Kwa akili ya kupambanua mambo haraka haraka naona Masoud hapa anataka kutuambia hivi: Hii MAGUMASHI DETECTER ni x-ray au microscope ya CCM (Rangi ya kijani). Kila mtu anajua kuwa kila mwana CCM husema kuwa ukimkata ngozi na wembe inatoka ''green blood''. Sasa fikiria mtu mwenye damu ya kijani anafananaje!!!Kwa hiyo rangi ya MAGUMASHI DETECTOR inajieleza yenyewe kuwa ni mtambo wa CCM!
Kwa hiyo MAGUMASHI DETECTOR ni chombo cha CCM ambacho kazi yake ITAKUWA KUCHAKACHUA MATOKEO YOTE YA KURA ZITAKAZOPIGWA HIYO SIKU YA TRH 31/10/2010. Hii MAGUMASHI imeandaliwa maalumu kwa ajili ya kupotosha,kubadili na kufuta karatasi zote za wale watakaopiga kura za kuwanyima CCM kura.
Lipumba aliwahi kuambulia kura sifuri (0) kwenye kituo alichopigia kura kwa maana kuwa hata yeye mwenyewe hakujipigia kura!!!!
Maana yake ni kwamba MAGUMASHI inabadilisha na kufuta kura zozote zilizo kinyume na CCM bila kujali hata kama umejipigia mwenyewe.
Hi MAGUMASHI ni hatari sana.
Namshukru Kipanya kwa kututahadharisha kuwa UWIZI WA KURA LAZIMA UTAKUWEPO NA UTAFANYWA NA WANA CCM(Rangi ya kijani).
Kinachotakiwa ni ulinzi wa uhakika ili kuzuia kura zetu wasije wakapata nafasi za kuziingiza kwenye mashine hili.
Safari hakuna kulala mpaka kieleweke.