Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Sikumbuki ni lini baada ya uchafuzi mkubwa wa kilichoitwa uchaguzi wa serikali za mitaa, CCM ilisikika tena popote! Hata matukio ya kutengenezwa ili kuiweka ccm kwenye ramani ya mijadala yalikufa mimba changa...
CCM imeumilaliza mwaka 2024 kinyonge na kwa udhaifu mkubwa.. Bila nuru usoni wala matumaini ya ule urijali wake wa kibabe
Bundi ametua kwenye paa la chama chawala.. Bundi ni ndege awezaye kunusa harufu ya kifo toka mbali kwenye nyumba yenye mgonjwa anayeelekea kifoni.. Bundi huja kuweka kikao karibu na hapo akitarajia mzoga wa marehemu baada ya kifo
Kwa spidi ile ile mwaka 2024 umelala na CHADEMA na kwa spidi ile ile mwaka 2025 umeamka na CHADEMA..kama ni upper punches na knockouts CCM mbele ya CHADEMA imezipata za kutosha sana.. Basi tu ni kwa vile refa ana huruma nyingi na mbeleko kubwa. Lakini tayari muda huu CHADEMA wangeshavikwa taji lao
Hakuna tena kitu kinaitwa ccm midomoni mwa watu hasa Watanganyika..
Hata makada wake maarufu mitandaoni na nje ya mitandao wote wametekwa na kimbunga kikali cha CHADEMA!
Hizi ni dalili za anguko kuu na la mwisho la kilichowahi kujulikana kama CHAMA Dume mbabe wa fitina na majungu
Hakuna tena kitakachoirudisha CCM hewani maana tayari jahazi lake linaishia kuzama na kama ni mgonjwa ni yule mahututi anayepigania pumzi yake ya mwisho isitoke kwa maumivu
CHADEMA KIMEIFUTURU CCM BILA BISMILLAH..!
sucker punch 👌🏿