MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Na Gregory J.Mahanju;
Kimekua ni kilio cha muda mrefu sana toka kwa wananchi wa jimbo la Singida Magharibi kuomba ufafanuzi na mchanganuo wa Matumizi ya pesa za mfuko wa jimbo lakini wamekua wakiambulia patupu na majibu ya kejeli kutoka ofisi ya mbunge.
Kuna tetesi kua Mhe Mbunge kama mwenyekiti wa mfuko huo na wajumbe wake wamekua wakiogopa kutoa ufafanuzi wa pesa za mfuko huo kwa sababu ya ufujaji wa pesa hizo na kuogopa kuandika miradi hewa ambayo haikufanywa kwa mfuko huo. Wanaelewa wakiweka wazi mchanganuo wananchi watafuatilia uhalisia wa matumizi na Mradi husika.
Ikumbukwe ya kwamba mwaka 2020 aliwahi kutiwa mbaroni na PCCB Wilaya ya Ikungi na kumhoji masaa kadhaa kuhusu matumizi ya pesa za Mfuko wa jimbo kwenye mambo yake binafsi. Kama haitoshi, Katibu wa mbunge huyo aitwaye Abubakary Muna hivi karibuni pamoja na makatibu wa majimbo mengine ya mkoa wa Singida waliitwa PCCB na kuhojiwa masaa kadhaa juu ya matumizi ya pesa hizo na kupewa maelekezo ya kutoa taarifa kila pale wanapozitumia pesa hizo ili umma uweze kufahamu, cha kushangaza mpaka sasa wapo kimya kabisa wala hawana mpango wa kutoa taarifa hizo.
Inasemekana kua mbunge huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM ndani ya Wilaya hiyo akiwemo mwenyekiti kwa CCM Wilaya ya Ikungi ni wanufaika wakubwa wa pesa za mfuko wà jimbo waligeuza kua pesa binafsi za mbunge.
Ombi la wananchi wa Jimbo la Singida Magharibi kwa Mhe Rais Dkt Samia kama mwenyekiti wa CCM taifa,TAKUKURU Mkoa wa Singida na makao makuu, CCM makao makuu,Polisi na vyombo vingine vya kiuchunguzi kufuatilia ni wapi mbunge huyo anapeleka pesa za mfuko wa jimbo? Kama anaitumia kwenye miradi ya wananchi, kwanini hatoi taarifa kwa umma kama ambavyo wabunge wengine wamekua wakifanya akiwemo Mbunge wa Singida Kaskazini Mhe Ramadhani Ighondo.
Mungu Ibariki Tanzania!
Kazi iendelee!