CCM difinisheni gani utaipa?

Nimesikia na kusikiliza mengi ila hili jina la CCM naona limebeba urefu wa maneno mengi kila mmoja na tafsiri yake ukilinganisha na vyama vingine vya siasa.
Maana zipi ambazo unazozijua wewe?kama si mamneno ya kihuni ambayo hulwetwa na wapinzania waio na hoja??
Je wewe kama mfuatiliaji wa siasa za Tanzania na vyama vyake kutokana na hali ilivyo tokea unapokumbuka mpaka hii leo conclushen yako ni nini juu ya kirefu cha CCM zaidi ya msemo maarufu wa " CHAMA CHA MAPINDUZI
wewe unataka iwe na kirefu kipi???Mbona maana ya CHADEMA ni Chama cha Demokrasia Makini.Haujasemee vyana vingine kama TLP ambavyo kirefu chao hata si cha kiswahili..Hoja yako ni zaifu na naijibu kwa ufasaha huku nikitabasamu
Kwa upande wangu nimeona kirefu na mabacho kinabeba uzito ulio na maana ya kina kabisa ni CHAMA CHA MATAPELI.
hili ndilo lilikuwa lengo la thread yako,si ungesema tu mapema,Unmaleta Vioja sasa.
Chama cha matapeli CCM kinautapeli tokea kwenye uchaguzi mpaka kwenye majukwaa,Raisi Mkapa ni tapeli mawaziri wake matapeli haya madili makubwa makubwa yote wamefanyiana utapeli wenyewe kwa wenyewe.
Mzee Mkapa Amekuwa Tapeli toka lini,Tuoneshe ni utapeli upi aliowahi kuufanya na ni wangapi aliwatapeli.
Kikwete amewatapeli wananchi kwa kuwaahidi maisha bora kwa kila Mtanzania wananchi walio wengi wakainunua sera ya kasi mpya nguvu mpya na ari mpya ,leo jamaa anapanda paipu akielekea maulaya utazani anaenda kulala zamu (ameoa wake zaidi ya mmoja
Sera ya maisha Bora ni sera ya chama cha Mapinduzi na kamwe usidhani Maisha Bora yanaletwa na Viongozi,mathalani Jk.Tumlaumu kwa kushindwa kusimamia Sera ya Chama na si vinginevyo,Maisha Bora Yanaletwa kwa kujituma kwa kila mtu na kufanya kazi kwa bidii huku tukipinga ufisadi unaofanya na mtu yeyote aliyemdogo ana anayejiona ni mkubwa!
Sijui nyie wengine mtaiona vipi maana ya CCM ,hebu elezeni vile muionavyo CCM ,dah chama hakina dira wala lengo ni wizi tu !!Kila unapopagusa basi wameshapita na kumega !!!
Mie naiona CCM kama chama kinachobadilika kila siku,Kina muelekeo tofauti na vyama vingine ambavyo vimeshindwa kustahimili,si kwa kukosa pesa ila kwa kushindwa kuzieleza Vyema Sera za vyama vyao.Poleni sana kwa hili.Mwiba,Nahitimisha kwa kukusihi sana kusoma ujembe huu na kuulewa La msingi si kuwarudisha nyuma wanaotajirika kwa njia halali, bali kuwasaidia wanaofukarika
 
Mkuu Gembe

Mnachoongea sijui kufanya kazi kwa bidii na maisha bora kwa kila mtanzania inakuwa ni ndoto.

Kama kweli mnataka tusiwaite majina hayo hamna budi kukamatana ndani ya chama. CCM ni chama kinachofuga majambazi. Angalia mfano mdogo tu mtanzania anayefanya kazi ya kwa bidii anakusanya vijisenti vyake.

Wale walio katika maadili ya chama wanapiga dubious moja garama ya umeme inapanda mara mbili. Na hiyo gharama inakwenda kwa mwananchi anayeshinda anapiga mzigo ili kupata maisha bora. Hayo pia yako katika vitu vingine.

Hiyo kufanya kazi kwa bidii mnataka tuwafanyie nyinyi wenye Chama cha majambazi?

Mnataka mtanzania afanye kazi vipi?

Tumechoka na misamiati yenu migumu ambayo haiendani na vitendo.

Hivyo hivyo Mwenyekiti Wa Chama CHa... mstaafu alikuwa anazunguka na kupiga Lecture za utangawazi na kutufanya watanzania kama vile hatuelewi maana Utandawazi, tukashangaa.

Lakini kumbe yeye alikuwa anaongea lugha tofauti, alimaanisha utandawizi(hicho ndio chama kinachotuelekeza tutapata maisha bora kwa kufanya kazi kwa bidii)
 
CCM ina wanachama Milioni 3 nchi nzima ina maana wote hao ni mafisadi?Kuna wana CCM wazalendo kabisa wanaokerwa na Ufisadi,rushwa na hila zote za kuvuruga Chama!Kama kuna Mwana Chadema mla rushwa ina maana chadema yote haifai?

Heshima Mbele Mkuu, kuwa na wanachama milion 3 hata kama sio mafisadi lakini wanaongozwa na timu iliyobobea kwa ufisadi maana yake hata hao wanachama wamefumbwa midomo yao kushindwa kuwaambia viongozi wao kuwa basi mmeshindwa kutuongoza achieni ngazi (labda nasikia umoja wa vijana Tanga wamedai waliohusishwa na ufisadi waachie vyeo vyote walivyobakiwa navyo, nayo ni sawa na kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala) Chama imara ni kile wanachama wake wanaweza kuwaengua viongozi waliowachagua pale wanapovurunda ref. Gordon Brown alivyopigwa mweleka wa chaguzi za Serikali za mitaa
 
Maana zipi ambazo unazozijua wewe?kama si maneno ya kihuni ambayo hulwetwa na wapinzania waio na hoja??

Hakuna maneno ya kihuni ila yote yamebeba maana inayolingana na sifa za CCM ni sifa ambazo zinajieleza wazi na mifano ndio kama inavyotolewa tena kwa ufupi zaidi.

wewe unataka iwe na kirefu kipi???Mbona maana ya CHADEMA ni Chama cha Demokrasia Makini.Haujasemee vyana vingine kama TLP ambavyo kirefu chao hata si cha kiswahili..Hoja yako ni zaifu na naijibu kwa ufasaha huku nikitabasamu

Kirefu cha CCM kwa lugha ya kigeni ipo na hutumika katika habari za magazeti ya kizungu .. Revolutionary Party ( RP ) kama sijakosea.
Mimi kama nilivyosema siwezi kumaliza kwani kadiri nitakavyosema bado maana zake haziwezi kumalizika kwa leo au kesho mfano nikisema CCM ni Chama Cha Mizengwe..si uongo muwafaka juzi wameupiga dafrau ,maneno yote waliyokuwa wakiyasema viongozi wake wa juu kwamba umefikia mwisho yameonekana ni uongo na walikuwa wakifanya usanii tu.

Hili ndilo lilikuwa lengo la thread yako,si ungesema tu mapema,Unmaleta Vioja sasa.

Hapana sio lengo bali ni kuona WaTanzania wengine wanauelewa wa aina gani juu ya CCM na maana halisi iliyopo juu ya utawala wao miaka mingi tu iliyopita hadi hii leo ,na kama ulivyoona na unavyoendelea kuona ni jinsi gani CCM inaonekana mbele ya macho ya waTanzania ,jaribu kusoma between the line na upime kwa kina the real picture ya CCM.(Chama Cha Masaibu) Si unaona Taifa linavyopita shida na taabu mbali mbali na wapi tunapoelekea.

Mzee Mkapa Amekuwa Tapeli toka lini,Tuoneshe ni utapeli upi aliowahi kuufanya na ni wangapi aliwatapeli.

Unajua CCM kimeanza kupiga chenga na kuwatwisha wanachama wake kuwa haya yanayotokea ni yao peke yao ,lakini si kweli ukweli samaki mmoja akioza basi wameoza wote na ushahidi sio mwanachama mmoja wa CCM aliebakwa ndani ya tuhuma hizi za ufisadi ni wengi tena wengi sana.
Kitu kimoja haya mambo ya kuitana Mzee ,Muheshimiwa haya ndio mambo yanayowarudisha nyuma ,maana ukianza Mzee sijui Muheshimiwa hapa unapoteza power ya kupigania haki ,itakubidi uanze kutoa Shikamoo na kupinda magoti ,unaona hatari inayowakabili CCM na wengine nikimaanisha tabia hii iachwe mara moja hata kwa vyama vingine,mfano utaona katika nchi za ulimwengu wa kwanza au zilizoendelea Mr President hakuna muheshimiwa Raisi Kikwete kuna yule wa Uingereza Mr Brown au Gordon anaitwa mtu kwa jina lake hakuna mambo ya kutanguliza your highness na viraka vingine ,hapo ukianza kutanguliza basi ujue tayari unapoteza nguvu flani flani mbele yake na wewe unakuwa kama unazungumza na baba au mama yako atakalokwambia ndio ulifuate, Yaani jamaa wananiacha hoi kabisa utawasikia Basi Mzee jamaa wamesema .. basi Muheshimiwa..ni ovyo kabisa.

Mkapa alilitapeli Taifa hili kwa kujengesha mgodi misaada mingi ilitolewa wakiamini mradi ni wa Taifa Changa la Tanzania kumbe jamaa alikuwa na agenda za siri utakapokamilika ataununua na ndivyo alivyofanya tena kwa bei ya chini ambayo huenda hadi hii leo deni bado hajalimaliza wakati anateka faida.
Kuhusishwa kufanya biashara Ikulu huku amewatapeli wananchi alipokuwa akidai kura na kuwambia atakuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi yao na ya Taifa ,akiwaeleza na kuwalisha wananchi waliojaa kumsikiliza maneno matamu ,Ikulu amekwenda kufungua ofisi ya kupitisha miradi yake huo kama si utapeli ni kitu gani ?Huyu amejenga Nyumba juu ya mlima ambayo imezungukwa na mbuga inasemekana anaenda kwa helikopta au gari maalumu ,kwao Mtwara waulize wa Mtwara wakupe hiyo,wewe kaa hapo ukisema CCM ndio baba chini umevaa ndara rangi tofauti..!

Sera ya maisha Bora ni sera ya chama cha Mapinduzi na kamwe usidhani Maisha Bora yanaletwa na Viongozi,mathalani..

Naona hujui unalolizungumza Chama ndicho kinachotarajiwa kuleta Maisha bora ndio ukaona wamezunguluka nchi nzima kueleza nini watafanya nini wamepanga ili mwananchi awe ni mfanya kazi waliahidi makazi kwa maelfu ..hata jua halijakuchwa wameanza kuja na sera za ubinafsi ,wananchi wameachishwa kazi,sasa umekusudia watu wajitme yaani watu wote wakamate jembe wakalime ndio CCM mtaona mmeleata maisha bora kwa kila Mtanzania ,ndugu kuna watu wanalipwa tu ikiwa huna kazi na hutaki kufanya kazi wewe utakuwa kila mwisho wa mwezi unapokea burungutu kutoka serikalini ,uliza usifikiri tunasema ndoto hapa !!Ikiwa serikali imekisia mlo wa mtu mmoja kwa mwezi ni 50,000 Tsh basi serikali inawajibu wa kuwalipa WaTanzania wote wasio na kazi kiasi hicho cha fedha kila mwisho wa mwezi.Unaweza kuuliza fedha hiyo ingetoka wapi ,ila ukitazama huo ufisadi na fedha ambayo hesabu zake zimepatikanika basi utaona uwezo huo unakuwepo kwa serikali au Chama kilichoahidi kikikamata madaraka kitaleta maisha bora kwa kila Mtanzania ,Chama kingeliweza kuwapatia wanafunzi mlo mashuleni ,Chama kingeliweza kuwafundisha wanafunzi wavyuo vidogo na vikuu bila ya kuwadai vijisenti .Je wapi CCM ipo na wapi huduma hizo zipo. Hapa huwezi kumlaumu Lowasa au Chenge hapa kinaingia Chama chote kizima kizima kikianzia na Mwenyekiti wake ambae ndio mshika bendera hadi kwa mwanachama aliepigia kura na kuipa CCM ambae amedanganywa kumbe ametapeliwa haki yake,kwa kuipeleka kura yake kwa Mafisi na chama chao.Hakuna cha mdogo wala mkubwa CCM wanaogopana wenyewe kwa wenyewe halafu unasema watu wapinge watakaopinga ni hawa hawa waliomo nje ya CCM lakini waliomo ndani hata akifika kusema basi ujue ana mtandao ambao uko nyuma yake wanaongojea mkono usimamishwe kwenda kinywani wapate kuwahi wao.

Mie naiona CCM kama chama kinachobadilika kila siku,Kina muelekeo tofauti na vyama vingine ambavyo vimeshindwa kustahimili,si kwa kukosa pesa ila kwa kushindwa kuzieleza Vyema Sera za vyama vyao.Poleni sana kwa hili.Mwiba,Nahitimisha kwa kukusihi sana kusoma ujembe huu na kuulewa La msingi si kuwarudisha nyuma wanaotajirika kwa njia halali, bali kuwasaidia wanaofukarika
Kuwa na muelekeo tofauti ni kutokana na njia na mipango yao kuwa inakaribia mwisho kwani kila wanakokukamata wanaonekana, sasa wamebaki kubahatisha labda tukifanya hivi tutapata afuweni na kuweza kupumua mbele ya macho ya wananchi ambao wamekodoa mimacho kuwatizama wanapokimbilia mara wamekaa na kukutana kwa siri kuambizana nyie bora mjiuzulu,hawajakaa vizuri limezuka jingine ambalo ni hatari zaidi na kuhatarisha hata yale waliyoyapanga maana kama walipanga Lowasa ajiuzulu yeye na wenziwe yaishe sasa kuna hili jingine ambalo nalo jamaa amekwisha jiuzulu nae ni mwenzetu huyu tukimfunga hatokubali maana na wale kina lowasa bango ni hili hili la Ufisadi itakuwaje yaani hata hawajamaliza kuziba la chenge na kulichnaganya vizuri kuna la kasisi mKuu Mkapa nalo linachemka na tatizo kubwa ambalo wananchi wanaliangalia kwa makini ni hizi mbio zitaishia wapi ,mbio za kulindana ,mbio za huyu ni mwenzetu sera hizi mbovu ndizo kinakifanya Chama hiki CCM ni Chama Cha Mazezeta.
 
[/COLOR]Chama imara ni kile wanachama wake wanaweza kuwaengua viongozi waliowachagua pale wanapovurunda ref. Gordon Brown alivyopigwa mweleka wa chaguzi za Serikali za mitaa[/QUOTE]
Mkuu kumbuka CCM sio chama cha kihuni, kina endeshwa ka katiba na demoklasia ya hari ya juu,Huwezi kuamka tu asubuhi na kuwafuta watu uwanachama. wanachi waliomchagua kiongozi ndio wananguvu ya kutomchagua next tima kama watazani kiongozi huyo alishiriki katika vitendo vya kihuni.
 
Inategemea na mwaka:
1977-1987 - Chama Cha Mapinduzi
1987-1995 - Chukua Chako Mapema
1995-2005- Chama Cha Ma------ (naogopa kumalizia)
2005-20-- Sielewi kabisa
 
Hapo mwanzo nilikipenda Chama Cha Mapinduzi lakini kwa sasa nashindwa kuelezea mazuri ya chama hiki kwani wanaokiongozi, maadili wamejifunza kwa kusoma si kutenda. Hadi nasema hivi tayari ninazo tafsiri zangu kuhusu kirefu cha CCM
1. Changamkia Chako Mapema
2. Chama Cha Makanjanja
3. Chinja Chinja Makini
4. ChuChuMaa (Mkao wa kula lakini tayari kwa mbio)

Hakika hadi sasa hatuna mtu makini mwenye uwezo wa kukemea maovu ya wanachama wake, kila mmoja anaona yuko sawa kufanya anavyotaka. Nuru ya rangi ya kijani imeanza kufifia na hii inaashiria mmea huu kukosa jua. Jua lilishazama mwaka 1999. Sasa hivi ni gongana tu. Hata hivyo JK anatakiwa kutimua baadhi ya watendaji wadogo hawa lakini siyo hiyo staili ya kubadilisha MBELEKO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…