Messi Lionel
Senior Member
- Jan 11, 2018
- 170
- 159
(CASEMIRO 14)
Los Galacticos ni neno la kihispaniola linalotafsiriwa The Galaxes(The Group of stars) kwa lugha ya Kiingereza au Kundi la Nyota kwa Lugha adhimu ya Mama zetu Kiswahili..
Hili ni jina la kujisifia la klabu bora kabisa na yenye mafanikio katika bara la ulaya Real Madrid au Royal Madrid kwani Real kwa kihispania ni Royal kwa kiingereza.. hujiita pia Los Blancos(the whites).
Jina lao linasadifu hayo yote kwani ndio klabu pekee iliyoshinda mataji mengi zaidi katika ligi ya nyumbani La Liga au Primera Division(first division) lakini pia Klabu Bingwa barani ulaya maarufu kama Uefa champions league ikiwa na mataji 12 kwa maana nyingine kama wakitengeneza saa yao ya mshale ya mfumo wa masaa 12(12-hour clock) basi kila namba linaweza kukaa kombe moja.
Lakini yote hayo yamekuja kutokana na aina ya uongozi walionao..mabenchi mbalimbali ya ufundi yaliyowahi kupita..lakini zaidi sana ni wachezaji mastaa waliopita.
Tangu nipate ufahamu wa masuala ya soka nimeona majembe wengi sana wakivaa uzi wa Los Galacticos tangu TEKA,SIEMENS MOBILE,BWIN hata FLY EMIRATES.
LAKINI kama ilivyo sera ya Rais wao ya kupendelea mastaa basi wamepita kina Zinedine Zidane,Michael Owen,Luis Madeira Figo,Steve McManaman,Roberto Carlos,Ronaldo Luis Nazario De Lima,Raul Gonzalez Blanco(prince),Arjen Robben,Wesley Sneijder,Clarence Seerdorf,Fabio Canavarro n.k
Lakini kwa miaka yote iyo bado timu ilikuwa inabebwa zaidi na ukuta kwa maana safu ya ulinzi Kipa Iker Casillas mabeki kina Michel Salgado,Fernando Hierro,Ivan Helguera,Daniel Carvajal,marcelo vieira,Sergio Ramos,Kepler Lima pepe n.k
Na tangu kuondoka kwa Claude Makelele basi Real Madrid imetaabika sana kumpata kiungo wa ulinzi ambaye aliistabilaizi timu hata walipojaribu kununua watu kama Mamadou Diarra, Lassana Diarra, Sami Khedira, Xabi Alonso n.k lakini bado tatizo lilitibiwa kwa kiasi kidogo sana
Lakini katika miaka ya Karibuni hatimaye Fundi wa soka Zinedine Zidane kocha wa sasa wa Real Madrid alipata suluhisho la tatizo baada ya Kufufua matumaini ya soka la kiungo mbrazil Carlos Henrique Venancio Casimiro au wao humuita Casemiro kutoka jiji la Sao Paulo,Brazil.
Alipofika hispania akitokea Sao Paulo ilionekana naye anakuja kujaribu tu pale waliposhindwa wenzake na ndio maana kuna muda walimpeleka Fc Porto pale Do Dragao Portugal kwa mkopo wa msimu mzima kwa faida ya kupata uzoefu na hapo alirudi tena lakini bado hakupewa nafasi kubwa na kocha Aliyekuwapo kwa kipindi kifupi Rafa Benitez(kocha wa sasa wa Newcastle the magpies).
Lakini Zizzou akampa nafasi kubwa ya kucheza nyuma ya Luca Modric na Toni Kroos na kwa kiasi kikubwa ile kazi ya Makelele(Wao wameibatiza jina Makelele Role) ikapata angalao mtu wa kuitendea haki Casemiro..
kwangu namuita ni Shujaa asiyeimbwa kwani kwa miaka 8 ya karibuni wamepita mafundi wengi kama Ricardo Izecson Leite "kaka'" Mwakapesa humwita Brother..Angel di Maria, Mesut Oezil, James Rodriguez, Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro, Gareth Bale, Karim Benzema,Sergio Ramos, Marcelo Vieira lakini ilihitajika sana uwepo wa mtu kama Casemiro kuweza kuisimamisha timu..
Casemiro ameshiriki katika harakati zote za kuifikisha fainali na kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa ulaya Timu yake katika miaka miwili mfululizo(2 yrs in a row) lakini pia ni sehemu ya kikosi kilichochukua ubingwa wa uefa msimu wa 2013/14.Bila kusahau pia amewawezesha Real Madrid kupata ubingwa wa La Liga kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano.
Anafanya kazi ya kukaba vema,anapiga pasi za karibu na mbali,analink vizuri na ukuta wake pia viungo wenzake lakini kubwa zaidi anashiriki katika upatikanaji wa magoli ya Real Madrid huku mengine akifunga yeye mf.ni goli alilomfunga kipa veterani Gianluigi Buffon katika final ya UCL mwaka huu(long range missile)..
Hata katika timu yake ya Taifa ya Brazil bado Casemiro amekuwa na wakati mzuri kwa game chache alizoitwa kuitumikia.. Inavyoonekana kwa sasa Madrid haiendi mbele mbele kwenye mafanikio bila ya Casemiro
Japo kuna mpiganaji mmoja wa Real Madrid anaitwa Daniel Carvajal lakini Casemiro kwangu namuweka katika ukurasa huu
[HASHTAG]#footballaddicted[/HASHTAG]