CCM chama kikongwe lakini kinaogopa uchaguzi huru na Katiba Mpya

CCM chama kikongwe lakini kinaogopa uchaguzi huru na Katiba Mpya

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Pamoja na CCM kuwa Madarakani zaidi ya Miaka 60 bado Chama hicho hakijiamini kwenye Suala la UCHAGUZI HURU na HAKI.CCM imekuwa inatumia Vyombo vya DOLA Kushinda UCHAGUZI kama tulivyojionea UCHAGUZI wa KIHUNI wa Mwaka 2020.

Pia ni jambo la AJABU kwa CHAMA kikongwe kama CCM kuogopa Suala la KATIBA MPYA licha ya Wananchi kutaka KATIBA MPYA.Niliamini CCM kwa UKONGWE wake Ingejiamini katika UCHAGUZI na Pia KATIBA MPYA.

Bado Mwaka Jana tumeshuhudia VIONGOZI wanajiwekea KINGA najiuliza Wanaogopa nini? Kwani Wanataka kufanya nini kibaya kwa Wananchi ili WASISHTAKIWE? Mbona Marais Waliotanguliwa Hawakujiwekea Kinga?

Ni Dhahiri UKIUKWAJI wa KATIBA unaofanywa na hao VIONGOZI ndio Sababu ya Kujiwekea KINGA kwa mfano Suala la Wabunge 19 Waliofukuzwa na Chama chao lakini Bado Wapo Bungeni Wanalipwa na Mishahara wakati kwa Mujibu wa Katiba Walipaswa Wawe WAMEFUKUZWA BUNGENI.
 
Kwani ccm wenyewe wanaaemaje mfano wakitaka kuchagua mwenyekiti wa chama anagombea na nani ?
 
Bado Mwaka Jana tumeshuhudia VIONGOZI wanajiwekea KINGA najiuliza Wanaogopa nini? Kwani Wanataka kufanya nini kibaya kwa Wananchi ili WASISHTAKIWE? Mbona Marais Waliotanguliwa Hawakujiwekea Kinga?
Rais wa wanyonge alikuwa
-na ulinzi mkubwa kuliko RAIS yeyote Africa,
-anaogopa kabisa kusafiri kwenda kwa wenzake nje ya Tanzania,
-hataki kukosolewa na mtu yeyote kwa jambo lolote
-hataki kupewa ushauri na mwananchi yeyote
-na kinga ya kutoshitakiwa kwa lolote lile atakalotenda kwa yeyote.
 
Waambie wenzako wa chama dola wa level playing field tu,then itisha uchaguzi mkuu even within 3mths tuone Matokeo yake
 
Mbona uchaguzi ulipita hamkwenda kutoa nyongo kwenye box la kura
Nyie Ni magwiji wa kujimwambafai humu na Twitter
Kuna uchaguzi gani ulifanyika? Au unazungumzia ule ujambazi ulofanywa na nyie October last year ukiratibiwa na Mahela aliepokea maelekezo kutoka kwa Hayati?

Hakukua na uchaguzi pale bali ulawiti wa demokrasia..
 
Shida ya chadema ndio hiyo kwenye kampeni nyie mnajaza bando na kejeli mitandaoni
Vijana siwaoni mkipiga kura hata mara moja
 
Pamoja na CCM kuwa Madarakani zaidi ya Miaka 60 bado Chama hicho hakijiamini kwenye Suala la UCHAGUZI HURU na HAKI.CCM imekuwa inatumia Vyombo vya DOLA Kushinda UCHAGUZI kama tulivyojionea UCHAGUZI wa KIHUNI wa Mwaka 2020...
Jengeni kwanza chama acheni porojo!

Mmekula ruzuku billions of money lakini mmeng'ang'ania pale ufipa.

Uchaguzi 2020 ulikuwa huru na haki.

Wananchi hawajalilia katiba mpya,ila nyinyi wanasiasa wasakatonge ndio mnaoitaka hiyo katiba mkitarajia itawawekea mazingira rahisi kuingia IKULU.
Kenya walilia katiba mpya wakapata ya BOMAS!

Lakini leo wanataka BBI, wanasiasa wa kiafrika hamuaminiki kamwe! ni watu wa kusaka fursa tu.
FB_IMG_1619410849412.jpg
FB_IMG_1616409856423.jpg
FB_IMG_1616524447432.jpg
 
Pamoja na CCM kuwa Madarakani zaidi ya Miaka 60 bado Chama hicho hakijiamini kwenye Suala la UCHAGUZI HURU na HAKI.CCM imekuwa inatumia Vyombo vya DOLA Kushinda UCHAGUZI kama tulivyojionea UCHAGUZI wa KIHUNI wa Mwaka 2020...
Kabla ya mama samia kilikuwa kimopoteza mvuto kabisa.Shujaa alififisha kabisa umaarufu wa CCM
 
Bado Mwaka Jana tumeshuhudia VIONGOZI wanajiwekea KINGA najiuliza Wanaogopa nini? Kwani Wanataka kufanya nini kibaya kwa Wananchi ili WASISHTAKIWE? Mbona Marais Waliotanguliwa Hawakujiwekea Kinga?
Rais wa wanyonge aliekuwa
-na ulinzi mkubwa kuliko RAIS yeyote Africa,
-anaogopa kabisa kusafiri kwenda kwa wenzake nje ya Tanzania,
-hataki kukosolewa na mtu yeyote kwa jambo lolote
-hataki kupewa ushauri na mwananchi yeyote
-na kinga ya kutoshitakiwa kwa lolote lile atakalotenda kwa yeyote.

Mungu akamwona kuwa hafai kuendelea kuwa nasi huku
 
Back
Top Bottom