Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 308
Mimi nimeupata kutoka namba 2557071788. Kama kweli TCRA hawawezi kumbaini anayetuma ujumbe huu basi usalama wa nchi hii uko hatarini sana. Kama watu wa namna hii hawatakamatwa wanaweza kuliingiza taifa hili katika mgogoro kwani hatujui kesho na kesho kutwa watatuma ujumbe wa namna gani.
we kalumekenge angalia mwanajf mwingine ameshaupata ujumbe naye. na namba zimetofautiana. kuna kitu hapo. ila always utagundua tarakimu moja inamiss. linganisha na namba nilizotoa.
Acha upuuzi wa kizamani. shiriki kusimamisha hizi spinning dogo
MaFISADI WAMEKAMATA NCHI HIIII!TCRA? Yule ceo wa pale ni msn** sana! ni vibaraka, naomba uisome post hii, nyie ni vibaraka, tena nina hasira balaa :frusty:
kuna ujumbe umenifikia sasa hivi kutoka namba 078049550 kupitia mtandao wa zain usemao...
Kwenye bold hapo ni kwamba shibuda ndiye anayeshikiliwa isivyo halali mpaka sasa, hivyo wanavyosema kuwa mjumbe wa kampeni wa slaa amekamatwa huo ni uwongo na kuchafuana kama walivyo wachafu.
Wakuu nimeweka hii namba hapo kwani utata wake ni kwamba ina tarakimu tano badala ya sita hivyo naamini kuna niambaya makusudi imefanywa na hata hao wenye mtandao (zain) kupitisha huu ujumbe.
Pili ni kwamba mimi ninaomba msaada wa kisheria niweze kushtaki maana ujumbe huu maana sijui mtumaji ana lengo gani na mimi.
Nimejaribu kumpigia mwenye namba simpati. Kama kuna mtaalam anaweza kuipata chanzo ya hii namba tumwanike hapa jukwaani
Sasa mnalalamika nini? Hiyo SMS mi naona ina ukweli mtupu. Chadema wamemuua dereva wa CCM na Shibuda kawekwa ndani? Na ni ukweli kwamba watu wa Chadema walisema mwaka huu lazima kieleweke hata kama damu itamwagika.
People, this is politics. You can't do/say crazy things without suffering the consequences. Own it up, apologize or something then move on. Sasa nyie mnaanza kuplay victim kama kawaida yenu. The other day Slaa kasema kwamba karatasi za kura ziko tunduma. It turns out alikuwa anaropoka kama kawaida yake. Wabongo sio wajinga kiiivyo jamani.
na wewe acha uongo wako shibuda wala hashikiliwi, inaonekana wewe ndiyo umetunga hizo message na unasambaza.
Kuna mtu kaupata hapa kanionyesha!wakuu jana tarehe 24 oktoba, 2010, mnamo saa 1:09 jioni nilipata ujumbe wa maandishi (text message) kwenye kikasha cha kupokelea cha simu yangu; uliosema:
chadema wametekeleza ahadi ya kumwaga damu. juzi wamemuua ndugu wa mgombea wa ccm maswa. mjumbe wa kampeni ya slaa amekamatwa. tuwakatae chadema wamwagaji damu.
my take;
- je, ni kweli chadema walitoa ahadi ya mauaji kwenye ilani yao ya uchaguzi.
- ni nani hao waliotuma ujumbe huo na kwa nini hawajitambulishi?
- je, kuna mkuu yeyote aliyetumiwa ujumbe huu au kusikia popote au ndio mimi tu peke yangu ndiye niliyetumiwa?
Kuna mtu kaupata hapa kanionyesha!
Ni mipango-mikakati ya akina MAKAMBA hii, lakini haisaidii kitu!
Ingekuwa ni ishu hata waandishi wa habari wangemuuliza SLAA juzi kwenye mdahalo!
Wachana na hii upuuzi, tunza shahada yako ready for 31st October