Kiwalani finest
Member
- Jul 6, 2024
- 97
- 72
Serikali ya CCM inawekwa na wananchi baada ya kuridhia CCM iwe chama tawala. Hatupaswi, wanachama wa CCM, kuonekana na mionekano ya kimaskini na ombaomba.
Wakili Msomi na Jasiri, Boniface Anyisile Mwabukusi, Rais wa TLS, nakumbuka tarehe 05/10/2024 alisema:
"Lazima tuwe na sehemu tunapokutana na kuzungumza. Kwa sababu katika mazungumzo ndiyo mahali panapotupa fursa ya kila mmoja kuelewa na kutambua kile ambacho mwenzake amekifanya. Na kupitia hapo tunakubaliana kwa pamoja twendeje. Na tunapokutana kwa pamoja na kukubaliana twendeje, unapomuona mwenzako akienda tofauti, wote tunasema sasa wewe sio mwenzetu."
Mwisho wa kunukuu.
Kamanda Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, nakumbuka tarehe 05/10/2024 alisema:
"Nimshukuru sana Rais Boniface (Anyisile) Mwabukusi kwa hotuba yake nzuri ambayo nilikuwa naifuatilia mstari kwa mstari. Mtazamo wa TLS ni wa kuangalia nchi kuliko kuangalia makundi tofauti tofauti kwa nafasi tofauti."
Mwisho wa kunukuu.
Nayaandika yote haya kusisitiza kuwa sisi kama chama tawala tuna jukumu la kuuondoa umaskini kwa nchi na kwa mwananchi mmoja mmoja. Kazi tutaifanya kwa vitendo na si kwa maneno matupu. Na kazi hii haiwezi kupata ufanisi stahiki ikiwa wanachama wa CCM wataachwa kuwa na njaa huku tukiwataka wawe waadilifu na waaminifu wakati wanashinda na njaa.
Ni lazima sasa pawepo mikakati ya kuangalia kama chama tulipojikwaa, tukubali tumejikwaa na tuparekebishe. Hivi ni nani asiyejuwa kuwa miongoni mwetu watu walio wengi hawana kazi za kufanya na hivyo kulazimika kupangwa safu kwa wajanja na kutumika kijinga kusiko na maslahi kwa chama?
Turudishe makali ya chama. Nyakati zingine tuwe tunakaa, tunaweka mijadala na maazimio, kisha yanaandikiwa mihtasari kwa utekelezaji. Sasa hivi sisi ni watawala wa nchi, hatusaidiani. Tunasubiri tuwe nani ndo tuweze kusaidiana kukiimarisha chama. Tunaposema uimara wa chama maana yake wanachama wa CCM nao wanawiri kiuchumi na sio wachache kunawiri na kuwa na furaha ya kufurahia maisha kwa niaba ya kundi kubwa lenye njaa.
Kufokeana sio njia sahihi ya kutatua tatizo, bali njia bora kwanza ni kwa viongozi kujitambua kuwa wanapaswa kuwa wanyenyekevu kwa wanaowaongoza na kuwa tayari kusikiliza mateso na dhiki zao, ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi magumu kwa maslahi mapana ya kundi kubwa lililojawa mambo mengi moyoni, lisilosema.
Nimetoa yangu ya moyoni. Tuyatafakari. Tusiishi kama vile ni watu tuliolishana yamini kuto kubadilika. Tuwaze mawazo mapya ya kuinuana na kukiimarisha chama. Kuweka viongozi ndani ya chama wasio kuwa na kipato kisha kuwapa jukumu la kuwapata viongozi wasiokuwa wala rushwa huku wao nao wakiwa na njaa ni kama maigizo yasiyo kuwa na ukweli ndani yake.
Niiteni viongozi wakuu wa chama na wa serikali ya CCM, tukae niwaonyeshe fedha zilipo za kuondoa aibu hii ya chama tawala kuwa na mionekano ya kimaskini ngazi za shina, tawi, kata, na jimbo. Binafsi nauchukia umaskini mpaka nasikia maumivu ya mwili. Niiteni jamani. Hatuwezi kuwa chama tawala tuna maono ya kuondoa umaskini kwa Watanzania huku wanachama wetu wakiteseka na umaskini na kulazimika kupangwa safu na kuishi maisha ya utumwa kwa aliyewapanga safu wakilazimika kuitikia kila jambo hata kama hawataki.
Kamanda Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, akifanya mahojiano na mwanahabari Odemba, nakumbuka tarehe 05/10/2024 alisema:
"Watu kuongea ni haki yao. Kutoa maoni ni haki yao. Kutoa comments ni haki yao. Recommendation ni haki yao". Mwisho wa kunukuu.
Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2022 ibara ya 5(8), na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara ya 18(a) na ibara ya 19(1) kwa maana ya uhuru wa mawazo.
Nakumbuka tarehe 05/10/2024, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Robert Wilson Makaramba, Ex Mwalimu wa Chuo Kikuu UDSM aliyemfundisha Dkt. Tulia Ackson na Mheshimiwa Kamanda Jumanne Muliro, akiwa katika kongamano kuhusu utekaji lililofanyika Ubungo Plaza Dar es Salaam, alisema:
"Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema hivi: Ukitaka kumuelewesha mtu aelewe, mweleze kama vile unavyomueleza mama yako. Si ndiyo ehee?"
Nimewaeleza kama ninavyomueleza mama yangu. Haiwezekani watoto wachache wale wafurahi kwa niaba ya walio wengi wenye njaa pasipo kuwa na sababu, wakati vyakula vipo tu vinaliwa na wasiokuwa wanafamilia ambao hawakuumia kulima. Watoto kuhisi wamefanywa kama karai ambalo hukenga ghorofa, ila ghorofa likikamilika karai ile hugeuka kuwa uchafu na kutupwa stoo iliyo na makoro koro.
Nikashtuka ndotoni, kumbe nilikuwa naota tu.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Mathias Mugerwa Kahinga