CCM dhidi ya serikali 3

CCM dhidi ya serikali 3

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Chama tawala nchini Tanzania, CCM bado kinaonekana kuendeleleza sera yake ya kupinga muundo wa serikali tatu ambao hivi sasa unapendekezwa pia katika rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa mwanzoni mwa wiki iliyopita. Itakumbukwa kwamba hapo kabla tume mbili zilizoundwa zilipendekeza mfumo wa serikali tatu katika muungano kati ya iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar lakini mapendekezo yao hayakutekelezwa .

Rasimu ya Katiba Mpya imezingatia maoni yaliyotolewa na wananchi wa Tanzania ambao ndio wenye maamuzi juu ya hatima ya nchi yao. Tume ya Nyalali na Jaji Kisanga zilipata maoni kutoka kwa wananchi, ambao ndio waliotaka uwepo wa serikali tatu. Inasikitisha kwamba CCM wanataka kuwaamulia wananchi aina ya serikali wanayaoitaka wao. Huku ni kusigina demokrasia na ni dharau kubwa kwa wananchi. Siku zote CCM inadhani kwamba wananchi ni mazezeta na kwamba hawawezi kujiamulia mambo yao wenyewe. Sasa ikiwa wananchi ndio wanaotaka serikali tatu, iweje kikundi kidogo cha wanachama wa CCM wajifungie chumbani huko Dodoma na kuazimia kuchakachua maoni ya wananchi?

Nchi hii ina jumla ya watanzania million 45. Wanachama wote wa CCM hawazidi million 5! Iweje kikundi cha watu million 5 watake kuchakachua maoni ya watanzania million 45? Hii ndiyo demokrasia kweli? CCM wanataka kubaka maoni ya wananchi kwa manufaa ya mafisadi wachache kama walivyozoea kuwatumikia mafisadi huku wakiwaacha solemba wananchi. Hii haikubaliki hata kidogo. Ifike wakati wananchi waone kwamba CCM haiweki maslahi ya wananchi mbele isipokuwa wanalinda maslahi ya wachumia tumbo wachache ndani ya chama na serikali. Hii maana yake ni kwamba serikali haina nia njema na ustawi na mustakabali wa wananchi bali inawatumia kama ngazi ya kutimizia haja zao za kiutawala na kinyonyaji!

Maoni yaliyozaa rasimu ya katiba hii yalitolewa na wananchi wote bila kujali dini, kabila, kanda, vyama, jinsia au hali zao. Kwa hivyo, sio busara hata kidogo kwa CCM kuwaelekeza wanachama wake wakatae muundo wa serikali 3 wakati ni wanachama hao hao ndio waliohojiwa na kukubali kuwa na muundo wa serikali 3! Kufanya hivyo ni sawa na kuwashikia akili watanzania na kuwaona kama hawakuwa na akili nzuri wakati wanatoa maoni ya kuwa na serikali 3. Na nitawashangaa sana wananchi na wanachama wa CCM watakaokubali kushikiwa akili na kubatilisha maoni yao ya awali ya kuwa na serikali 3.

Tujiulize ni kwa nini tume zote tatu (Tume ya Warioba, Jaji Kisanga na Nyalali) waliamua kukusanya maoni ya wananchi badala ya kuwaachia CCM wawaamulie wananchi kama wanavyotaka. Kama hali ni hiyo basi ni bora tume hizi zisingeundwa na kutumia mamilioni ya walipakodi katika kusaka maoni ya wananchi. Basi tungewaachia CCM (wajuzi wa kila jambo) wajifungie ukumbi wa Chamwino huko Dodoma watuamulie watanzania aina ya katiba tunayopaswa kuwa nayo—jambo ambalo ni kubaka demokrasia waziwazi.

Enyi wanaCCM/wananchi, akili za kuambiwa changanya na za kwenu. Saa ya ukombozi ni sasa. Msikubali kamwe kulamba matapishi yenu wenyewe. Acheni msimamo wenu wa kuwa na serikali 3 ubaki hivyo hivyo. Nina imani kwamba kipindi mnatoa maoni yenu mlikuwa watu wazima na mlikuwa na akili timamu. Wapuuzeni hao wanasiasa wanaotaka kuchakachua maoni yenu kwa maslahi ya mafisadi na wachumia tumbo wachache. Wekeni maslahi ya nchi mbele ya maslahi ya chama. Vyama vinazaliwa na kufa lakini taifa la Tanzania litadumu milele. Tafakari, chukua hatua!
 
Chama tawala nchini Tanzania, CCM bado kinaonekana kuendeleleza sera yake ya kupinga muundo wa serikali tatu ambao hivi sasa unapendekezwa pia katika rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa mwanzoni mwa wiki iliyopita. Itakumbukwa kwamba hapo kabla tume mbili zilizoundwa zilipendekeza mfumo wa serikali tatu katika muungano kati ya iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar lakini mapendekezo yao hayakutekelezwa .

Rasimu ya Katiba Mpya imezingatia maoni yaliyotolewa na wananchi wa Tanzania ambao ndio wenye maamuzi juu ya hatima ya nchi yao. Tume ya Nyalali na Jaji Kisanga zilipata maoni kutoka kwa wananchi, ambao ndio waliotaka uwepo wa serikali tatu. Inasikitisha kwamba CCM wanataka kuwaamulia wananchi aina ya serikali wanayaoitaka wao. Huku ni kusigina demokrasia na ni dharau kubwa kwa wananchi. Siku zote CCM inadhani kwamba wananchi ni mazezeta na kwamba hawawezi kujiamulia mambo yao wenyewe. Sasa ikiwa wananchi ndio wanaotaka serikali tatu, iweje kikundi kidogo cha wanachama wa CCM wajifungie chumbani huko Dodoma na kuazimia kuchakachua maoni ya wananchi?

Nchi hii ina jumla ya watanzania million 45. Wanachama wote wa CCM hawazidi million 5! Iweje kikundi cha watu million 5 watake kuchakachua maoni ya watanzania million 45? Hii ndiyo demokrasia kweli? CCM wanataka kubaka maoni ya wananchi kwa manufaa ya mafisadi wachache kama walivyozoea kuwatumikia mafisadi huku wakiwaacha solemba wananchi. Hii haikubaliki hata kidogo. Ifike wakati wananchi waone kwamba CCM haiweki maslahi ya wananchi mbele isipokuwa wanalinda maslahi ya wachumia tumbo wachache ndani ya chama na serikali. Hii maana yake ni kwamba serikali haina nia njema na ustawi na mustakabali wa wananchi bali inawatumia kama ngazi ya kutimizia haja zao za kiutawala na kinyonyaji!

Maoni yaliyozaa rasimu ya katiba hii yalitolewa na wananchi wote bila kujali dini, kabila, kanda, vyama, jinsia au hali zao. Kwa hivyo, sio busara hata kidogo kwa CCM kuwaelekeza wanachama wake wakatae muundo wa serikali 3 wakati ni wanachama hao hao ndio waliohojiwa na kukubali kuwa na muundo wa serikali 3! Kufanya hivyo ni sawa na kuwashikia akili watanzania na kuwaona kama hawakuwa na akili nzuri wakati wanatoa maoni ya kuwa na serikali 3. Na nitawashangaa sana wananchi na wanachama wa CCM watakaokubali kushikiwa akili na kubatilisha maoni yao ya awali ya kuwa na serikali 3.

Tujiulize ni kwa nini tume zote tatu (Tume ya Warioba, Jaji Kisanga na Nyalali) waliamua kukusanya maoni ya wananchi badala ya kuwaachia CCM wawaamulie wananchi kama wanavyotaka. Kama hali ni hiyo basi ni bora tume hizi zisingeundwa na kutumia mamilioni ya walipakodi katika kusaka maoni ya wananchi. Basi tungewaachia CCM (wajuzi wa kila jambo) wajifungie ukumbi wa Chamwino huko Dodoma watuamulie watanzania aina ya katiba tunayopaswa kuwa nayo-jambo ambalo ni kubaka demokrasia waziwazi.

Enyi wanaCCM/wananchi, akili za kuambiwa changanya na za kwenu. Saa ya ukombozi ni sasa. Msikubali kamwe kulamba matapishi yenu wenyewe. Acheni msimamo wenu wa kuwa na serikali 3 ubaki hivyo hivyo. Nina imani kwamba kipindi mnatoa maoni yenu mlikuwa watu wazima na mlikuwa na akili timamu. Wapuuzeni hao wanasiasa wanaotaka kuchakachua maoni yenu kwa maslahi ya mafisadi na wachumia tumbo wachache. Wekeni maslahi ya nchi mbele ya maslahi ya chama. Vyama vinazaliwa na kufa lakini taifa la Tanzania litadumu milele. Tafakari, chukua hatua!

Changa la macho hilo! 2015 uchaguzi na Wazanzibari ni turufu kubwa kwa CCM. Mfumo wa serikali tatu utawaumiza viongozi wa CCM Zanzibar ambao wanategemea fedha kutoka Tanganyika. Ukija mfumo wa serikali 3 huenda CCM Tanganyika ikawaacha mkono wale wa Zanzibar hivyo kula ya viongozi wa CCM Z'bar itakuwa mashakani. Na huku CCM Tanganyika viongozi wake wanataka baraka za CCM Z'bar. Sasa unafikiri nani atachomoza na kushabikia serikali 3 huku akikumbuka yaliyomkuta Kikwete hapo nyuma?
 
tpaul CCM ndo Chama tawala kwahiyo wao ndo dira ya nchi. Endapo maoni yenu yanakataliwa ujue mnatoa maoni yasiyo jenga nchi. Sasa kama chama lazima kikatae kwa nguvu zote hata kama pendekezo liletwe mara miamoja, jibu likiwa NO! ni NO! Isitoshe hao member 5,000,000 wa CCM ndo wapigakura wakizidi na wengine labda inafika 8,000,000. Kwahiyo hao 3m hawana ubavu kwa 5m! kupitisha jambo la nchi yote!
 
Last edited by a moderator:
Brightman Jr, kwanini sasa tume iliundwa kutafuta maoni ambayo hayatafanyiwa kazi? Huoni kwamba huku ni kupoteza pesa za umma kwa manufaa ya mafisadi wachache?
 
Back
Top Bottom