CCJ waibukia kwa Nyerere

Kulialia mbele ya kaburi la Nyerere may seem like a cheap publicity stunt to some. Lakini it could be taken as a serious gesture of empathy by others.

No doubt to CCJ this is a calculated move to gain political mileage and ultimately votes. These people know their customers. All political parties do what they have to do to beat the competition.

Miaka nenda rudi kila nikiona kwenye kampeni za uchaguzi CCM wakigawa khanga, kapelo, t-shirts, maonyesho ya ndondi, kwaya, taarabu, nk nilikua nadhani hawako makini. Kumbe wao wanajua kile wapigakura wakitanzania wanachotaka.

Asilimia ya wapigakura wa kitanzania wanaotaka kusikia manifesto, sera, mikakati na kuichambua ni ndogo mno. Nadhani hata negligible. Idadi ya wale wanaotaka burudani, mandazi na vitumbua ni kubwa sana.

Hawa jamaa wa CCJ are definitely on to something.
 

Mzee wa kijijini unataka kutuaminisha hawa jamaa wana kitu? Mbona watu wanakituhumu kwa mengi, cha vigogo, cha Lowassa nk....kama mtu anajua ukweli halisi wa CCJ, tafadhali tujuze. Hata mimi haya majina ya viongozi wao yananingónyesha, hawana profile yeyote. Siamini mtu unaibuka leo, ukafanikiwa kisiasa leo leo.
 
Hawa jamaa wasilete ya Kambona kwamba ana siri za Mwalimu Nyerere kumbe alikuwa hana kitu. Wanatangaza kuna vigogo wa CCM kumbe ni uongo mtupu.

 
Nawapenda CCJ, nalipenda tamko lao kuhusu vigogo! Ni ukweli usiopingika vigogo wa nchi hii ni wananchi wanaowapa uongozi wale tunaowaita na kuwatambua kwamba ndio vigogo. Kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba CCJ wamefika mahali wameona kwamba hao vigogo ndio walioifikisha nchi hapa ilipo - pabaya. Sasa iko haja ya kufanya mageuzi ili vigogo halisi wa nchi hii wajulikane na watambulike vilivyo kwamba ndio vigogo haswa. Ni darasa la aina yake toka CCJ, ni wenye akili nzuri peke yao ndio watakaoweza kuelewa fundisho hilo toka CCJ.
 
Ndiyo wameibukia Butiama. Nasikitika kuhusu yule mtu aliyepiga busu kaburi la Mwalimu Nyerere. Watu kule wanapaswa kutoa heshima zao bila kubusu kaburi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…