Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Lilian Lugakingira, Bukoba
HALMASHAURI ya CCM, Wilaya ya Bukoba mjini, imewasimamisha kushiriki katika kampeni za chama hicho, viongozi watano, akiwemo mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) wa wilaya hiyo mjini, Murungi Kichwabuta.
Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Robert Bahati alitaja viongozi wengine wa chama hicho waliosimamishwa wasishiriki katika kampeni za chama hicho kwa madai ya kukihujumu chama kuwa ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa, Abdalah Kichwabuta na Pius Kaijage ambaye ni katibu wa CCM , Kata Kahororo.
Bahati aliwataja wengine waliosimamishwa kuwa ni Sylivanus Muhyoza aliyekuwa diwani wa Kata Kahororo kipindi kilichopita na Udi Miruko katibu mwenezi CCM Kata Bilele.
Alisema wanachama hao wamezuiliwa kujihushisha na kampeni za chama hicho juzi na halmashauri ya CCM wilaya ya Bukoba mjini baada ya kubainika kukihujumu chama katika kampeni zinazoendelea kwa kupinga wagombea wa CCM.
Mwenyekiti huyo wa CCM Bukoba mjini alisema kuwa pamoja na kusimamishwa wasihusike katika kampeni, wanachama hao wataendelea kuwa chini ya uangalizi wa chama hicho.
Alisema pia baadhi ya wanachama hao wamejihusisha na vitendo vya kufanya kampeni ya umeya wa Manispaa ya Bukoba kabla hata ya uchaguzi wakati meya huchaguliwa na madiwani.
Imedaiwa kuwa wanachama hao wanapita kwa wagombea udiwani ambao wanaonyesha uelekeo wa kushinda na kuwaomba wakichaguliwa wamchague tena Samwel Ruangisa ambaye alikuwa meya katika kipindi ilichopita, ili aendelee na wadhifa huo.
Hivi karibuni uongozi wa CCM Bukoba mjini, mbele ya mke wa mgombea urais wa CCM mama Salma Kikwete, uliwatuhumu Samwel Ruangisa ambaye pia anagombea udiwani katika kata Kitendaguro na Murungi Kichwabuta mwenyekiti wa UWT Bukoba mjini kuwa wanakihujumu chama na watakikosesha kura.
Chanzo: Mwananchi