CCM ifanye vetting ya chawa

CCM ifanye vetting ya chawa

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
9,016
Reaction score
24,650
Siku za nyuma kidogo kulikua na tuhuma kwamba kuna watu wameandaliwa na chama tawala kuja kutetea kila kitu kinachofanywa na serikali huku mitandaoni kwa malipo ya shilingi 7000 kwa siku, sina uhakika kama izo tuhuma zilikua za kweli

Lakini matokeo tunayaona mitandaoni, kuna wapambe ambao wamejizima data kichwani na kukubali kutetea kila kitu kwa mategemeo ya kupata reward fulani, miaka ya karibuni wamepewa jina maarufu la "chawa".

Bahati mbaya hakuna vetting inayofanyika kuwapata hao chawa matokeo yake kila mtu anajikuta mtetezi wa chama na serikali kwa mategemeo ataonwa na kulambishwa asali bahati mbaya zaidi hoja zao dhaifu sana na za kutia aibu ivyo kukosa ushawishi wowote kwa mtu ambae yupo neutral katika kudadavua mambo.

Wenyewe wanajiona wanatetea chama kumbe ndio wanazidi kudhihirisha kwamba hicho chama ni cha vilaza. Ushauri wangu kwa CCM fanyeni vetting ya chawa.
 
Hayo malipo ya 7000 sio yetu
Halafu sisi tunashughulika na mambo ya maendeleo hatushughuliki ili tulipwe
Tuna mishahara yetu sie check number zinasoma...... Ole wa wale wanaosubiri wanunuliwe viroba ili wafanye fujo😁
 
Hayo malipo ya 7000 sio yetu
Halafu sisi tunashughulika na mambo ya maendeleo hatushughuliki ili tulipwe
Tuna mishahara yetu sie check number zinasoma...... Ole wa wale wanaosubiri wanunuliwe viroba ili wafanye fujo😁
Wewe ni chawa?
 
CHAWA ni Ishara ya uchafu!!!!

Mnatuambia kuwa viongozi wetu ni wachafu na Wana CHAWA🙃🙃😳😳!!!
 
Chawa anakaa kwenye uchafu.

Hakuna mwenye kujielewa atakaa mahali pachafu.

Ukilaza ni sifa kuu ya chawa. Hivyo kuwa chawa lazima uwe kilaza.
 
Back
Top Bottom