LGE2024 CCM Dodoma Mjini Yaanza Kuwanoa Mabalozi Kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 CCM Dodoma Mjini Yaanza Kuwanoa Mabalozi Kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.33.jpeg

▪️Kukutana na Mabalozi zaidi ya 2000

▪️Mabalozi wagawiwa vitendea kazi

▪️Mwenyekiti Mamba awataka kuhimiza wanaCCM kushiriki uchaguzi

▪️Mbunge Mavunde awahimiza kuhakikisha ushindi wa CCM

𝐃𝐎𝐃𝐎𝐌𝐀

Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Dodoma Mjini kimeanza mikutano ya ndani ya kuwajengea uwezo wenyeviti wa mashina(Mabalozi) kuelekea Uchaguzi wa serikali za mitaa kupitia mafunzo na elimu juu ya umuhimu wa kushiriki uchaguzi kikamilifu.

Mikutano hiyo inayofanyika kitarafa inawakutanisha mabalozi zaidi ya 2000 wa kata mbalimbali ambapo mabalozi wamepata fursa ya kupewa elimu ya uchaguzi na kujengewa uwezo katika masuala ya uchaguzi ikienda sambamba na ugawaji wa vitendea kazi.

Soma Pia:
WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.34(1).jpeg

Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Dodoma Mjini Cde Charles Mamba leo ameongoza mkutano wa mabalozi kwa Tarafa ya Kikombo katika mkutano uliofanyika katika ya Ihumwa na kuwahimiza mabalozi hao kuhakikisha wanaCCM wengi wanajitokeza kushiriki uchaguzi na kuchagua viongozi ifikapo tarehe 27.11.2024.

“Tumefanya vizuri kwenye kujiandikisha kwenye daftari la wakazi,sasa twendeni tukashiriki kwa uwingi kwenye uchaguzi wa serikali Za mitaa ili huko nako tufanye vizuri“ Alisema Mamba

WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.36.jpeg

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde amewapongeza mabalozi kwa kazi nzuri waliyofanya ya kuhamasisha uandikishaji wa daftari la wakazi na kuwataka kutumia ushawishi mkubwa zaidi kushawishi ushiriki wa idadi ya wanaCCM ili kuwezesha CCM kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa.

Uongozi wa CCM Wilaya umemshukuru Mbunge Anthony Mavunde kwa kuchangia vitendea kazi kwa mabalozi ikiwemo sare 2000 na bendera 2000 kwa mabalozi wote wa Jimbo la Dodoma Mjini

WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.38.jpeg
WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.38(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.33(1).jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.34.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.34.jpeg
    182.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.35.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.35.jpeg
    181.8 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.36(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-06 at 18.46.36(1).jpeg
    142.4 KB · Views: 2
Wanawafundisha jinsi ya kutoa hongo na kujumlisha rushwa kwa wapiga kura?
 
Back
Top Bottom