Uchaguzi 2020 CCM anzisheni "Kipima joto" kwa Madiwani na Wabunge wenu

Uchaguzi 2020 CCM anzisheni "Kipima joto" kwa Madiwani na Wabunge wenu

nyumbamungu

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2017
Posts
1,033
Reaction score
895
Haya ni maoni yangu kwenda kwa watunga sera wa Chama Cha Mapinduzi, ikumbukwe mwezi Julai 2020 kulikuwa na kura za maoni kwa waliokuwa wanadhamiria kugombea nafasi ya Udiwani na Ubunge katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwezi wa Kumi mwaka huu. (20201028, Jumatano)

( i ) Wafanye utafiti kujuwa kero ( siku hizi ni changamoto ) zinazowakabili wananchi wa kila Jimbo la uchaguzi katika Majimbo yote 264 Tanzania nzima.

( ii ) Mathalani kero zinazojirudia , zichukuliwe kero Tatu zinazofana kwa kila Jimbo zitungiwe Sheria, kuwa kila mgombea anayetoa ahadi kuwa endapo akichaguliwa ataiondoa kero husika ahakikishe anatimiza ahadi hiyo kabla ya Uchaguzi mwingine.

Kwa mfano: Maji safi na salama, Huduma ya Mama na Mtoto, Kuhakikisha watoto waliotimiza umri wa kwenda shule wanakwenda shule. Upatikanaji wa Dawa kwenye Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali nk

( iii ) Kwasababu kipindi cha kuhudumu kwa Wabunge ni Miezi 60, ( miaka mitano )hivyo kila inapokamilika miezi 30 ( sawa na miaka miwili na nusu ) ifanyike mikutano ya jimbo kama "Kipima joto" kufanya tathmini ahadi walizoahidi Madiwani na Wabunge zimetekelezwa kwa asilimia ngapi?

Kwa mawazo yangu itakuwa ndio njia rahisi na nyepesi kufanya mchujo kwa watakaotaka kurejea kujitathmini kama wanatosha.
 
Back
Top Bottom