Case study: Waliosoma english medium ni "wazuri" kuliko waliosoma shule za kawaida

Hivi Kiswahili ni lugha yetu ya asili au tumeamua kuifanya yetu tu? Kwangu Kiswahili na Kingereza vyoto vina tamaduni za nje
 


English is better mate since we use it all way long in higher school and work, we need it from primary to make our tongue easier expressing and to a better understanding, having Swahili just at primary and not using further more studying at secondary, its no point from first place, it's worth ----le, you know what I mean?. anyways, In the End, we are who we are. By the way, your English is sweet, hope your accent is just as good as you expressed (its not a compliment dude) but I still owe you one, lol.
 

una point nzuri lakini we jamaa kingereza chako yaan mpaka nakuhurumia, usishike dictionary na kukariri maneno, unataka kujua kingereza vizuri, zama kwenye muvy zao na muziki, usikariri vitini na dictionary, it's totally off. samahani kama ntakua nimekukera au kukukwaza, ni maoni yngu tu ili ufanikiwe zaidi kwenye uandishi na kuongea boss.
 

UMESEMA UKWELI KABISA, LUGHA YA KINGEREZA SIYO SULUHISHO LA KUBORESHA USHINDANI KTK SOKO LA AJIRA, mimi kiingereza changu cha kuongea ni POOR - AVERAGE, lakini ni kiwango ambacho ninawazidi Wajerumani , Waholanzi, Wagiriki, Wajapani na Warussi ndyo kabisa kule naweza kuajiliwa nikawa Mwalimu wa kiingereza chuo kikuu, ukiancha waingereza wenyewe, wananchi ambao ni wasomi ktk nchi nyingi za Ulaya Ki-english chao ni cha kuungaunga tu, lakini wako vizuri sana ktk fani zao walizosomea?
 

Obviously, you either have not understood the mere gist of my post, or did not address it, possibly both.

I haven't said whether English or Swahili is better. In a globalized workforce, English is a tool that one can certainly not ignore.

My point is, for those who think that English is better, how sure can they be that this advance we see among some in English is due to the English medium schools and not the home environment and other factors that is ascribed to those in the socioeconomic bracket that could afford to go to English medium schools?

I noted that correlation does not equal causation.
 

Mimi ni mshabiki na mpenzi wa Kiswahili kwa sana, nishakichambua Kiingereza na kukiona hakina logic kama Kiswahili, kwa kutumia nukuu za George Bernard Shaw at that. Nonetheless, kujilinganisha na Wajerumani, Wagiriki, Wajapani, Warusi is a bit of a stretch.

Mjerumani anaweza kusema hahitaji sana Kiingereza kwa sababu akitaka gari liliotengenezwa Ujerumani, lenye manuals za Kijerumani na system yote iwe imeandikwa Kijerumani anaweza kupata.

Scratch gari, anaweza kupata mitambo ya kiwanda cha kutengenezea gari iliyoandikwa kwa Kijerumani tu.

Sie tumeshatengeneza microwave oven yenye manual na dials za Kiswahili?
 
Asante kwa kunihurumia lakini kunihurumia bila kunisahisha hainisaidii kitu. Nasubiri masahisho yako. Kama unaamini Kiranga alijifunza lugha kutokana na movies na nyimbo za Marekani (labda kuna tofauti kati ya 'movies' na 'muvy' kama ulivyoandika) nashindwa jinsi ya kuuchukulia ushauri wako. Kiranga anaweza kuwa alipata mwanga mkubwa wa lugha kutoka kwenye filamu za marekani lakini bottomline Kiranga ANASOMA na ANAPENDA KUSOMA. Acha porojo za filamu.
 
Ni kweli, nakubaliana na mtoa hoja. Zamani ndio ilikuwa sio tija sana wakati shule za serikali zikiwa na waalimu na vifaa walau mpaka mwishoni wa 199_. Lakini kwa hizi shule za kata na walimu wa crash program ni bora english medium
 

Kama nilieleweka kwamba nimejifunza lugha kwa movies na muziki tu, hilo ni kosa. Nimeeleza kuhusu literature. Nimesoma kuanzia the pulp fiction of Mills & Boon mpaka James Hadley Chase, kuanzia mashairi kama "The Ancient Mariner" mpaka Joyce's "Ulysses" na Homer's "The Illiad", Stephen Hawkins mpaka Ian Fleming, Robert Ludlum mpaka Jeffrey Archer, Frederick Forsyth mpaka Maeve Binchy kabla ya ku graduate O-Levels nikawa nishamaliza my quota of fiction for three lifetimes (labda ndio maana sisomi fiction sana siku hizi).

Kwa hiyo hii notion kwamba Kiranga amejifunza Kiingereza kwenye MTV na CNN is a half truth.

Shout out to Julius Mushi who always had a soft heart for any Tambazan mischief, so long as it was commited with a novel in one's hand.

I will always remember what he used to say "Never get caught with time on your hands and no good book to read".

With all these gizmos nowadays, I am thankful to be able to carry an entire library with me.
 
Ni kweli, nakubaliana na mtoa hoja. Zamani ndio ilikuwa sio tija sana wakati shule za serikali zikiwa na waalimu na vifaa walau mpaka mwishoni wa 199_. Lakini kwa hizi shule za kata na walimu wa crash program ni bora english medium

Hii ni point muhimu sana katika kuijibu kwa sehemu ndogo hoja yangu ya "imekuwaje Kiranga aliyesoma shule za serikali kaweza angalau Kiingereza cha kuombea maji halafu wanafunzi wa leo washindwe vibaya kabisa".

Kile ambacho ningependa kujua ni kuona wanafunzi wanaotoka katika socioeconomic backround ya kuweza kumudu kusoma English medium, ambao hawasomi English medium, uwezo wao wa kusema na kuandika kiingereza ukoje?

That is assuming there is such a crowd remaining.
 
Najua tunapenda kiswahili kitumike kufundishia mashuleni lakini kwa mfumo wa elimu yetu uliopo, hupatakua na tija.
Nakubaliana na Tuko kwa kiasi fulani juu ya umuhimu wa watoto kusoma english medium kwa sababu:-

1. Masomo ya sekondari yanafundishwa kiingereza, na jinsi unavyokua na uelewa mkubwa wa lugha ina maana utaelewa zaidi kinachofundishwa.

2. Jamii yetu kwa asilimia kubwa tunaongea kiswahili, hii inafanya mtoto anaesoma shule za kawaida kuwa na kazi ya ziada kuwa vizuri kwenye kiingereza kutokana na mazingira yanayotuzunguka. (Kuna nchi watu wanaongea kiingereza kiasi kwamba hata kama hujaenda shule, lazima tu utaongea kiingereza kwa sababu asilimia kubwa wanakitumia)

Kwa kuwa tunafanya kazi na makampuni ya watu binafsi kutoka mataifa mbalimbali na kwa kuwa kiingereza ndio lugha inayotumiwa na makampuni hayo kuanzia kwenye usaili, ni wazi kwamba watu wenye uwezo wa kutumia kiingereza vizuri wataonekana kupata kipaumbele kwenye kuchaguiwa kupata kazi hata kama uwezo wao kiutendaji sio mzuri, wakati wa usaili hakuna muda wa kuonyesha ueledi wako wa kazi kwa vitendo. Unachofanya ni kuwashawishi tu kwamba uko safi.

Kama tunataka tutumie kiswahili mashuleni, inabidi tubadili mfumo wote wa elimu, tuweke msisitizo kwenye vitu vichache tunavyoviweza. Kwa mfano kuwafundisha watu Kilimo, Ufugaji, Ujasiriamali kwa kiswahili ni rahisi ukilinganisha na kufundisha masomo kama ya elektroniki, kompyuta, kwa kiswahili (Huwezi kukwepa kiingereza kwenye hayo masomo).

Ni kweli kiingereza hakimaanishi ufanisi au utendaji bora wa kazi lakini kina umuhimu sana kwenye kukupa ujasiri kwenye jamii na maeneo ya kazi.
 
Mmmmh!!!, we jamaa kwa kizungu ni noma, I am proud you can speak my mother tongue.
 
Mmmmh!!!, we jamaa kwa kizungu ni noma, I am proud you can speak my mother tongue.


Bebe nang'ho!

Sio hatari wala nini, cha kawaida tu. Tatizo inawezekana viwango vyetu viko chini sana kiasi mtu anayeandika Kiingereza cha kawaida tu, kisicho exceptional in any way lakini kizuri, kinaonekana cha juu sana.

Hakuna shortcut, kusoma sana, kujifunza sana, kujenga msuli wa msamiati na ufasaha kwa miaka nenda miaka rudi, mawazo ya uchunguzi ambayo hayatachoshwa na mfumo wa ajabu wa lugha hii, matokeo yatajionesha.

Halafu kama alivyosema mdau hapo juu, zamani kidogo unaweza kumkuta Mwalimu Lulindi kaingia darasani anaanza kukueleza kuhusu Socrates na falsafa zake (form one hapo), unataka kujua zaidi huyu Socrates alikuwa nani, unakuta vitabu vyote vinavyomuelezea Socrates ni vya Kiingereza, na wewe unataka kujua, inabidi usome tu, hata kama kwa kamusi pembeni.

Siku hizi shule za kata unaweza kukuta huyo mwalimu mwenyewe wa vodafasta hajawahi kumsikia Socrates!
 
I am college graduate, lakini sasa hivi ukija nyumbani kwangu utakuta Vitabu kadhaa vya James Hadley Chase, yaani ndio nimeanza kuvisoma hata mwaka haujaisha, Nimeshangaa sana nilisoma kuwa wewe ulivimaliza hata kabla ya kumaliza O-LEVEL( These are more than 88 books), you deserve the English you have.

OLI LI SHINO NKOYI.
 
"Da watu mnatema ung'eng'e kama hamna akili nzuri".

Basi nakiogopa kiingereza nisije semwa sina akili nzuri.
Kuna watu wanapiga kingereza acha bhana, huwezi amini kama ni mbongo I see, mpaka akiandika kisukuma ndio unaweza kuamini, ni noma sana.
 
Mtoa mada upo sahihi kabisa..

Kiswahili kimechangia sana kutunyima confidence watanzania na hata wawekezaji wanatuona vichwa maji..

Hakuna chochote wakenya wanachotuzidi zaidi ya lugha ya malkia..

Lakini cheki sasa wakenya walivyojaa Tanzania katika makampuni ya kigeni kuchukua nafasi zetu..

Nenda kafanye utafiti na Kenya kuna watanzania wangapi waliochukua nafasi za wakenya..

Watoto wa english medium wana advantage sana sokoni hata kama ni average student..

Ukimchukua mtu aliyesoma kayumba ambae ni kichwa kweli kweli like To na then umchukue average student aliyesoma english medium then uwapambanishe katika usahili, kazi, kujiamini, kujenga hoja etc uone nani mshindi kama sio academia..

Mifano hai ipo kibao bila hata majungu
 

Now now now now, namaanisha nilimaliza kusoma vitabu fulani vya Chase.

Ningevipata vyote probably ningeweza kuvimaliza, lakini sikubahatika kuvipata vyote. Chase had that page turning style ambayo nilikuwa naipenda sana, it is addictive.

Sasa mtu kama wewe una vitabu hivyo, kama una watoto hapo nyumbani, wanaanza kuona mazingira ya vitabu nyumbani (although some of the Chase covers are not exactly child friendly, but in any case I am referring to books in general).

Kwa mtoto mdadisi, yale mazingira ya nyumbani yanaweza kuwa stimulant kubwa ya kujua lugha kuliko hata shuleni.

Mimi nakumbuka nilivyokuwa mdogo nilikuwa nasoma mpaka Engineering plans zilizokuwa nyumbani, sasa hapo mtu unaanza kupata udadisi kuhusu hizi plans zinasomwaje, hivi vialama vina maana gani etc kabla hujajua trigonometry.

Ndiyo maana naona umuhimu wa kuhoji hii dhana ya kutafsiri "watoto wanaoenda english medium wanajua zaidi kiingereza" kumaanisha kwamba english medium schools zinawapa advantage ya kujua zaidi kiingereza.

Obviously kufundishwa kwa kiingereza kunachangia, lakini kwa kiwango gani? Na kiwango gani kinachangiwa na mazingira ya nyumbani?

Inawezekana mtu kwao wana Time Magazine subscription, akiwa bored anajisomea, anajenga msamiati na uelewa wa Kiingereza, halafu akija kuonekana anajua, sifa zinaenda kwenye english medium school.
 
Ukisema Shule za English Medium zinatoa wanafunzi competent kwa kuwa walimu wake ni wazuri kwa kuwa wanalipwa vizuri na miundombinu ya kusomea ni mizuri zaidi ukicompare na st Kayumba nitakuelewa! Lakini ukisema kwa sababu ya Kiingereza hapo sikubaliani na wewe hata kidogo, maana kama jitu bomu hata liongee kiingereza kiasi gani kama halijui vitu ni halijui vitu tu.

Ushauri wako kwa serikali ungekuwa ni kuboresha miundombinu ya kusomea ikiwemo na maslahi mazuri kwa walimu na Kuabadili sifa wanazozitumia sasa kupata walimu hapo nitakuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…