Makomangilo
Member
- Oct 14, 2011
- 20
- 3
[h=2]KWETU TANZANIA: SABABU ZA UFAULU MCHACHE WA KIDATO CHA NNE 2012.[/h]
- Shule za sekondari kuhamishiwa TAMISEMI. Watendaji wa Tamisemi badala ya kusimamia taaluma mashuleni, wanasumbua na kuharibu taaluma kwa (a) kuingilia utawala wa shule katika kuendesha shule; (b) kusumbua, kuwahamisha na kusambalatisha walimu kila wakati ambapo wanawakatisha tamaa na kuwaondolea utashi 'Morale' wa kufundisha (c) kukata au kuwanyima walimu mafao yao kwa makusudi, sababu inayowaondolea wito wa kufundisha.
- Wanafunzi kutotimiza majukumu yao ya kujifunza. Jamii kwa ujumla na wazazi waelewa kuwaacha tu watoto kuendelea na uzembe.
- Wanafunzi kutokuwa na nidhamu mashuleni na jamii kuwakingia kifua wanapokosa wasipewe adhabu. Kitu hiki huhamisha fikra za mwanafunzi kuwa mtii katika kusoma na kuwa kichaa na mwenye kibuli.
- Watoto kuachiwa kutumia simu mashuleni na maeneo mengine ambapo muda mwingi husikiliza muziki, au huchati na rafiki zao au hupiga simu za kutongozana na wapenzi wao. Muda huu ambao ni wa manufaa kielimu hutumika isivyo. kwa mwanafunzi kuacha kusoma na kufikiria kusoma hawezi kufaulu mtihani. Mwanafunzi ameweza kuandika wimbo wa muziki kwenye mtihani ambayo ni kazi ngumu sana na ya kutumia akiri nyingi; kumbe akiri hiyo hiyo ageihamishia kwenye somo la kiswahili angeweza kufaulu hata kama hakuna mwalimu. wimbo wa muziki ameandika bila kufundishwa, hata kiswahili angeweza kujifunza bila mwalimu kwa kutumia vitabu na muhitasari.
- Walimu kutolipwa mishahara inayoshotosha mahitaji yao kama wafanyakazi wengine wenye elimu sawa na wao, mfano TRA, AFYA N.K. Hii ingewafanya walimu watulie, wafanye kazi ya ualimu vizuri na kuwaza namna ya kuwaelimisha wanafunzi kwa matokeo ya kufaulu.
- Walimu kutotambuliwa na kuheshimiwa na jamii. Jamii inawanyanyasa sana walimu kwa sababu ya masalahi yao duni. Inafikia mahala baadhi ya walimu wakiulizwa na watu ambao hawawafahamu kuwa wanafanya kazi gani, huficha kazi zao na kutaja kazi zingine zenye masilahi makubwa ili kulinda heshima ya utu wao au ili wapatiwe huduma nzuri. Kitendo cha mwalimu kutotambuliwa na jamii naye ameondoa wito wake wa kufundisha wanafunzi. Amebakiza tu kuingia darasani kama muhubiri ambapo wasikizaji wake hana shinda ya kuwapima kama wamemwelewa au yale aliyosema wameyashika au la. Dawa ni kuwalipa walimu malipo yanayowatosha kuishi vizuri. Mtu fukara katika jamii hana thamani kwa watu kiushirika (social life).
- Ukosefu wa walimu wa hisabati, sayansi, maabara na vifaa vya kutosha vya maabara katika shule nyingi za serikali. Watoto wawapo shuleni, wanatakiwa wajifunze mafunzo yaliyopangwa kujifunza wakati ule ule uliopangwa kujifunza. kwa sasa watoto hawajifunzi wakati ule ule ulipangwa na wengi hawajifunzi kabisa. Mwanafunzi anapofanya mtihani wa somo ambalo hakufundishwa ipasavyo au hakufundiwa kabisa, hawezi kufaulu bali hufeli.
- Hakuna mtaala wa elimu wa kudumu unaoeleweka Tanzania (clear and consistent curricurum for all Tanzanian schools). Kwa kuwa mtaala haueleweki, syllabi nazo hazieleweki. kwa kuwa syllabi hazieleweki, vitabu na vitu vingine vya kufundishia masomo navyo havieleweki. Mfano: Kwenye somo la Geography, Mtihani wa mwaka 2012 (CSEE - SCHOOL CANDIDATES); swali la 6 ambalo ni la lazima (09%); Mtunga swali ametumia syllabus ya 1997 hali syllabus iliyotumika kufundishia wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2012 katika shule nyingi za Tanzania ni ya 2010. Swali linahusu LEVELLING IN LAND SURVEY. Topic hii haipo kwenye syllabus ya 2010 bali ipo kwenye syllabus ya 1997. Kwa hali hiyo basi, wanafunzi walioweza kufanya swali hilo, ni wale tu waliofundishwa na mwalimu aliyelitunga na wale tu waliofundishiwa syllabus ya 1997. Wale wa shule za KATA na za kawaida hawakuweza kulifanya, kwa hiyo wakafeli. Yapo mapungufu mengi sana ukiyachimbua. CHA KUANDIKA TU NI KWAMBA, MSIMAMO IMARA ULIOTULIA WA ELIMU TANZANIA HAUPO, NA KWA MAANA HIYO WANAFUNZI WALIOWENGI HAWAWEZI KUFAULU HATA KAMA WAKIWA NA UWEZO MKUBWA KIAKIRI. MPAKA USANII NA UBABAISHAJI UONDOLEWE NDIPO ELIMU TANZANIA ITAKUWA BORA.
- Tatizo lingine ni utofauti wa walimu wanaofundisha masomo. Mwalimu wa somo fulani aliyetoka UDSM ni tofauti na aliyetoka UDOM, ni tofauti na aliyetoka MWENGE, ni tofauti na aliyetoka SEKUCO, ni tofauti na aliyetoka SOKOINE, ni tofauti na aliyetoka RUCO, ni tofauti na aliyetoka ............... Hii ni kwa sababu hakuna usawazishaji wa mitaala, course contents na vitu vingine vyote vinavyotumika kufundishiwa walimu wajifunzao katika vyuo vikuu vya elimu Tanzania. Matokeo yake ni kwamba, watoto wanakuwa wanaeleweshwa tofauti tofauti. Kwa maana hiyo, kwenye mtihani wa Taifa, wanafunzi watakaofaulu vizuri ni wale tu watakaofundishwa na walimu waliotoka katika chuo kikuu alichosomea mwalimu mtunga swali. TANZANIA HAKUNA MTAALA NA UTARATIBU WA ELIMU UNAOELEWEKA. Hii nayo ni mojawapo ya sababu zilizochamgia wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2012 kufeli.
- Kupeleka sekondari wanafunzi mbumbu (waliofeli) kutoka darasa la saba. Mwaka 2012 serikali iliangalia idadi ya wanafunzi waliopelekwa sekondari bila kujua kusoma na kuandika, ikapata namba kubwa tu. Haikuwatoa ili waongeze idadi wanafunzi watakaofeli baadaye. Wanafunzi wengi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012 hawakuchujwa wala kuangaliwa kama wote walikuwa wanajua kusoma na kuandika. Ukweli ni kwamba wengi walikuwa hawajui ndiyo maana wamefeli.