Mzee wa Code
Member
- Sep 23, 2024
- 61
- 91
Kuna vichekesho vinaendelea nchini hii vya ukiukaji wa sheria, kwa hoja za dhaifu sana eti kukosa kupigiwa kura na ujinga huyu unaongozwa na watumishi wa halmashauli kwa kuwasikiliza viongozi waliopata vyeo kwa nafasi za uteuzi, kuna hii tabia imekuwa ikifanywa na halmashauli nyingi nchini kuwaacha wafanyabiasha kujenga sehemu zisizokuwa rasmi nyakati hizi za uchaguzi mbalimbali.
Tabia hii uvunjaji sheria imekuwa ikifanyika na wananchi inaachwa kwa hoja ya kupigiwa kura lakini baada ya uchaguzi kumaliza watumishi na serikali ya CCM hurejea kuwavunja wafanyabiasha ambao kwa sasa wanawaona wanavunja Sheria ila kwa sababu ccm inatafuta huruma ya kupata kura wanawaacha alf baadde wanakuja kuwasababishia hasara kubwa watanzania kwa kuendesha bomoabomoa kwa kugezo kuwa wamejenga sehemu sio sahihi.
Mfano nimechukua mkoa wa Dodoma ambapo kumejengwa soko la machinga lakini kwa sasa wafanyabiasha wameanza kuzagaa mitaani na mamlaka zimekuwa zikiwaangalia tu, lakini sababu kubwa ni Hofu za uchaguzi, CCM acheni huruma ya kutafuta kupigiwa kura kwa kuacha makosa yafanyike alf Baade msababishe hasara na usumbufu kwa wananchi.
Kuna eneo linatwa njia ya panda ya area c, hapa kwa sasa imekuwa stendi ndogo ya kupakia na kushusha abaria ene ili limewekwa banco nabiça kuwa hakuna shughuri zinaruhusiwa, kama biashara, kupaki magari lakini kwa kuwa ccm inatafuta huruma kwenye chaguzi wameacha sheria zivunjwe na baada ya uchaguzi watakuja kuwaondoa wananchi eneo kwa Nguvu, ccm na Mkurungenzi wa jiji la Dodoma simamieni Sheria kikao chenu na Mkuu wa Mkoa kuwa "waacheni tutakosa kura" ni woga amjiamini
Mpango wenu kuwa mtaendesha bomoabomoa baada ya uchaguzi 2025 tumeshaujua kina madeleka mjiandae tu mtatueleza kisheria.
Mpango wenu kuwa mtaendesha bomoabomoa baada ya uchaguzi 2025 tumeshaujua kina madeleka mjiandae tu mtatueleza kisheria.