Cassper Nyovest: Rapa pekee kutoka Afrika Kusini anayemiliki ndege Afrika

Cassper Nyovest: Rapa pekee kutoka Afrika Kusini anayemiliki ndege Afrika

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
vllkyt217rt8m4d9ng.4a6db7cd.jpg

HAKUNA ubishi kwamba Cassper Nyovest ni miongoni mwa marapa wakubwa zaidi Afrika Kusini kwa sasa kutokana na mafanikio aliyoyapata kwenye muziki toka mwaka 2009, alipoanza kujulikana zaidi.

Kwa Afrika Kusini, ndiye mwanamuziki pekee aliyefanikiwa kujaza mashabiki kwa shoo ya peke yake kwenye uwanja wa michezo wa Dome unaobeba watu 20,000 (mwaka 2015) na mwaka 2016, wanja wa Orlando, wenye uwezo wa kubeba watu 40, 000.

Lakini pia kwa ngoma kali zikiwemo Doc Shebeleza, Tsibip, Mpumakim na Mama I Made pamoja na kolabo kubwa zikiwemo alizofanya na wanamuziki Vee Money (Tanzania), Diamond Platnumz (Tanzania), Davido (Nigeria), Talib Kweli (Marekani), The Game (Marekani) na Casey Veggies (Marekani), tunaweza kuelewa ni kwa nini jamaa ameweza kuliteka gemu la Muziki wa Hip Hop, Afrika.
DQnTQ3vXUAAYaIG-1.jpg

Kwa Cassper, mkwanja mrefu anapata kupitia shoo, mauzo ya albamu, kampuni yake ya Familly Tree, ambayo ni lebo ya muziki pamoja na media ya habari, dili kutoka kwa makampuni ya Castle Lite, KFC, MTN, AG Mobile pamoja na kinywaji cha Ciroc Vodka, ambacho anakitangaza.
Utajiri wake kwa jumla unatajwa kufikia dola za Kimar-ekani milioni 3 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 6.8 za Kitan-ania. Wengi wana-weza kujiuliza kutokana na fedha zake maisha yake ya ‘luxury’ yanakuwaje, vipi kuhusu nyumba, magari anayoendesha na vitu vingine, sasa sikia;

Mbali na kumiliki majumba kadhaa ikiwemo aliyowanunulia wazazi wake, Cassper, nchini Afrika Kusini anaishi huko Kyalami, jijini Johannesburg, kwenye jumba lenye vyumba vingi, studio pamoja na bwawa la kuogelea lililomgharimu takribani Randi milioni 10 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.8.
Cassper-did-not-buy-a-new-Rolls-Royce.png

Rapa huyu anayemiliki albamu kadhaa zikiwemo Refiloe, Tsholofelo na Doc Shebeleza, anamiliki magari kadhaa yakiwemo BMW, magari mawili aina ya Bentleys na Rolls Royce.

Screen-Shot-2018-01-08-at-05.09.49.png

NDEGE BINAFSI
Cassper anaendelea kuonesha kwamba ni mtu anayependa vitu vizuri. Sasa kwa Afrika ni rapa pekee anayemiliki ndege binafsi aina ya King Air B200 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 1.7, (zaidi ya bilioni 3) aliyonunuliwa na kampuni ya kinywaji cha Ciroc Vodka mara baada ya kuingia nao mkataba.

Pamoja na yote hayo kutokana na kukua kwa muziki wake, akiwa na miaka 27 tu, Cassper anatazamiwa kuwa miongoni wa wanamuziki matajiri zaidi Afrika ndani ya miaka michache ijayo kutokana na kipato chake kukua kwa kasi.
Katika miaka miwili iliyopita, utajiri wa Cassper ulikuwa unatajwa kuwa dola za Kimarekani 800,000 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1. 8, lakini kwa sasa yupo mbali zaidi kutokana na dili anazopata kila kukicha na muziki wake kuzidi kukubalika zaidi. Kwa hiyo tutegemee mengi kutoka kwake.
 
Huyu jamaa nae pamoja na jina kubwa alilonalo lakini ana tabia za kswahili swahili tu.

Nilicomment kwenye page kuwa hawezi kufikia level ya AKA, jamaa lilivyokuwa puuzi eti lika ni block.

Ni lifala kweli kama bashite.
 
Dini inahusikaje ivi kwenye mafanikio ya msanii, maana ukiskia msanii anahela nying tu bas ujue ni Mkristo. Shida iko wap kwa waislam, mbona tupo nyuma??
 
Huyu jamaa nae pamoja na jina kubwa alilonalo lakini ana tabia za kswahili swahili tu.

Nilicomment kwenye page kuwa hawezi kufikia level ya AKA, jamaa lilivyokuwa puuzi eti lika ni block.

Ni lifala kweli kama bashite.

Alikuuliza kama anataka kufikia level ya AKA??

Kungekuwa na block hapa na mimi ningekublock. Kumuunga mkono
 
Huyu jamaa nae pamoja na jina kubwa alilonalo lakini ana tabia za kswahili swahili tu.

Nilicomment kwenye page kuwa hawezi kufikia level ya AKA, jamaa lilivyokuwa puuzi eti lika ni block.

Ni lifala kweli kama bashite.
Hapo ulipomfananisha na Bashite umenifurahisha sana Mkuu.
 
kuna mmoja naskia an billion 10 hapa home,nyovest hamwezi
 
Ndege ina bei hiyo ,ye anakodishiwa hasa anapokua na promo umbali mrefu wa hiyo kinywaji.
Kumiliki ndege mchezo?kina PDidy na 50 senti mpaka leo wanaishia ku-act tu na ndege.
May TMT peke yake ndio kajikomboa
..Bongo..Chid Benz katoka katika Mabenzi hadi katika Baiskeli...ha ha
 
Huyu jamaa nae pamoja na jina kubwa alilonalo lakini ana tabia za kswahili swahili tu.

Nilicomment kwenye page kuwa hawezi kufikia level ya AKA, jamaa lilivyokuwa puuzi eti lika ni block.

Ni lifala kweli kama bashite.
Kwa mtazamo wangu naona wewe ndio Mswahili. Haiwezekani utoke tu from nowhere ukapige ramli kwenye kurasa ya jamaa tena ukiingizia na habari za A.K.A ambaye hausiani kabisa na hiyo page.
 
Ndege ina bei hiyo ,ye anakodishiwa hasa anapokua na promo umbali mrefu wa hiyo kinywaji.
Kumiliki ndege mchezo?kina PDidy na 50 senti mpaka leo wanaishia ku-act tu na ndege.
May TMT peke yake ndio kajikomboa
Sijui kwanini lakini mimi siwezi kuandika post kama yako bila kufanya utafiti kwanza.
 
Kwa mtazamo wangu naona wewe ndio Mswahili. Haiwezekani utoke tu from nowhere ukapige ramli kwenye kurasa ya jamaa tena ukiingizia na habari za A.K.A ambaye hausiani kabisa na hiyo page.
Ahahahaa... Eti ramli lakini hakupaswa kuni block ule ni utoto kwa kweli ambao hata dogo janja hawezi kufanya
 
Back
Top Bottom