Ngida1
JF-Expert Member
- Aug 25, 2009
- 586
- 206
Dear All,
Mwezi uliopita tuliiona video moja hapa inayoonesha vipi watoto wanavyodhalilishwa mashuleni kwa kupigwa bakora. Wengi wetu tukasema kwamba mtoto Wakitanzania kama hujamchapa basi ushampotoa. Kwa kweli sisi wengine hatukubaliani na maneno haya, japokuwa tunakubaliana kuwa mtoto akikosa atiwe adabu, lakini adabu iwe nyepesi na sawa na kosa.
Hii hapa ni video ya shule moja huko Kilimanajaro. Kama wewe unao watoto nyumbani basi bora usiitizame hii video, kwani machozi yatakutoka kwa namna watoto wanavyotiwa adabu na walimu wao. Sijui mwalimu anaipata wapi hamaki ya kumpiga mtoto wa mwenziwe bakora 13 za nguvu. Mtoto analia na anamueleza mwalimu kuwa amemuumiza lakini mwalimu bado anaendelea kumcharaza bakora za mikononi.
Kuna organizations kubwa kubwa na church fulani inayoisaidia hii shule, lakini inasikitisha kuwa abuses kama hizi hawazikemei.

Last edited by a moderator: