Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Awali napenda kumpongeza Ndg. Kinana kwa kazi nzuri anayoifanya ya kukiimarisha chama, ni kazi anayoimudu tangu akiwa katibu mkuu wa CCM. Na zaidi ya yote nampongeza kwa juhudi zake za kusimia HAKI na USAWA wa wanaCCM kuchagua na kuchaguliwa ambao ni msingi imara wa demokrasia makini ndani ya CCM.
Zaidi ya yote sio jambo rahisi kusimamia HAKI na USAWA huo kwa asilimia 100 kwa sababu kuna wengine wanaona fursa katika kuvunja HAKI huko. Tumesikia malalamiko mengi juu ya Chaguzi zinazoendelea ambayo kimsingizi yananyima HAKI inayohubiriwa.
Kufanya chaguzi za marudio za kidemokrasia kama za CCM ni aibu na pia ni gharama. Je aibu hii nani ataificha na gharama hizi nani atafidia? Ni jambo linalohitaji mjadala mpana na uongozi wa CCM kuja na suluhisho la kudumu ili hofu ya kunyimwa HAKI itoweke.
Kabla ya viongozi wakuu na vikao vya chama kuja na suluhisho naamini tunaweza kutoa mapendekezo ya nini kifanyike?
Leo nina machache kwa CCM kuelekea kujenga mfumo imara ya kusimamia HAKI na USAWA wa kuchagua na kuchaguliwa.
i) Kwanza, CCM itambue haki ya MTU inapominywa kuna upande unafaidika kutokana na uminyaji huo. Mkianza na upamde unaofaidika kwa kunyima haki kwa kuangalia maslahi yatokanayo na jambo hilo kwa hakika mtakuwa mmetatua tatizo hilo.
ii) Msiishie kukemea na kuagiza kurudiwa chaguzi bali muende mbali kwa kutoa adhabu Kali kwa sababu mengine yanarekebishika kwa adhabu kali sana.
iii) Imarisheni kitengo cha utafiti kama kipo na kama hakipo kianzisheni, kitengo hiki kitawasaidia kufanya tafiti za kisayansi na majibu juu ya matatizo hayo.
iv) Msioneane haya wala aibu kukemeana kama afanyavyo ndg.Kinana hili itasaidia kila MTU kujua mipaka Yake. Kukaa kimya kunazalisha tatizo zaidi.
Naomba kuwasilisha hayo machache kwenu Ndg.Samia, Ndg.Kinana na Ndg.Shein na uongozi wa CCM kwa ujumla kwa mapitio