Na wanataaluma.....nina imani nimeingiliwa na kirusi fulani katika tarakilishi yangu inayonipa data zote za JF. kila mara kunatokea kipop up alert kinasema BN5.tmp is infected ni inaomba ruhusa ya kuzima tarakilishi yangu. Yamekuwa maudhi sasa. Kuna kipindi nilikuwa katikati ya ubishi na mbishi fulani hako kataarifa kakatokea na ikabidi nizime, nina imani jamaa alifikiria nimeshindwa hoja.
Naombeni msaada wa kuondoa tatizo hilo kwa mwenye taarifa.