Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Mkurugenzi Mkuu wa CBE, Prof. Emmanuel Mjema
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kimepanua wigo wa elimu ya biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kwa kuongeza idadi ya wahitimu 14,000 kila mwaka.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho, Mkurugenzi Mkuu wa CBE, Prof. Emmanuel Mjema, alisema kutakuwa na mafunzo kwa wajasiriamali, mafunzo kwa ajili ya maandalizi ya maisha ya ustaafu, pamoja na harambee.
Aidha, maadhimisho hayo ya miaka 50 yataendana na mafunzo katika mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Mbeya na Zanzibar.
Katika kuadhimisha miaka 50 tutatunisha mfuko na tunatarajia kupata Shilingi bilioni tatu, ambazo zitatumika katika ujenzi wa madarasa, maabara na tutatoa msaada wa mashuka kwa baadhi ya hospitali zilizopo katika mikoa hiyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii, alisema Prof. Mjema.
Alisema awali chuo hicho kilikuwa ni kwa ajili ya mafunzo kwa mameneja kutoka taasisi mbalimbali kwa ngazi ya cheti na hivi sasa kimeweza kuongeza wahitimu wa fani mbalimbali zikiwamo za utawala wa biashara, uhasibu, uzito na vipimo.
Fani ya shahada ya biashara itakayoanza itaweza kutatua changamoto ya uhaba wa walimu wa biashara katika shule na vyuo, alisema Prof. Mjema.
CHANZO:NIPASHE