Car wash pembezoni mwa mlimani city

Mjuzi Wenu

Senior Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
108
Reaction score
108
Wakuu mimi ni kijana ambaye nina ujuzi wa kutengeneza magari licha ya kwamba sina uzoefu wa kutosha katika hii fani pia ni mwanafunzi wa mechanical engineering ngazi ya diploma.

Hivyo nimetokea kushawishika zaidi na kazi ya kuosha magari maana mara nyingi nikipita upande wa mlimani city pembezoni kuna car wash ambazo inaonesha kuna wateja wa kutosha na hii yote ikionesha kuwa hii huduma ni muhimu katika ile sehemu.

Hivyo wakuu nilikuwa naomba nijue kiundani kuhusu hii kazi na uwezekano wa kupata eneo maeneo yale ili niweze kufungua kakibanda cha kuoshea magari na kufanya service ndogo ndogo za magari mana nina ujuzi wa kiasi katika upande wa magari.
 
Sehemu nzuri ila kupata nafasi kisanga sana.

Nishazunguka sana hapo kutafuta sehemu upande wa Sinza huu kuna Carwash 3 moja inaitwa Arusha Express inajaza sana gari, inafata The Beast kuelekeza jengo refu nayo ina jaza kidogo, then inafata MlimaniCity Carwsha haina magarikabisa...

Ubaadhi huu kulipobakia kuzuri ni baada ya Arusha Express kama unaelekea Mwenge nyumba kama ya 3,4 ina space kidogo niliwai kuuliza mwenye nyumba kakataa, mbele tena kuna nyumba ina Banda bovu Force na hapo sikuona mwenye nyumba ila nahisi sio sustainable wanaweza kuuzia ma-Don.

Ukiondoa sehemu hizo hakuna sehemu nyengine kabisa labda mtu awe na Mtaji mkubwa sana aongee biashara na Carwash moja ubaadhi wa balabala ya kuelekea Ardhi university aijenge ya kisasa sehemu nzuri sana ila ipo local mpaka inasikitisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…