Ccm: Dar-es-salaam, dodoma na zanzibar ndiyo tanzania!!!!!!!!!! Muswada batiliii

Ccm: Dar-es-salaam, dodoma na zanzibar ndiyo tanzania!!!!!!!!!! Muswada batiliii

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
25,556
Reaction score
25,342
Ndugu watanzania, mjadala unaoendelea bungeni "muswada wa katiba" nawaambia ya kuwa wabunge wa ccm kupitia bunge wanatuambia kuwa dar-es-salaam, dodoma na zanzibar ndiyo tanzania!!!!!! Maajabu na ukiukwaji huu mkubwa wa katiba unatokana na kauli zao kuwa muswada umewafikia watanzania, wameusoma na kutoa mapendekezo yao kwa tume, tume ya bunge iliandaa public hearing dar, dom na zenj, tume imehiari kuchukua maoni ya watanzania wasiozidi 100000, ambao kati ya hao waliotoa maoni ya kulalamikia madaraka ya rais ni wengi hata kwa ushahidi wa ukumbi wa karimjee, tume iliyatupilia mbali maoni hayo kwa vigezo gani hatujui!!!! siielewi thamani ya mtanzania tanzania kwani naona rais ana mamlaka mpaka ya kuiuza nchi, na wananchi hakuna mahali tunaweza kama wananchi kumzuia. huku ccm ikitaka tumuongezee madaraka!!!
kwa kuwa tume haikuwafikia wananchi wa arusha, shinyanga, lindi, morogoro, mwanza, bukoba, singida, tabora, mbeya, iringa, rukwa, ntwara, tanga ............ tume imekiuka majukumu yake, na mchakato wa kuandika katiba ni batili kwani katiba itakayoandikwa tayari ina mwelekeo,
bado kuna element za wananchi kuwakilishwa sawa na katiba ya sasa. hiyo itakuwa ni katiba ya ccm na wala si ya watanzania.

NAOMBA KUTOA HOJA.
 
Nami nimesikitika niliposikiliza katika mahojiano ya BBC, eti wamekusanya maoni ya wananchi kutoka mikoa mitatu: Dar, Dodoma na Zanzibar.
Kwanza ni haki kwa Nchi yenye mikoa zaidi ya 30 kuwakilishwa na mikoa mitatu tu katika jambo nyeti kama hilo la kupata maoni ya wananchi? Walau wangewakilisha kanda mbalimbali kama alivyosema Tundu Lisu kuwa ratiba ilipangwa kabisa, ila tu bi kiroboto akakwamisha eti alikuwa India sijui alikuwa akitanua tu au alikuwa kikazi.
Jambo la pili hata kama alikuwa India kikazi hawezi kuwakilishwa na naibu wake? maana tumesikia eti alisema shughuli ya kukusanya maoni haifanyiki kwa sababu eti yeye (bi kiroboto) hakwepo.
La tatu, huo mkoa wa Zanzibar ndo upi? Nifahamuvyo hakuna mkoa wala kituo kinachoitwa Zanzibar. Bali kuna Unguja, Pemba, au mkoa wa kusini unguja, nk.
 
Back
Top Bottom