Leo tena nimerudi kuleta andiko langu kuhusu Cashless itakavyoongeza pato la Taifa.
Kwa hali ilivyo nchini kwetu hakuna kitu kinachotuzuia kuachana na matumizi ya fedha Taslimu kwenye malipo mbalimbali. Ili serikali ikusanye mapato vizuri inabidi kulazimisha wafanya biashara wote na makampuni yote nchini kutopokea malipo kwa fedha tasilimu na badala yake malipo yote yafanyike kwa simu.
Serikali itengeneze sera kwamba kila mfanyabiashara au mkubwa au mdogo awe na lipa namba kwa ajili ya kupokelea malipo mbalimbali.
Pia line za simu kwenye menyu ya kulipia bidhaa ziwekwe bei za bidhaa mbalimbali zinazouzwa nchini, halafu mteja anapolipia bidhaa mtandao unakata kodi ya bidhaa kwenye fedha itakayolipwa kwa muuzaji halafu kiasi kinachobaki baada ya kodi kinabaki kwa muuzaji.
Hapa mnunuaji asikatwe tozo ya kurusha muamala na badala yake kodi na tozo ikatwe kwenye bei ya manunuzi.
Namna nyingine kama njia ya pili haitakuwa nzuri seriakali iweke kiwango kwamba kwenye kila shilingi 100 itakayoingia kwenye akaunti ya muuzaji serikali itakata sh 5 ya kodi. Kwa kila 1000 sirikali itoze sh 50...huo ni mfano tu.
Ukiangalia mahesabu hayo ukilinganisha na idadi ya miamala kwa mwezi, serikali ingeweza kupata pato kubwa sana. Mimi ninaamini kwamba simu ni migodi isiyohitaji nyundo na surulu kupata pesa badala yake ni kutengeneza mifumo tu ambayo sio kandamizi.
Mfumo huu utaipatia serikali mapato mengi sana: Hapa natahadharisha seriakali isiingiwe na tamaa ya kuweka tozo kubwa sana, serikali inaweza kutoza kodi za vishilingi vichache lakini kwa idadi ya miamala serikali inaweza kuingiza kiasi kikubwa cha fedha na kuwezesha utekelezaji wa miradi mikubwa pengine bila hata kukopa.
Naomba kuwasilisha.

Upvote
4