Msanii ajifungua katika mkutano wa kampeni
Thursday, 16 September 2010 08:17
Frederick Katulanda, Sumve
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida msanii na mwachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shinje Mataifa (25) amejifungua mtoto wa kiume katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa chama hicho Jimbo la Sumve wilayani Kwimba Richard Ndassa.
Mwanamke huyo ameamua kumwita mtoto huyo jina la Ndassa ikiwa ni ishara ya kumbukumbu ya tukio hilo la kujifungua katika kampeni za uchaguzi mwaka 2010 ambapo alisema mgombea anayemuamini ni Ndasa..
Tukio hilo lilitokea saa 10 jioni wakati Shinje akiwa miongozi mwa wasanii wa vikundi vya CCM ambavyo vilialikwa katika kampeni hizo ili kutumbuiza mkutano huo.
Akisimulia tukio hilo Shinje alisema kuwa alifika katika eneo la mkutano huo saa 4:00 asubuhi akiwa na wasanii wa ngoma za asili wa kikundi cha Masaligula ambapo walikuwa wakitoa burudani, lakini ilipofika muda huo (saa 10 jioni) alianza kijisikia vibaya na baada ya kuona anazidiwa aliamua kutoka eneo hilo, lakini alishindwa kuendelea mbali kutokana na kuzidiwa uchungu.
"Nilikuja katika kampeni nikiwa mjamzito. Lakini, sikujua kama hali hii itanitokea, tangu nilipofika nilikuwa nacheza ngoma, lakini baadaye hali yangu niliona inabadilika sana, kwanza nilidhani kuwa ni maumivu tu, lakini wakati nataka kwenda nje ya uwanja huo kutafuta msaada, hali ilibadilika na kuwa hivyo," alisimulia Shinje.
Kufuatia hali hiyo Shinje alizungukwa na wanawake wenzake waliotumia kanga za kampeni zilizokuwa na maneno ya Chagua Kikwete kuweka uzio na kugeuza uwanja huo wa kampeni kuwa wadi ya uzazi kwa muda ambapo baada ya kujifungua salama alipelekwa katika Zahanati ya Nyambiti kwa matibabu zaidi.
Muuguzi wa zamu katika Zahanati ya Nyambiti, Josephina Barnabas alithibitisha kumpokea Shinje akiwa katika hali nzuri na kumpatia huduma nyingine za kitabibu ambapo alisema kuwa mtoto huyo(Ndassa) amezaliwa na afya njema na anaendelea vyema.
Akizungumza tukio hilo la kujifungua kwa mama huyo katika mikutano yake ya kampeni mgombea ubunge jimbo hilo la Sumve, Ndassa alisema amelipokea kama Baraka na ishara ya kuzaliwa upya katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Comments
0 #7 jonas 2010-09-16 14:20
mama mbumbumbu na masikini kama huyu huenda alijua muda umefika lakini hana kitu tokana na ccm ya kina ndasa. watanzania fikirini ma 2 mafisadi wanatuumiza. hukumu ya mabadiliko kisiasa ktk sanduku la kura. woga wa mabadiliko tuache ili tuendelee. ccm wamejenga tabaka la makabwela mpaka wanafungua benki ya makabwela, hamuoni [NENO BAYA] hayo? hawana nia ya kuwakomboeni.
Quote
0 #6 juma ngole 2010-09-16 13:40
Akizungumzia safari ya hivi karibuni mkoani Mara ambapo Mama Salma alitumia ndege ya serikali, Kinana alisema CCM ililipa Sh. 22,950,000."NIPASHE YA LEO 16/09/2010"
SUALI KANGU: KAMA MAMA SALMA ANALIPIWA NA CCM PESA ZOTE HIZO, NINI FAIDA KWA MTANZANIA WA KAWAIDA, HASA TUKIJUA KWAMBA MAMA HUYU SI KWAMBA NI MSOMI, WALA MEMBER WA CC YA CCM, WALA HANA MCHANGO MAALUM UNAOJULIKANA, NI MWALIMU TU WA PRIMARY SCHOOL-NINI PICHA TUAYOPATA WA TZ? SI NI UNYONYAJI MKUBWA MNO??? DUU HII KALI. NADHANI AKILI YA HUYU MAMA NI NGOGO KULIKO YA MUMEWE! HUU NI UFISADI NDANI YA CHAMA KABISA.
Quote
0 #5 Mwananchi Mwema 2010-09-16 13:31
Huyo mama hana hata mume. Kama anaye basi hatimizi wajibu wake.
Angekuwa mke wangu ningempa taraka.
Quote
+1 #4 Isaya 2010-09-16 12:48
Afanyeje jamani huyu mama, hakuwa na khanga ya kumpokea mtoto angalizaliwa, sis em wamempa kwa malipo ya kura angeacha si angepokonywa! kama ana mpango na mtoto mwingine inabidi aibebe mizi tisa kabla ya kampeni za 2015 wakati atapopewa khanga ingine. Kwa ufahamu huu bado kazi ipo watu aina hh kuelewa sentesi za kisomi km za dk wa ukweli. Tuombe mungu afanye maajabu.
Quote
+2 #3 lapa 2010-09-16 12:34
alijijua yupo taabani lkn nyumbani hamna kitu,afenyeje sasa wkt kuna mkutano wa sisiemu ambapo wanalipwa, hivyo vijihela ndio aalikuwa anavitegemea kujiandaa kununulia beseni,nepi na vinguo vya mtoto
Quote
+1 #2 Debby 2010-09-16 12:29
Stupid kabisa we mama, unaacha kumuomba msamaha huyo kachanga eti unafurahia na kumpa mtoto jina la haramu.
huwezi kuwa mama mwenye malezi mema usiyejijali hata wewe mwenyewe, unaenda kucheza ngoma na mimba ya miezi 9 kweli harafu sheria ipo kimya!.....
kweli hii ccm!.
Quote
+1 #1 Dulla 2010-09-16 09:41
Huyo mwanamke ni careless! huwezi kwenda kucheza ngoma na mimba ya miezi tisa! alikuwa anatafuta balaa tu! sheria za nchi hii zimelala, nchi nyingine angeshtakiwa kwa kuhatarisha maisha ya mtoto
Quote