CCM ifanye nini ili hata isipoondoka madarakani iwe ni sawa tu?

CCM ifanye nini ili hata isipoondoka madarakani iwe ni sawa tu?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Kuna kila dalili kwamba CCM itaendelea kututawala watanzania kwa namna yoyote kwa miaka mingi ijayo, na ukizingatia kwamba mtaani njaa ni kali sana.

Hata kama ingekua ni wewe ndugu yangu, katika mazingira kama ya Tanzania ambapo chama tawala kinahodhi kila kitu serikalini, ungeacha kutumia fursa hiyo kugandamiza wapinzani ili uendelee kula mema ya nchi?

Hata hivyo kuna mambo ya msingi ambayo sisi kama wananchi kwa umoja wetu tukiyapazia sauti angalau hawa watawala wanaweza kutusikia na kurekebisha mambo kuliko kukaa kimya au kulalamika tu na kusubiri CCM iondoke madarakani jambo ambalo sioni dalili likitokea hivi karibuni.

Hivyo nikuombe mdau uorodheshe mambo ambayo unadhani CCM inapaswa kujibadilisha/kubadilika ili yatufae sisi wananchi wote ikiwemo na wa vyama vingine na si CCM peke yao.

Maana hii nchi ni yetu sote si ya CCM peke yao.
 
1- Kupunguza gharama za kuhudumia serikali.

2- Kuwa mlezi/mbia wa sekta binafsi ( serikali iachane kabida na biashara ).

3- Kuruhusu mgombea binafsi, na kusikiliza wananchi.
 
Warudishe FAO LA KUJITOA

Serikali ilipe madeni ya NSSF

Wabunge na Mawaziri wachangie mfuko wa uzalendo, kupunguza mishahara yao
 
Back
Top Bottom