To the best of my knowledge ni kuwa ukipewa Gari mbili zenye cc zinazolingana ie 1980 lakini zinaztofautiana idadi ya cylinder, labda Moja four cylinder nyingine six, uko salama zaidi kama utachukua yenye cylinder Sita! Kuanzia ulaji WA mafuta hadi kudumu kwa engine
Iko hivi!, stress kwenye parts za engine za four ie pistons, rods na bearing ni kubwa kuliko engine za six, means kwa kazi Aina Moja engine ya four ita struggle wakati engine ya six itafanya kwa kurelax
Cha pili ni cooling efficiency engine kubwa huwa (six) Zinachukua eneo kubwa na pia kuingia maji mengi, hii ni advantage Kwan kuchemsha ni ngumu sana
Tatu ni stability ya torque,! Firing order kwenye engine za four ipo mbali mbali, yaan Kuna interval kubwa Kati ya pogo Moja na jingine, hii hupelekea vibration flani katika engine inapo run, katika engine za six interval ni karibu karibu, na ndo sababu engine za six huweza ku idle katika Rev mdogo Sana na isitetemeke au kuzima
Stable torque ni Moja ya sababu ya engine zenye cylinder nyingi kudumu muda mrefu.
Ulaji wa mafuta naamini kwa engine zinazolingana cc, engine ya six itakula vizuri kushinda ya four, kama utafata kanuni za kuendesha engine kubwa.
Sent using
Jamii Forums mobile app