi wa Yanga na baadhi ya wachezaji wakimtaka sana wawapate Hamisi Kibunzi siku zile akijulikana kama, ''Mapafu ya Mbwa,'' kwa ile stamina yake ya kupanda kushambulia na kurejea nyuma kulihami goli na wampate pia Arthur Mambeta. Lakini Yanga walikuwa kila wakiwapima wanaona kuwa Hamisi na Arthur walikuwa na mapenzi makubwa na Sunderland wasingeweza kucheza vizuri katika jezi ya Yanga. Hiki ndicho kipindi labda Yanga wakageuza macho yao kuelekeza Morogoro na kuwachkua akina Gibson Sembuli, Juma Matokeo na wengineo.

Mimi namjua vizuri Captain Malik na TFF haitajuta kumtafuta kwa mazungumzo.
Nyongeza kutoka kwa Sharif Mohamed Yahya:
[8:25 PM, 1/25/2018] Shariff Mohamed Yahy: Samahani!
Timu hiyo ya Gossage ni ya mwaka 1965, ambayo ndiyo alocheza Rashid Seif, kijana mdogo wa Primary School wakati huo.

Mashindano yalikuwa Kampala.
Alobeba kombe ni Sharif Salim (capt).

Nakumbuka hivyo kwani mwaka huo, 1965, ndio Tanga ilichukua Taifa Cup kwa mara ya kwanza nami nilkuwamo kwenye kikosi hicho.

Mwaka 1964 Dsm, Tanganyika ilichukua pia, Captain akiwa ni Mbwana Abushiri.

1963 Gossage Nairobi alipoumizwa Kitwana na Enos Bondo, aliechukua nafasi ni Wingi Mzenga (Tanga) ambae alikuwa kwenye Timu ya Taifa tangu 1959.

Ni majuzi baada ya kifo cha Omar Kapera, na kusikia Sunday Manara yu mgonjwa nilizungumza na Kitwana.

Alifurahi sana nilipomwambia mwaka ule 1965, mwandishi wa Nation, Poly Fernandes, aliandika, "Tanganyika itachukua tena kombe, kwasababu kipa wao ni Kitwana Ramadhani, ili umfunge itabidi upige kwenye mstari wa goli, jambo ambalo haliwezekani kutokana na ngome imara ya Tanganyika, na kupiga nje ya box itachukua karne moja kumfunga Kitwana.''
 
nikiona sredi yako ni lzm niisome, kweli bro huchoshi kwa uandishi wako, pesa ilotumika kukusomesha haikufa bure kama ilivyo kufa iliyotumika kumsomesha jingalao.
 
Captain Malik katika ujana wake miaka ya mwishoni 1950 na kuanzia 1960 alikuwa akicheza mpira Young Africans ya Dar es Salaam akiwa nahodha na hapo ndipo alipopata jina lake hili la ‘’Captain,’’ ambalo limemganda hadi leo.
Ndugu yangu Said, nimeisoma habari hii ya kusisimua kwa hamu sana. Nimeifurahia. Subira yavuta kheri. Nilijiuliza: Huyu tena ni Captain wa NINI? Wa JESHI? Jibu nikalipata aya ya tatu....Hakika hata Yanga Afirika yafaa WAISOME hii Sankolopidia ya Soka. Pia wampe kheshma yake huyu Mzee na wenzake wote...
 
Chuwaa...
Siku hizi kuna mabadilo makubwa sana katika hivi vilabu hakuna tabia
ya kuwaleta karibu waliopita katika hizi timu kama viongozi, wachezaji
au washabiki maarufu.

Salaam zitafika In Shaa Allah.
Hii hapo chini niliandika hapa siku nyingi zilizopita:

Utangulizi

Kumekuwa na mjadala mkali sana kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika katika JF:

Angalia hapo:

Tuepuke sumu hizi: Brigedia Jenerali mstaafu Francis Mbena

Mjadala umevutia wachangiaji wengi na nimejibu kila swali lililokuja na kuweka rejea kadhaa, picha za zamani na ''links,'' kumsaidia msomaji kuijua histori ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.

Wengi wanahangaishwa na kusoma majina ya watu ambayo hayamo kwenye historia kama waijuavyo wao.

Ikafikia mahali nilihisi kuwa wametosheka.

Ghafla mjadala ukageuka ukawa sasa ni mimi kutukanwa matusi khasa.

Hapo ikawa tena siwezi kuendelea na mjadala kwani ni tabu kujibu matusi ndipo nikaamua kuja na haya niliyoandika hapo chini:

Mohamed SaidmahaliVerified User ✅
[HASHTAG]#601[/HASHTAG]
31 minutes ago
Joined: Nov 2, 2008
Messages: 8,440
Likes Received: 1,872
Trophy Points: 280

Hii kauli kubwa na kauli thabit wenye kutaka kuelewe wataelewa wasio taka wataendelea kujitia ujinga na kuendeleza mabishano yasio na mantiki wala mashiko.

Hakika sheikh Muhamed allah amekuruzuku mengi ambayo wengi wetu allah ametunyima.

Hakika yeye ndio mwenye kila sifa na anestahiki kuabudi wa na kushukuriwa.

Sahimtz,
Majuzi hapa kulikuwa na Simba Day.
Nimekaa leo asubuhi na kuwaza vipi Simba ilikotokea.

Sijui kama Simba walifanya kisomo, yaani khitma ya kuwarehemu
viongozi, wachezaji na wapenzi wa club toka enzi za Sunderland.

Ikiwa walifanya kisomo naamini kabisa katika majina ambayo
yaliyotajwa moja litakuwa la Ayubu Kiguru.

Aliitwa Ayubu Kiguru kwa kuwa mguu wake mmoja ulikuwa na
athari.

Hii ilikuwa miaka ya 1960.

Mimi bado mtoto na nikipenda Sunderland na nikimjua Ayubu kwa
karibu sana na sababu ni kuwa Ayubu alikuwa na ubao wa biashara
Soko la Kariakoo na mjomba wangu Bwana Khamis Salum na yeye
alikuwa na ubao wake si mbali na ubao wa Ayubu Kiguru.

Ayubu alikuwa na sura jamil na alikuwa mweupe wa rangi.
Mungu alimjaalia Ayubu kipaji cha kuongea na kubishana.

Soko la Kariakoo enzi hizo lilikuwa moja ya vituo vya ushabiki wa mpira
Dar es Salaam.

Yanga na Sunderland walitawala soko na Yanga washabiki wao wengi
walikuwa na biashara ya kuuza samaki kiasi ikawa watani wao wakiwaita
Yanga, ''Wauza Samaki.''

Siku ya mechi ya Sunderland na Yanga moto ulikuwa unawaka sokoni pale
toka mapema asubuhi.

Ushabiki huo utaendelea kwa juma zima takriban baada ya mechi.
Sasa ikitokea kuwa Yanga imefungwa na Sunderland washabiki wa Yanga
walikuwa tabuni kwa juma zima pale sokoni wakipigwa makombora na
Ayubu Kiguru.

Ayubu
alikuwa na uwezo wa yeye peke yake kuwanyamazisha Yanga wote
pale sokoni kwa maneno yake, kejeli na kebehi lakini katika namna ambayo
mtu hawezi kughadhibika bali ni kucheka tu.

Enzi zile za Ilala Stadium kelele za kuzomea zikizidi kutoka upande wa Yanga
Ayubu atasimama kuwaelekea Yanga na atatoa maneno watu watacheka.

Yanga maneno yakiwaingia kisawasawa na sasa wamepwelewa hawana la
kusema basi watamwambia, ''Wewe Ayubu nani atakuweza bwana kiwete
wewe nyie mlojaaliwa na Allah ni mdomo tu.''

Jibu litakalotoka litamaliza ubishi wote watu watatawanyika watamuacha
Ayubu anapanga nyanya zake huku amevaa jezi ya Hamisi Kilomoni.

Ilikuwa Sunderland ikishinda Ayubu anachukua kikombe anakujanacho
sokoni anakiweka mbele ya ubao wake watu wanapita wanatunza.

Ayubu alikuwa akizoza lakini si kutokana na hamaki wala hasad ya nafsi.
Ilikuwa ndiyo kusherehesha ushabiki wa Yanga na Sunderlaand wala mtu
haendi Msimbazi Polisi kushitaki kuwa kabughudhiwa na Ayubu Kiguru.

Ayubu Kiguru hakuwa na maradhi ya nafsi ya chuki na husda kutaka nema
iliyo kwa Yanga iwaondokee.

Moja ya dalili za husda katika moyo wa mtu ni chuki na hii chuki huja baada
ya mtu kujidhihirishia ndani ya moyo wake kuwa fulani hamuwezi kwa lolote.

Kinachobaki ni kumwaga matusi na kumchukia.

Labda ''administrators,'' wa hii barza yetu wataliangalia hili la mtu hana kheri
ila kila aandikapo yeye ni kumwaga matusi.

ZOKqAPBmC8q1UbYrbXg59vBZeKzVpKf9Wu3ZBQKJRK8buK7jqXPlZbnYiXjFt74XQ95hda2vVKX8R6peFY-wpn-fcDMOHFgIl6E8IILuYKsSINjCYUQt9iTkttnzb96_Gz-kGjuTQyy2goQtOIFcx5H86rcRP7f1gI96PLk5FD3LudGalWSABrYM2TlVEf7v5sMXVRuyEFYPy8oKsHENjt-CvWIlXP7Yr8eGvaVgegBMHw7mlMwNYRqVdpzD0GSQr_lTQCEk2wSU7j_mxzJ5XcXBYDl31GPx2-CotchSWa5l2sBqVP18o-SRCZexCjWF4v_0ncn0zY0qyT-y3Io2XnxUvG194A9Mdr0BSKhb9XtlayuO5EqMA-0YlAqwkiWOXh3AJ6v4b8M9iPSAiNtIAO-Qj3gI9GcO59NapGKis4a395qK1xm_x4vOsICU4-o3dlqxzBii5aU9roRF6xMwac-dxeiD4spNY01V0JWdp8kLhoqk2aQHG_qArAKpKtmDnqJddC5fHD7flU8Z3q_UWDLGDJfQHe_lFEMbEcnkO_elbaKmiZ67UNQQ-hnMFANgHEpOqN8ySCSs11GQeubtFBzv7ehL7q8l=w596-h657-no

Ilikuwa ''ambition,'' yangu siku moja nivae jezi ya Sunderland lakini kipaji kilikuwa
kidogo nikaishia mchangani.

Rafiki yangu marehemu Jumanne Masimenti (Cosmopolitan FC, Simba na
National Team) siku moja tushakuwa wakubwa kanambia, ''Wee ungecheza
mpira gani bwana uko mazoezini sisi tunapiga danadana, wewe uko pembeni
ushavaa jezi unasoma kitabu. Mchezaji mpira gani anakwenda mazoezini na
vitabu?''

Matokeo ndiyo haya leo niko JF hapa nadarsisha historia.
 
nikiona sredi yako ni lzm niisome, kweli bro huchoshi kwa uandishi wako, pesa ilotumika kukusomesha haikufa bure kama ilivyo kufa iliyotumika kumsomesha jingalao.
Ninangale,
Ahsante sana kaka.
 
Chuwaa...
Siku hizi kuna mabadilo makubwa sana katika hivi vilabu hakuna tabia
ya kuwaleta karibu waliopita katika hizi timu kama viongozi, wachezaji
au washabiki maarufu.

Salaam zitafika In Shaa Allah.
Hii hapo chini niliandika hapa siku nyingi zilizopita:

Utangulizi

Kumekuwa na mjadala mkali sana kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika katika JF:

Angalia hapo:

Tuepuke sumu hizi: Brigedia Jenerali mstaafu Francis Mbena

Mjadala umevutia wachangiaji wengi na nimejibu kila swali lililokuja na kuweka rejea kadhaa, picha za zamani na ''links,'' kumsaidia msomaji kuijua histori ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.

Wengi wanahangaishwa na kusoma majina ya watu ambayo hayamo kwenye historia kama waijuavyo wao.

Ikafikia mahali nilihisi kuwa wametosheka.

Ghafla mjadala ukageuka ukawa sasa ni mimi kutukanwa matusi khasa.

Hapo ikawa tena siwezi kuendelea na mjadala kwani ni tabu kujibu matusi ndipo nikaamua kuja na haya niliyoandika hapo chini:

Mohamed SaidmahaliVerified User [emoji736]
[HASHTAG]#601[/HASHTAG]
31 minutes ago
Joined: Nov 2, 2008
Messages: 8,440
Likes Received: 1,872
Trophy Points: 280

Hii kauli kubwa na kauli thabit wenye kutaka kuelewe wataelewa wasio taka wataendelea kujitia ujinga na kuendeleza mabishano yasio na mantiki wala mashiko.

Hakika sheikh Muhamed allah amekuruzuku mengi ambayo wengi wetu allah ametunyima.

Hakika yeye ndio mwenye kila sifa na anestahiki kuabudi wa na kushukuriwa.

Sahimtz,
Majuzi hapa kulikuwa na Simba Day.
Nimekaa leo asubuhi na kuwaza vipi Simba ilikotokea.

Sijui kama Simba walifanya kisomo, yaani khitma ya kuwarehemu
viongozi, wachezaji na wapenzi wa club toka enzi za Sunderland.

Ikiwa walifanya kisomo naamini kabisa katika majina ambayo
yaliyotajwa moja litakuwa la Ayubu Kiguru.

Aliitwa Ayubu Kiguru kwa kuwa mguu wake mmoja ulikuwa na
athari.

Hii ilikuwa miaka ya 1960.

Mimi bado mtoto na nikipenda Sunderland na nikimjua Ayubu kwa
karibu sana na sababu ni kuwa Ayubu alikuwa na ubao wa biashara
Soko la Kariakoo na mjomba wangu Bwana Khamis Salum na yeye
alikuwa na ubao wake si mbali na ubao wa Ayubu Kiguru.

Ayubu alikuwa na sura jamil na alikuwa mweupe wa rangi.
Mungu alimjaalia Ayubu kipaji cha kuongea na kubishana.

Soko la Kariakoo enzi hizo lilikuwa moja ya vituo vya ushabiki wa mpira
Dar es Salaam.

Yanga na Sunderland walitawala soko na Yanga washabiki wao wengi
walikuwa na biashara ya kuuza samaki kiasi ikawa watani wao wakiwaita
Yanga, ''Wauza Samaki.''

Siku ya mechi ya Sunderland na Yanga moto ulikuwa unawaka sokoni pale
toka mapema asubuhi.

Ushabiki huo utaendelea kwa juma zima takriban baada ya mechi.
Sasa ikitokea kuwa Yanga imefungwa na Sunderland washabiki wa Yanga
walikuwa tabuni kwa juma zima pale sokoni wakipigwa makombora na
Ayubu Kiguru.

Ayubu
alikuwa na uwezo wa yeye peke yake kuwanyamazisha Yanga wote
pale sokoni kwa maneno yake, kejeli na kebehi lakini katika namna ambayo
mtu hawezi kughadhibika bali ni kucheka tu.

Enzi zile za Ilala Stadium kelele za kuzomea zikizidi kutoka upande wa Yanga
Ayubu atasimama kuwaelekea Yanga na atatoa maneno watu watacheka.

Yanga maneno yakiwaingia kisawasawa na sasa wamepwelewa hawana la
kusema basi watamwambia, ''Wewe Ayubu nani atakuweza bwana kiwete
wewe nyie mlojaaliwa na Allah ni mdomo tu.''

Jibu litakalotoka litamaliza ubishi wote watu watatawanyika watamuacha
Ayubu anapanga nyanya zake huku amevaa jezi ya Hamisi Kilomoni.

Ilikuwa Sunderland ikishinda Ayubu anachukua kikombe anakujanacho
sokoni anakiweka mbele ya ubao wake watu wanapita wanatunza.

Ayubu alikuwa akizoza lakini si kutokana na hamaki wala hasad ya nafsi.
Ilikuwa ndiyo kusherehesha ushabiki wa Yanga na Sunderlaand wala mtu
haendi Msimbazi Polisi kushitaki kuwa kabughudhiwa na Ayubu Kiguru.

Ayubu Kiguru hakuwa na maradhi ya nafsi ya chuki na husda kutaka nema
iliyo kwa Yanga iwaondokee.

Moja ya dalili za husda katika moyo wa mtu ni chuki na hii chuki huja baada
ya mtu kujidhihirishia ndani ya moyo wake kuwa fulani hamuwezi kwa lolote.

Kinachobaki ni kumwaga matusi na kumchukia.

Labda ''administrators,'' wa hii barza yetu wataliangalia hili la mtu hana kheri
ila kila aandikapo yeye ni kumwaga matusi.

ZOKqAPBmC8q1UbYrbXg59vBZeKzVpKf9Wu3ZBQKJRK8buK7jqXPlZbnYiXjFt74XQ95hda2vVKX8R6peFY-wpn-fcDMOHFgIl6E8IILuYKsSINjCYUQt9iTkttnzb96_Gz-kGjuTQyy2goQtOIFcx5H86rcRP7f1gI96PLk5FD3LudGalWSABrYM2TlVEf7v5sMXVRuyEFYPy8oKsHENjt-CvWIlXP7Yr8eGvaVgegBMHw7mlMwNYRqVdpzD0GSQr_lTQCEk2wSU7j_mxzJ5XcXBYDl31GPx2-CotchSWa5l2sBqVP18o-SRCZexCjWF4v_0ncn0zY0qyT-y3Io2XnxUvG194A9Mdr0BSKhb9XtlayuO5EqMA-0YlAqwkiWOXh3AJ6v4b8M9iPSAiNtIAO-Qj3gI9GcO59NapGKis4a395qK1xm_x4vOsICU4-o3dlqxzBii5aU9roRF6xMwac-dxeiD4spNY01V0JWdp8kLhoqk2aQHG_qArAKpKtmDnqJddC5fHD7flU8Z3q_UWDLGDJfQHe_lFEMbEcnkO_elbaKmiZ67UNQQ-hnMFANgHEpOqN8ySCSs11GQeubtFBzv7ehL7q8l=w596-h657-no

Ilikuwa ''ambition,'' yangu siku moja nivae jezi ya Sunderland lakini kipaji kilikuwa
kidogo nikaishia mchangani.

Rafiki yangu marehemu Jumanne Masimenti (Cosmopolitan FC, Simba na
National Team) siku moja tushakuwa wakubwa kanambia, ''Wee ungecheza
mpira gani bwana uko mazoezini sisi tunapiga danadana, wewe uko pembeni
ushavaa jezi unasoma kitabu. Mchezaji mpira gani anakwenda mazoezini na
vitabu?''

Matokeo ndiyo haya leo niko JF hapa nadarsisha historia.
Allah akuongoze ili udumu kuyafikisha yale uliyonayo kichwani mwako
 
Asante sana mzee Mwamedi Said, wakati ni ukuta. Ninavuta tastiest ya Captain akiwa uwanja ni
 
Kuna msomaji mmoja hapa JF nakumbuka aliwahi kumuasa ndugu yetu Yericko Nyerere pale aliposema:
"-Mimi sio mfuasi wa Mohamed Said
-Simpendi Mohamed Said kwa sababu ni mdini
-Lakini pamoja na yote hayo, Yericko huna ubavu wa kushindana na Mohamed Said kwa sababu pamoja na yote hayo, Mohamed Said anajua!" Mwisho wa nukuu isiyo rasmi.

I wish watu wazima na wazee wengi wangekuwa kama wewe Mohamed Said. Nchi hii wapo wazee wengi sana ambao ni wasomi huku wakiwa na utajiri wa historia za aina mbalimbali lakini wamezikalia! Na wengine hata ukiwauliza, huwa hawatoi ushirikiano!

Nakufananisha na babangu lakini kwa bahati mbaya yeye hakupata elimu kubwa kwahiyo anayoyafahamu ni yale at "regional level" yanayoendana na hadhi yake ya kijamii!

Ukimuuliza kuhusu historia ya Temeke na vitongoji vyake na yale yaliyokuwa yanaendelea enzi zao pamoja na majeshini; atakupa moja baada ya lingine ingawaje kuna swali moja hadi leo hajawahi kunijibu na sidhani kama atakuja kunijibu kwa sababu ni la uchokozi!

So, Mohamed Said unajua mambo na hufanyi hiyana ku-share na wenzako; hususani akina sie tusiofahamu A wala Be!

Sema hapo kwenye neno "Simba" ungekuwa unatumia maneno "katimu kamoja kanakopatikana Mtaa wa Msimbazi!" Nadhani ingefaa zaidi!
 
Mkuu Chige naona so busara kuingiza upinzani wa Yeriko na mzee Mohamed kwenye uzi huu.
Mambo mengine yaachie yapite tuendelee na burudani anazotoa mzee wetu.
 
Kuna msomaji mmoja hapa JF nakumbuka aliwahi kumuasa ndugu yetu Yericko Nyerere pale aliposema:
"-Mimi sio mfuasi wa Mohamed Said
-Simpendi Mohamed Said kwa sababu ni mdini
-Lakini pamoja na yote hayo, Yericko huna ubavu wa kushindana na Mohamed Said kwa sababu pamoja na yote hayo, Mohamed Said anajua!" Mwisho wa nukuu isiyo rasmi.

I wish watu wazima na wazee wengi wangekuwa kama wewe Mohamed Said. Nchi hii wapo wazee wengi sana ambao ni wasomi huku wakiwa na utajiri wa historia za aina mbalimbali lakini wamezikalia! Na wengine hata ukiwauliza, huwa hawatoi ushirikiano!

Nakufananisha na babangu lakini kwa bahati mbaya yeye hakupata elimu kubwa kwahiyo anayoyafahamu ni yale at "regional level" yanayoendana na hadhi yake ya kijamii!

Ukimuuliza kuhusu historia ya Temeke na vitongoji vyake na yale yaliyokuwa yanaendelea enzi zao pamoja na majeshini; atakupa moja baada ya lingine ingawaje kuna swali moja hadi leo hajawahi kunijibu na sidhani kama atakuja kunijibu kwa sababu ni la uchokozi!

So, Mohamed Said unajua mambo na hufanyi hiyana ku-share na wenzako; hususani akina sie tusiofahamu A wala Be!

Sema hapo kwenye neno "Simba" ungekuwa unatumia maneno "katimu kamoja kanakopatikana Mtaa wa Msimbazi!" Nadhani ingefaa zaidi!
Chige,
Ahsante sana nimecheka hii asubuhi ala kumbe wewe Kanda Mbili...
Ndiyo maana na mie nikakuchomekea - ''Wauza Samaki.''

Nia yangu ni kuhifadhi katika maandishi yale yote ninayokumbuka
wakati wa utoto na ujana niliyoyashuhudia hapa Dar es Salaam.
 
Hamfikii Nabii Yona
Kanali...
Hiyo hapo chini niliandika hapa Majlis alipofariki Athmani Kilambo ambae
alikuwa mtu wangu sana tukizungumza ''hours on end. '':

Abunwasi,
Siku zimekwenda.

Kwenye maziko ya Abdulrahman Lukongo nilikutana na Hamisi
Kibunzi
nikamweleza mazungumzo niliyokuwanayo na marehemu

Athmani Kilambo kuhusu yeye na Arthur Mambeta, Yusuf Salum
na wengineo.

Nikamwambia kuwa Yanga wakiwahusudu sana baadhi ya wachezaji
wa Sunderland na akinitajia majina.

Kilambo anasema, ''Unajua kulikuwa na watoto kule Sunderland wana
mpira mzuri sana kama Kibunzi na Arthur Mambeta na Mzee Mangara
akiwataka awalete Yanga kuongeza nguvu ulinzi na ushambuliaji...''

Kilambo anasema kuwa Mzee Mangara anatuuliza, ''Mimi nikamwambia
kuwa hawa watoto akina Kibunzi na Arthur hata tukiwaleta Yanga
hawataweza kucheza mpira huku wana mapenzi makubwa sana na
Abidjan.''

Siku zile jina lingine la Sunderland ilikuwa ''Abidjan,'' na sijui lilitokana
na nini.

Kibunzi
alikuwa hana habari hizi hata chembe.

Akacheka akanambia, ''Kilambo kasema kweli sisi tusingeweza kucheza
Yanga tukipenda sana Sunderland.''

Kilambo alikuwa mzungumzaji wangu mkubwa na akijua mie siipendi
Yanga sasa yeye ikawa kila siku kuniweka roho juu.

Mechi ya Yanga na Simba Zanzibar mwanzoni 1970s, Yanga walitokea
Nigeria, basi kanifata ofisini kunitisha ananiambia, ''Tumekufanyieni
fitna kubwa Zanzibar mnachukiwa kama Hizbu.''

Kweli Zanzibar tukafungwa Yanga wakachukua kikombe.

Kilambo alikuwa muungwana akiingiliana na wachezaji wa Simba vizuri
sana na akipenda sana kumtania Emmanuel Mbele ambae akipenda
kumwita, ''Fullup.''

m0AkTF7F_x7v3uUz2l23EpBUg-NuCixyFrth0Tb9uYA0crQq3KNKaXelEjFoRNlxHFUONs3932iil-jrro7ThdOFtCK4OJbIxeXITF01HigMjTKPcqpoNxAKuN0l192NamsWUTlv296Ip3oMJIexF0KtwXqD13xbZJPRayjMmnY4taN7X1TJ1DlLZiA5mzLXazFBLJAFseuk1P146pLPgvutcKSIT52ouzgr1BRO8FoAiEXBvuMUsSsojbL1zUNC0CZ7EtVwopylKgWKd3uPNGlk_zmL7Kt7N-2ZfZ37ltzp3OkmehLJGSUUBDC9bMcUVXAzaEf_Rkw-y_8lvWuaCeiQ7O8Igu9JksHFZ2RI6dHYce9X4yWhVwsdODcaOZTwo4wiSeCS5jgdbtppZtWMXn7TOyTQQ1VhZcRFkoPrFHXPFsuEGpBYONvF5kk4WVJsi3wYgcb8sTsv2608j8TLTonSeZSfD32Fehp36W0amrSqgS80S2BUncyiMsC379ii_fNZVYGfswq0h8bG5P1CV-62yKv9xQGueOrOuwR4Ezl_dhY-KLBKMNPSxeFR5B2XzcieroR0MEAm5G4eV-_4eT_iKhj-aXF6=w876-h657-no

Waliosimama wa tatu kulia ni Athmani Kilambo, wa tano Abdulrahman Lukongo
timu ya East African Cargo Handling Services

2016%2B-%2B1

Golikipa Athmani Mambosasa (Simba) kushoto ni Kitwana Manara na pembeni yake ni
Shaaban Baraza

Akijua mapenzi yangu ya mpira na alikuwa akinipa habari nyingi sana za
Yanga hadi uchawi wa kuloga mechi.

Siku za mwisho za maisha yake tukiswali pamoja msikiti wa Manyema na
akija akiniona hataingia ndani msikitini sharti kwanza aje anisalimie.

XGLv9aiIr6aRQxikp3KyYIemtMOzk4wiDYGsKgXZBPoBx4Lvnzjjj_6InCUxJztppvycitZbf2umdl3cwi2otJcRzl1hJLtu2xQ35G7TMOJFipVN3pKHhDroX68OGm3xwzGTyzR48CCGtpXeLcHyfZupQA59VUMTLmMaLGN_WbQboAzLy5hnvKjcxJgV6VL2gjat8eMsUBQy4aWaQcr_TaIhlumWzuirk9mnF5is52gCmRQ9zTHG8wjGPtBh98lVmZZf5iENiVLXjZztr5jBpEZp4Kwyr4XQU0hbb5B7C82D0nC99pQ_NpTtkbA-4qDlRw4uqBc9gnWofHNj3G8zq0XE4D29dOi9NimCBpBKelwss7pmrnLQsIoRyV04AI6E-oFCUf8ccuinwK38CKaLdNYZh8Mwx0WGGpbyl2jPyud94FeGevOVNw9MU_dPPvz6L93r1--UQJ9Gph7MGwMzre6RCDSVtZgZeWZ0S3pBw5xUILlU--LPdlxkCRii1dPHd0lr2eqFspgNUmM3cEGqSPzuPlUlmbJkW5j6bBrUHBA_NXeCJnkk1GBgZPreFpevwVR-iuE1Mt9EOFMMUSxO7duU-LsuljQ=w330-h220-no

Athmani Kilambo (Yanga) kushoto na Abuu (Cosmo)
kulia kwenye khitma Saigon.

cVvBeW3-lqa-Sd7MqUlDplfoUmWunLyb39y1HpawtAKj8pHw3WNTEvxKiA7ZuHrnEkYeEVbWdPmM7h8Rw-gNsWNRmTRpYU6speUv4RGaooeiDXtbuOocZ1LWjosiMRYnLYZn62Eh4pJLSJdr3B-xiMLsnnAhuVOAjrd7BgX6SseyklnKhX3y-VDeD0bTO4oM195dRkI1PIYApi75HUH9ngf-TaMlPe6CTf5NgWy3ESnwxwdaOJQFLhwLbSUph0eYR8UF1p4RuUjCzvy263-LMhD5ZyM850psRTbRLcEK_Qd4JFf0XTuF2ltLiUh3ROOadG7SBQNaXkaGEE_QtEnYx60z1GmE8kgaYqUHd8-teqAL4ck2RYet6xe-JM-72LAQzKWdJdOmIiVZdLUx4TNID7BtQaBN1umspcDn31bgc5eithBOHlhhDB6HdfYPEqK302gmwfDeq97AzPSuUDF4OwAdTGBLK-LvH-ZGkwTCNrmu1klTT_PPyFsnR8F_PF7ox0SEsPIAlXli5sMmBurAIgCYX5iAJTbzEiDvvXBu1njpIhTcUvrMcgJYYwT_BJ8Ypp0zmI7fg1U9BwmAnUiTedwbQw9XMog=w986-h657-no

Kushoto wa kwanza mbele ni Hamisi Kibunzi, nyuma kulia wa kwanza waliosimama ni Arthur Mambeta
anaemfuatia ni Emmanuel Mbele na wa sita ni Yusuf Salum.

Yanga ya AHSANTE KOTOKO: baba watoto Kilambo Athumani akiwa na beki Kapera na Boi Wickens wanapaki bus nyuma; GOALKEEPER Elias Michael na Centre half wao Abdulhaman Juma. Hiyo ndio Yanga ya Mangara Tabu!!!

Ndinani,
Abdulrahmani Juma
hakuwa ''centre half,'' watoto wa mjiini wakiita
''mkoba.

''Yeye alikuwa akicheza mbele na Yanga wakimuita ''Bwana Fedha.''
Abdulrahmani alikuwa na ''gentleman player,'' ''excellent ball control.''

Sasa pale katika alikuwa akigawa mipira kila mahali kama vile ''cashier,''
anavyolipa fedha ndiyo wakampa jina hilo.

Yanga hawakuwa na staili ya kuzuia lango yaani, ''kuegesha basi.''
Yanga walikuwa na wachezaji hodari wa kufunga kama Maulid Dilunga.

Kilambo kwa kuwa alikuwa more ''flamboyant,'' na mpira akiweza kuuchezea
yeye alikuwa ''stopper,'' akicheza mbele ya Kapera kwa kuwa Kapera
alikuwa ''stiff player.''

Kwa ajili hii Kapera akawa, ''swipper,'' yaani akipitwa Kilambo ''striker,''
atakutana na Kapera.

Hii staili wakiita ''double centre half'' yaani ''stopper na sweeper.''
Ndiyo maana Yanga walikuja kupata tabu sana kuwashinda Simba enzi za

Abbas Dilunga na Willy Mwaijibe kwa kuwa walikuwa wanashambuliwa
kutoka pembeni na ma ''winger,'' wenye mbio na wepesi.

Nitakuambia kitu ujue vipi Allah anawapa watu nema zake.
Huwezi amini lakini juu ya kuwa Kilambo alikuwa hana elimu ya sekula
lakini alikuwa hodari wa kujifunza maneno ya Kiingereza khasa yanayohusu
mpira.

Nimejifunza mengi kutoka kwake.
Yeye ndiye akinieleza tofauti ya ''placing,'' na ''shooting.''

Alikuwa akinambia, ''Mwambieni Sabu si kila mahali ni ''shooting,''
mmetukosa kutufunga kwa ajili mipira mingi ambayo angefanya placing
yeye ana shoot inakweda juu. Ile mipira ange-''place,'' yote yale magoli.''

''Hapakuwa na haja ya ''lobbying,'' pale. Yeye angepiga kweye ''box.''
Kilambo alikuwa ''sportsman,'' wakati mwingine baada ya Simba na Yanga
bila kujali matokeo yeye atafanya uchambuzi wake wa mechi.

Utamsikia anawalaumu Simba anasema, ''Nyinyi Simba mechi ya jana ndiyo
mmeiharibu.

Hivi yule Bobeya mnampangia nini?''

Bobeya
alianza kama mlinda malango Zanzibar kisha akaja Simba kama
''centre half,'' lakini yeye akitumia nguvu sana uchezaji wake.

Kilambo atasema, ''Pale nyuma wangekuwa Arthur na Kibunzi mpira
ungekuwa mzuri sana jana.''

Kilambo
hata alipokuja kuwa mwalimu wa mpira baada ya kustaafu soka
timu yake akiifunza kucheza staili ya Kibrazil.

Ulikuwa ukiongea na Kilambo unastarehe.
Utoto wake alikuwa Bagamoyo akivua samaki.

Akikupa strori za uvuvi utashika mbavu.
Jumapili iliyopita nilikuwa na Captain Malik kwa kipindi kirefu.

mEOhxVC2Q9uDHfYDI9LEDby5Lr9xRmniP6z3Y2hDOTDI8zf1REeJb1NoIWeTRCSbHOEeEncPKx3G-OqglU46ooz0BtyS2KSJOC0nZFthuUNKolPTMRnorID4HQm5rQ0jkG5kDYJGDJI-mw2nIxVAbX8bflgBbd4LpRhZkLg6tV_HmZjHekddgMvPOCJknM233HC6Zi749dxNkMoaTBIDks1mjl_3L3OBch_WLL_sPQN7xu97xQyhx7G61nA_de6Rw7dVT2vUa04KdgrxrTD3-xwZS60pId38VSKeXl2A0BNTq0A-3_NKZxaxjuK1qWxYP3l0g_VkzQTFhhtupjA123etbrOw2TeOAktSb_2YxKJhi4n05kP20jTKl_2qIvLQYrJblaJjCDo9O2PkzzIBMWUsj36P229caAGB9BF66G74Gkm8FHn-1CXQU0vga6S5Ds-pZUd-_edHjmP2wKJOqoYJAtp6LA6_ve4o5lkIe-qt4NQYZZJoAG6OVxWoMJTx93VNLuWckhUz5W19uNizqdu0ehC6LxAf5WaVR6K_wXWYGiZ7AVoTpbzBSPsFq0scTtkYzWkEjiWz96RAu0uVFCnnhz8PUU0i=w624-h657-no

Wa kwanza kulia ni Captain Malik
Captain Malik
alikuwa Captain wa Yanga nadhani katika miaka
ya awali ya 1960 na ndiye aliyempokea Kilambo Yanga akitokea
Bagamoyo na kumtia moyo kuwa anaweza kupata nafasi kikosi cha
kwanza.

Juzi alinihadithia mkasa uliotokea Ilala Stadium.

Yanga walikuwa na mechi na wachezaji wote walikuwa weshaingia
uwanjani lakini Kilambo alikuwa kachelewa.

Hakuna aliyekuwa anamjua Kilambo wakati ule hivyo akazuiwa lango
kuu ikabidi Captain Malik aende akampitishe mlangoni.

Sifa moja kubwa ya Captain Malik ni kuwa yeye ni Encyclopedia ya
historia ya mpira Tanzania.

hGe9HtLNYarjGzopFnmuyEuG-P3rXOQJPrrbsSFy_sNCvZgNttqWeFBcjIRYR1AN1xG3g8r3-6I=w891-h600-no

Kushoto: Boi Wickens, Captain Malik, Emmanuel Mbele na Khalid Abeid kwenye Khitma Saigon Club 2001
 
Back
Top Bottom