Cc ya CCM naomba ufafanuzi juu ya msimamo wenu

MAKUNDA

Senior Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
115
Reaction score
39
Kwanza nawapongeza kwa uchambuzi wenu wa kina mlioufanya kwenye rasmu ya Katiba mpya. Mambo mengi mmeyaeleza na kuweka msimamo. Pamoja na msimamo wenu nashukuru kwa kumalizia kila hoja kuwa wanachama wajadili na kutoa maoni yao.

Suala ambalo limenileta kwanza ni juu ya Serikali mbili kwa mujibu wa msimamo wenu. Katika maelezo mliyotoa mmesema kuwa mnataka serikali mbili ya Zanzibar na ya Muungano na kuwa Serikali ya Zanzibar itashughulikia masula ya Zanzibar yasiyo ya Muungano na Masuala ya Tanzania bara yasiyo ya Muungano yatashughulikiwa na Seikali ya Muungano. Hii inamaana kwamba Rais wa Zanzibar ndiye msemaji mkuu wa mambo ya Zanzibar, na rais wa Serikali ya Muungano ndiye msemaji mkuu wa mambo ya Tanzania bara yasiyokuwa ya Muungano.Sasa maswali langu ni haya:-

Je itakuwaje pale rais wa Muungano atakuwa ametokea Zanzibar?
Je itakuwa ni halali mtu wa zanzibar kusimamia mambo ambayo hayahusiani na kwao anakotokea?

Kama msimamo ni huo maoni yangu ni haya

KATIBA ITAMKE WAZI KUWA RAIS WA SERIKALI YA MUUNGANO WAKATI WOTE ATAKUWA ANATOKEA TANZANIA BARA.

Kama hili haliwezekana basi nitakuwa na msimamo tofauti na Chama Changu sitaunga mkono Serikali mbili badala yake nitaunga mkono serikali tatu au Moja.

Nimetanguliza hili lakini viko vipengere kadhaa ambavyo vinaukakasi katika msimamo mliotuletea na kutushawishi tuumeze alafu tuutetee.


MPINZANI WA LEO NI MTAWALA WA KESHO NA MTAWALA WA LEO NI MPINZANI WA KESHO, HEBU TUWEKE MIZANI YETU SAWA TUSIJE TUKAJUTA HAPO BAADAYE. KISU ULICHOKINOA KINAWEZA KUKUUMIZA WEWE MWENYEWE. NANI AJUAYE YA KESHO AU BASI KESHO KUTWA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…