Case File 2: Mahusiano yalianzia mtandaoni yakaishia kwa mwanamume kumwagiwa tindikali (True Story)

jerrytz

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
5,975
Reaction score
4,266
Tarehe 22 Mei 2018 taarifa ilitoka kwenye vyombo vya habari kuwa mwanamke anayeitwa Berlina Wallace, mwenye miaka 49 amekutwa na hatia ya kumjeruhi mpenzi wake wa zamani Mark van Dongen umri miaka 29, kwa kumwagia tindikali (acid) kiasi cha kumsababishia upofu wa macho na kumuunguza sura.

Taarifa hii ilitoka katika mahakama ya Bristol, nchini Uingereza.

Tutoke mahakamani, ngoja nikurudishe nyuma ya mkasa halisi wa mahusiano ya kimapenzi yaliyoishia kwenye kumwagiana tindikali(acid).

Mwezi Machi mwaka 2011 ndipo historia ya mapenzi kati ya Berlina na Mark ilianzia kwenye mtandao mmoja wa kimahusiano (dating site).

Wawili hao baada ya kuwasiliana kwa muda wakaona ni wakati sasa kuweza kukutana na kuanzisha rasmi mapenzi yao.

Tarehe 2 Agosti 2011 Berlina na Mark wakaanza kuishi kama wapenzi katika nyumba moja eneo la Westbury Park, Bristol, Uingereza. Mahusiano yao yalikuwa na changamoto kadhaa, ikisimuliwa kuwa Berlina alikuwa ni mtu mwenye hasira na kumfokea Mark mara kadhaa, na hata wakati mwingine kumrushia vitu pale wanapogombana.

Mahusiano yao yalidumu mpaka June 2015, wakati Mark kwa mara nyingine tena alipokutana na mwanamke mwingine anayeitwa Violet kwenye mtandao mwingine wa kimahusiano.

Yule mwanamke akagundua kuwa Mark ana mahusiano na Berlina, hivyo akamwambia kuwa sharti pekee la yeye kukubali mahusiano na Mark, ni pale tu Mark atakapomuacha Berlina.

Mark akaanza taratibu za kuachana na Berlina, jambo la kwanza ilikuwa Mark kuhama nyumbani mitaa ya Westbury na kwenda kuishi mahali kwingine.

Pili akamwambia Berlina kuwa, yeye Mark ameamua kusitisha mahusiano, hivyo uhusiano kati yao umefikia tamati. Habari ya kuachana na mwisho wa mahusiano haikuwa njema kwa Berlina, alilia na kutishia kujiua.

Tarehe 2 Julai mwaka 2015 Berlina alikimbizwa hospitali baada ya kunywa vidonge vingi kwa nia ya kujitoa uhai, bahati nzuri aliwaishwa hospitali na alipona.

Baada ya kutoka hospitali Berlina alikuwa akimtumia Mark meseji na hata barua za vitisho mara kwa mara. Mark aliamua kuripoti polisi, baada ya hapo polisi wakamzuia Berlina kuwasiliana na Mark kwa namna yoyote ile, na iwapo atakiuka basi atapata adhabu.

Maisha yakaendelea huku hali ya kiafya ya Berlina ikiwa mashakani haswa afya ya akili. Marafiki wakatoa ushauri kuwa anahitaji kumuona daktari na mtaalamu wa saikolojia ili aweze kusaidiwa.

Tarehe 22 Septemba 2015 , majira ya ya saa 12 jioni, Mark anafika katika mtaa wa Ladysmith Road, Westbury nyumbani kwa Berlina. Hata hivyo ilishangaza wengi, kwanini Mark aliamua kwenda nyumbani kwa Berlina jioni ile. Mark aliimbia polisi kuwa alikwenda kwa Berlina kama rafiki ili kumshauri apate msaada kwa ajili ya tiba ya afya ya akili. Lakini aliongeza kuwa alikuwa pale kumhakikishia Berlina kuwa yupo tayari kutoa fedha ama kuchangia gharama kwa ajili ya tiba. Huu ukawa uamuzi mbaya zaidi katika maisha ya Mark.

Ajabu zaidi, Mark aliamua kulala nyumbani kwa Berlina japo wote Berlina na Mark walithibisha kuwa walilala vyumba tofauti.

Majira ya saa 7 usiku, Dokta Nic, anayeishi karibu na nyumba ya Berlina, alishtushwa na kelele za mtu anayelia huku akiomba msaada akisema ‘’tafadhali nisaidieni’’, anasema alivuta pazia na akaona mwanamume aliyevaa boxer tu amesimama pembeni ya barabara akiwa analia. Muda huu pia alikuwa akitaja jina la Berlina kuwa ndiye amemwagia kimiminika kinachompa maumivu makali.

Majirani wengine walipoamka ndipo wakapiga simu 999 kwa ajili ya msaada wa Ambulance.

Wakati wakisubiri ambulance waliamua kumwagia maji maana ni wazi kuwa waligundua itakuwa amemwagiwa kimiminika chenye sumu maana ngozi na nyama za mwili maeneo ya usoni vilikuwa vikimeguka kama udongo, lakini pia Mark alilalamika kuwa haoni, macho yote mawili yalikuwa yameshaliwa na acid.

Afisa wa polisi Thomas Green ndio alikuwa wa kwanza kufika kwenye tukio na kukuta sehemu kubwa ya mwili wa Mark ikiwa na majeraha huku nyama zikiendelea kuungua na damu nyingi kutoka.

Mark alikimbizwa hospitali wakati polisi wakielekea nyumbani kwa Berlina kujua kilichotokea.

Polisi walipofika kwenye nyumba ya Berlina, walishangazwa kuona Berlina akiwa hana wasiwasi kabisa.

Contabo Mathew Griffin, akamuuliza ‘’ unamfahamu mtu anayeitwa Mark van Dongen? Berlina akajibu ‘’ndio namfahamu na alikuwa hapa dakika chache zilizopita’’

Konstebo Mathew akauliza ‘’Umemwagia nini mwilini mwake’’; Berlina alikaa kimya kisha akajibu ‘’ni sulfuric acid’’;

Afisa wa polisi Mathew akashusha pumzi na kuwapigia polisi walioondoka na Mark kwenye ambulance kuwa ‘’Mark amemwagiwa sulfuric acid’’, wakati huo polisi wengine wakakuta chupa yenye lebo ya sulphuric acid na kikombe.

Berlina alikamatwa na Mark akafikishwa katika hospitali ya Southmed iliyopo Bristol kwa ajili ya matibabu. Kwa namna alivyokuwa ameumizwa na acid Mark alikuwa na hali mbaya sana hivyo akawekwa chumba cha wagonjwa mahututi.

Iliwachukua polisi siku kumi kuipata familia ya Mark iliyokuwa ikiishi nchini Uholanzi na kuwaeleza kilichotokea kwa Mark

Baba na kaka yake na Mark wakasafiri kutoka Uholanzi kwenda Uingereza, walipofika hospitali walishindwa kabisa kumtambua Mark kwa sababu sura ilikuwa imeharibika vibaya.

Mark alidumu kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kwa muda wa miezi miwili. Kwa kipindi chote hichi Mark alipitia maumivu makali, kuchanganyikiwa na madhira mengine. Alipoteza mwonekano wote wa usoni.​

Baada ya kukaa kwenye maangalizi maalumu huku akipata matibabu, hali ya Mark ilizidi kuwa mbaya.

November 26 mwaka 2016 Mark anasafirishwa kutoka Uingereza kwenda Uholanzi kuungana na familia yake.

Tarehe 31 Desemba mwaka 2016 Mark anaomba achomwe sindano ya kifo ili apumzike kutokana na mateso na maumivu anayopitia.
Baada ya majadiliano na familia pamoja na wanasheria, upande wa serikali unakubali ombi la Mark kuchomwa sindano maana maisha yake yamekuwa ya maumivu makubwa.

Tarehe 2 January 2017 majira ya saa 3 asubuhi Mark anaagana na ndugu zake, maafisa wa hospitali wanafanya maanadalizi ya kumchoma sindano . Saa 5 asubuhi Mark anachomwa sindano na kufariki.

Turudi kwa Berlina na kesi yake

Berlina akafunguliwa mashtaka na hatimaye akahukumiwa kifungo cha maisha jela tarehe 22 Mei 2018.
Ikagundulika kuwa alinunua chupa ya sulphuric acid yenye ujazo wa Lita 3 kupitia mtandao wa AMAZON.

Baba wa Mark akaanzisha kampeni ya kuzuia uuzwaji holela wa sulphuric acid na hatimaye serikali ya Uingereza ikapitisha sheria ya kuzuia uuzwaji holela wa kimiminika hicho. Kwa sasa unahitaji kibali maalumu kuuza na kununua sulphuric acid nchini Uingereza.
 
Attachments

  • Glass ya sumu.png
    Glass ya sumu.png
    717.1 KB · Views: 23
  • kitanda alicholala mark.jpg
    kitanda alicholala mark.jpg
    92.9 KB · Views: 31
  • mark na baba yake.jpg
    mark na baba yake.jpg
    49.7 KB · Views: 29
  • sumu.jpg
    sumu.jpg
    88.7 KB · Views: 27
Daah Dunia yetu ina kila aina ya tukio. Pole kwa kijana Mark na aendelee kupumzika salama
 
Ok
 
Chai
 
Berlina anaroho mbaya sana,kama alikuwa anampenda sana mark asingekuwa mkorofi na mbabe hadi mark akaamua waachane,ila nae mark kajitakia matatizo alirudi kwa ex kufanya nini angamuacha apambane na hali yake
 
Nimetoka kum google Berllinah Wallace,kwa muonekano ni wazi alikuwa ana matatizo ya kisaikolojia
 
Back
Top Bottom