Nimeona kwenye mitandao ya kijamii video ya kijana akitapika damu wakidai kuwa tatizo ilo limemkuta baada ya kutumia dawa inayo itwa carbotoux je, taarifa hizi niza kweli?
- Tunachokijua
- Carbotoux ni dawa iliyo katika hali ya kimimika iliyotengenezwa mahsusi kwajili ya kutibu kikohozi. Dawa hii inatengezwa na kampuni ya PPM yenye makao makuu yake Cambodia.
Kufuatia uvumi wa dawa hii ya Carbotoux kutumiwa na watu na kusababisha madhara kama kutapika damu, Wizara ya afya kupitia akaunti yake rasmi ya Instagram imetoa tamko kuwa dawa hii haijasajiliwa nchini Tanzania pia kampuni ya PPM hajawahi kusajiliwa wala kusajili dawa yake yoyote Tanzania.
Vilevile Mamlaka ya chakula na dawa TMDA kupitia ukurasa wao rasmi wa X wamebainisha kuwa dawa aina ya Carbotoux ni dawa duni na ivyo watu watumie dawa zilizosajiliwa rasmi kwa matumizi kwa kuwa ni bora na salama kwao.
Je, video inayosambaa mtandao ikimuonesha kijana anayetapika damu akidaiwa kutumia dawa aina ya carbotoux ni kweli?
Video iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha kijana akitapika damu, haihusiani na tukio lolote la dawa aina ya Carbotoux.
June 28, 2023 WithAlvin alichapisha video hiyo kwenye mtandao wa X huku akimuombea kijana kwa kuwa alikuwa kapewa sumu.
Kijana huyo alikuwa Mnageria, ambaye taarifa zilizoripotiwa na waandishi wa habari wa Nigeria zilieleza kwamba kijana huyo alipewa sumu na rafiki yake siku ya sherehe yake ya kuzaliwa, hata ivyo kijana huyo alipoteza maisha baadaye akiwa hospitalini akipatiwa matibabu.
Kwahiyo, kutokana na vyanzo hivi video inayosambaa mtandaoni pamoja na sauti ikihusishwa dawa aina ya Carbotoux haina ukweli.