CCJ waibukia kwa Nyerere

Sijui kuna nini kati ya CCJ na Mwanakijiji. Maana debe analokipigia si la kawaida.

Hoja ya kwamba CCJ chama cha maana (serious) kwa sababu kimejulikana kwa muda mfupi ina utata. Kwani zilianza rumours kwamba baadhi ya vigogo wa CCM ndio waanzilishi wa CCJ. Ni hilo ndilo lililoipandisha "chati feki" CCJ. Zaidi ya huu udaku, hamna la maana. Hata wanapoulizwa viongozi wengine wa siasa juu ya nguvu ya CCJ, msingi wake ni hizo tetesi za vigogo hewa wa CCM.

Bado nasimama pale pale: ni waganga njaa. It is hoax.
 

Kwa kweli hata mimi namshangaa Mwanakijiji.Huenda na yeye akawa ni one of the founders...Hutuwezi kujua lets wait and see.
 

Mmh kwa kweli umejitetea sana lakini halijaniingia hata moja......CCJ inaogopwa kwa kuwa imekuja wakati mbaya kwa vyama vingine na imetumia njia nzuri ya kujipatia umaarufu na kwa kuwa wapiga kura wengi hatuna misimamo ndio maana tunaogopa....by the way nadhani hakitashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu..Nitafurahii ile mbaya.....Kuliko maelezo....
 

Katiba ni maandishi tu Mkuu,ngoma ipo kwenye utekelezaji..Usidanaganyike na Maandishi siku zote huwa yanavutia sana..
 

Mkuu, nina imani kwamba MMM anajua anachokipigania ingawa pamoja na chokochoko zangu nimeshindwa kukipata... personally najua kuna mchango fulani umeenda CCJ kama chachu ya mabadiliko Tz. Vilevile nafahamu what is wee is not the whole deal, lakini sasa na mimi ntaendelea kuchokonoa mpaka tupate ukweli na undani... la sivyo CCJ inaweza kuwa kama vyama vingine ya ruzuku tu.. so far tanzania tuna upinzani serious kutoka CHADEMA na CUF, nachelea kuwaingiza CCJ huko
 

jamani.. kama ni hoax inapuuziwa! jiungeni na muunge mkono vyama ambavyo mnaviamini kuwa siyo hoax... CCM, CUF, CHADEMA, NA TLP. Vyama hivi si ndiyo "zimwi likujualo"?

Bado sielewi kwanini SisiJuu kinawaumiza kichwa wakati hakina majina makubwa, hakina historia ndefu ya upinzani, kimechelewa kuja, viongozi wake wanalialia (sijawahi kumuona kiongozi wa chama kingine chochote akilia hadharani kuhusu Tanzania au hata kujililia nafsi yake!)... mimi naomba mkipuuze tu! for your own destruction..
 
Kwa kweli hata mimi namshangaa Mwanakijiji.Huenda na yeye akawa ni one of the founders...Hutuwezi kujua lets wait and see.


napenda watu walio bold, people who do things against the conventional wisdom! siyo watu wanaofanya watu wanachotarajia... hadi hivi sasa SisiJuu imepindua kabisa script ya uanzishaji wa vyama vya siasa nchini, imetumia mbinu mbalimbali za kimauzo n.k kama jeshi zuri lakini dogo linalojiandaa kupambana jeshi kubwa (a combined force of all other political parties)..

Labda msome "The Art of War".. mtaelewa kuwa wakati mwingine siyo wingi, na silaha kali kunakoleta ushindi.. its all about mbinu.. na mikakati. Hadi hivi sasa SisiJuu imewazidi mikakati vyama vingine vyote..!!
 
Katiba ni maandishi tu Mkuu,ngoma ipo kwenye utekelezaji..Usidanaganyike na Maandishi siku zote huwa yanavutia sana..

Sawa.. vyama vingine navyo si vina Katiba na maanndishi yao; vimetekeleza vipi? Sasa hawa mmeshawahukumu kuwa ni "hoax" wakati hata kiti kimoja cha serikali ya mtaa hawana, hawajapata hata usajili wa kudumu! Sasa ngojeni wapate usajili wa kudumu, subirini muone watakaposimamisha wagombea wake kila jimbo nchini mtashangaa! halafu waje waibuke na kuviume vyama vikonge kama kwa kushitukizwa...
 
CCJ inaweza kuwa kama vyama vingine ya ruzuku tu.. so far tanzania tuna upinzani serious kutoka CHADEMA na CUF, nachelea kuwaingiza CCJ huko

just count them out.. na endeleeni na vyama vingine "serious" vya upinzani.. CCJ siyo chama cha upinzani ni chama kinachotaka kuongoza mabadiliko ya kweli! Hivi vyama vingine viendelee tu kuwa wapinzani.
 
Mambo yote makubwa yanataka umakini na subira ili kuweza kupata manufaa yake. Hili ambalo CCJ inalipangilia kufanya ni jambo kubwa maana linaweza kuubadili mustakabali wa Taifa.
Mimi nawapa muda ili nione kama wanamaanisha wanayoyasema. Ntafanya kosa kubwa kama fatwa yangu ntaitoa mapema kiasi hiki.
It is for them to prove beyond no doubt that they mean what they say
 
na huu ndo mwendo wa ccj
mtafika
ongeza mwendo
msiangalie nyuma
hawa mbele yenu wanamatumaini nanyi
 

Ndahani.. hicho unachosema ni hekima; binafsi sijui watakuwaje huko mbeleni. Lakini niko impressed na jinsi walivyoingia.. na nina uhakika kama ni watu wanaosikiliza ushauri (yaani siyo kichwa ngumu) watasikiliza matamanio ya Watanzania na kuyafanyia kazi.

Hadi hivi sasa wamejaribu kujibu maswali kadhaa ambayo Watu wamekuwa wakiyatamani yajibiwe. Binafsi nitakuwa tayari hata kuwasaidia kuandika Katiba yao mpya ikiakisi fikra za kizazi kipya kuhusu uongozi na sitosita kuwasaidia kuchangia kuandika ilani yao ya uchaguzi, kwani ni chama pekee ambacho wamekuwa waunganwa kuomba ushauri wafanye nini...
 
just count them out.. na endeleeni na vyama vingine "serious" vya upinzani.. CCJ siyo chama cha upinzani ni chama kinachotaka kuongoza mabadiliko ya kweli! Hivi vyama vingine viendelee tu kuwa wapinzani.
mkuu, nina ugonjwa mmoja naupenda sana, kuona vitendo rather than kusikia mlio!!! i am for Tz na kama umesoma humu, i have never supported a party, i support maisha mazuri kwetu

nasubiri mambo ya CCJ yaje, but they have had a fault start, badala ya kuingia kwenye media kivile, basi wangekuja na namna nyingine
 
just count them out.. na endeleeni na vyama vingine "serious" vya upinzani.. CCJ siyo chama cha upinzani ni chama kinachotaka kuongoza mabadiliko ya kweli! Hivi vyama vingine viendelee tu kuwa wapinzani.

Mwanakijiji, unaweza kumpeleka ng'ombe mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji. Tatizo kubwa la Watanzania ni Utomasi - heri zimwi likujualo hata kama linakutafuna na kukumaliza. Ndio maana CCM pamoja na kututafuna usiku na mchana bado tunawakaribisha hadi majumbani kwetu watufaidi zaidi. Hawa waanzilishi wa CCJ ni Watanzania wenzetu, let's give them a chance - kama ni malimbukeni, time will tell. Lakini walichoweza kufanikisha kwa huu muda mfupi ni ishara nzuri tu ya penye nia pana njia - kweli akili mali.

Ndio ni sungura lakini kwa akili kidogo tu anaweza kukwepa kuwa kitoweo na badala yake akapata mlo mzuri tu !
 
nasubiri mambo ya CCJ yaje, but they have had a fault start, badala ya kuingia kwenye media kivile, basi wangekuja na namna nyingine

kauli yangu moja huko nyuma ni kuwa mabadiliko siyo yale tunayoyatamania au kuyangojea; ni yale tunayojiletea. Sasa endelea kusubiri mkuu.. subiri wengine walete na yakija we dandia
 
Kadiri ya magazeti ya leo, Mwananchi, Tanzania Daima, ni kwamba CCJ watafanya mkutano wa hadhara leo. Na inawezekana vigogo kadhaa kutoka CCM wakatambulishwa kama supporters/members wake.

Hivi hakuna mwanahabari (JF member) yeyote aliyeko huko kwenye mkutano atupe yaliyojiri?
 
Leo nilikuwapo pale mwananyamala kuangalia how serious are they. Nia yangu ilikuwa kuwaona vigogo wa CCM wanaoingia. wakabadili kibao kwamba vigogo ni wananchi mamilioni ya watanzania wanaoweza kufanya mabadiliko, well well well they are damn right! kisha wakasema ninachochukia kila siku ahadi zisizotekelezeka eti watanzania watapoatiwa kilo moja ya nyama kila siku wakiingia madarakani ahh labda falsafa ya kuonyesha kwamba watasaidia kuondoa umaskini si unajua tena kwamba nyama kwetu ni utajiri mhhh! kisha wakafanya upuuzi mwingine wakagawa kadi bila kusajili hii taratibu gani hii?, lakini lazima niwape hongera watu walifikia mia mna kitu hivi kinyume na mbatia ambaye ukihesabu watu pale Kawe jana utalia, haya na anasema atagombea kawe. Mhh wrong calculation labda si kweli.
 
kauli yangu moja huko nyuma ni kuwa mabadiliko siyo yale tunayoyatamania au kuyangojea; ni yale tunayojiletea. Sasa endelea kusubiri mkuu.. subiri wengine walete na yakija we dandia
Thanks Mkuu.... i can confirm that for the past three years i have made alot of changes around me, hiyo ni kwa level yangu

Ila ya CCJ ntadandia mikakati na sera kiutekelezaji na si propaganda wala "kulialia"
 
Huo wote ni USANII na unafiki matupu. Hawana lolote hawa, nimewasoma nimeona hawana dira. Kulia kaburini maana yake nini, wao wana uchungu zaidi ya Wana ukoo wa hayati Mwalimu au Wazanaki ?? Waende zao kule !!!!
 
Kuna mkuu anatuambia VILAZA ndio watamchagua Kikwete......................... aah!!! hapana bana, usituchagulie mtu wa kumpigia kura. Kama kilaza, wewe mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…