Elections 2010 CCM ifungue kesi ya Kikatiba dhidi ya CHADEMA kuwalazimisha kutambua matokeo!

nikaona Dr Mahanga anasema DR Slaa ni Dikiteta namba 1 na Mpendazoe Namba 2 kwa kukaataa matokeo ya segerea............. mliofuatilia matokeo ya segerea nani dikiteta?
 
Kwa mtazamo wangu naona mgogoro uliopo hapa ni kati ya CHADEMA na NEC sasa,CCM wameingia vipi katika mgogoro huu
 
Sasa hapo amechangia nini?
Ikiwa ameona haijaenda shule basi na alete yake kama hawezi kaa kimya kuliko kusema haijaenda shule.

mkuu unasumbuka na Taso? Browse nyuma uone michango hewa anayochangia. Yeye ni kuchukua post za watu na kuongezea upuuzi kidogo! Wala usisumbuke nae,hachangii anakebei tu!
 
 

kesi hiyo itafunguliwa chini ya sheria gani. Naona unataka kumchokoza katibu mkuu wa ccm
 
si ndo hapo. watu wanaropoka ropoka tu kuhusu katiba. naona ndo limekuwa neno mvuto kwa watu!!

Haropoki, anajua sana anachoandika maana yake ili rais atambuliwe na upinzani lazima kuwe na kesi mahakamani na wadaawa katika kesi watakuwa chadema. Ili ccm washinde itabidi watoe ushahidi ( amabao hawana ) kama rais alishinda kweli na ili kesi utupiliwe mbali lazima CHADEMA watatoa ushahidi ( amabao wanao ) kuwa rais hakupata kura ambazo nec wanasema.

Katika kufanya hivyo CHADEMA watapata jukwaa la uhakuka la kuchambua udhalimu wote uliofanyika kufuatia uchaguzi ( wenzetu wanaita washing the linen in public).

Ndio maana naona kama Mwanakijiji anamchokoza katibu mkuu wa ccm
 

iyo yote naelewa...swali ni simple - hiyo kesi itafunguliwa chini ya kifungu gani cha katiba?
 
CCM wanaendesha mapambano haya kisiasa zaidi na labda kisaikolojia. Wanajua kabisa kwamba kwenda mahakamani ni out. Hivyo wanachofanya ni kuwahamasisha wa-TZ kisiasa waone kwamba CHADEMA hawana maana. Na hapo ndipo ulipo mtihani mkubwa sana kwa CHADEMA. Ingekuwa mahakamani bila shaka wangefaidi sana. Lakini mahasimu wao wanawajengea wananchi fikra kwamba hawa hawana adabu kwa rais kinyume na "utamaduni wetu", hawajali wananchi waliowachagua, wanatishia amani na utulivu, wana kiburi - hawataki ushirikiano na wapinzani wenzao, wadini, wakabila, wamegawanyika (interviews za Zitto & Shibuda TBC), n.k. Na kwa kujua wa-TZ wengi walivyo "wavivu wa kufikiri" CCM wanaweza kufanikiwa! Hapo tena ya nini kwenda mahakamani? CHADEMA wajiandae kuipangua offensive hiyo kama wanataka kubaki kama chama mbadala-wasipoteze muda kujijenga kisheria/kikatiba pekee.
 

Hii hoja kama una simu ya Peter Kisumo mpelekee, yeye anapenda kesi dhidi ya vyama vya upinzani
 
Kitu kikubwa ambacho wote kimetupita kushoto ni kuwa HAKUNA KIFUNGU CHOCHOTE CHA SHERIA AU KATIBA AMBACHO KESI ITA-BASE,kwani kesi zinafunguliwa kwa kufuata sheria kwa hiyo kesi hiyo anayoitaka mtoa mada itatupiliwa mbali kwa kuwa haina vifungu vya sheria wala katibba inavyovisupport...
 

CCM haina time kwa sasa na upuuzi huo. Rais ni Jakaya Mrisho Kikwete naye anatokea CCM.
 
hakuna "mgogoro uliopo sasa hivi kati ya CCM na CHADEMA"

get your subject right

UKO TANZANIA HII AU WAPI??? HATA WALIOKO MAREKANI WANAJUA KWETU iko issue. Hivi yule Chiligati alieongea na kutishia kupeleka motion bungeni ni wa chama gani??? au ni wa Chama cha Dovutwa??? if so una haki ya kuongea upupu wako hapa JF.

Mwanakijiji hawa jamaa hawawezi fanya hivyo maana hawana haki ya kufanya hivyo hata kama mwanya wa kisheria na kikatiba upo.
 

Katiba ina kataza kuhoji matokeo ya Uraisi ambayo yametangazwa na NEC Lakini sina uhakika kama kifungu hicho kina ruhusu kuhoji namna NEC ilivyofikia kuyatangaza hayo matokeo kama anavyosema ndugu yangu Rutashubanyuma hapo juu. Kama hivyo ndivyo nahisi ni kama kitendawili cha Yai na Kuku kipi kilianza, maana kama unazuiwa kuhoji matokeo ya Urais vipi uruhusiwe kuhoji mchakato ulopelekea kuyapata hayo matokeo yalompatia Mr JK Urais??? Mi nafikiri njia muafaka ni CDM ambao wao wanaamini kuwa walishinda kwa mujibu wa returns zao walizopata kwa mawakala wao kama kweli ni AUTHENTIC basi kama walivyofanya kwenye Operation Sangara, basi waufikishe ukweli huu kwa wananchi na kuwaonyesha ushahidi kamili wa nani alifanya nini na kwa wakati gani. Wananchi wa leo si wa jana au juzi, wana uwezo mkubwa wa kuelewa mambo naamini kwa kuanzia na uchaguzi ujao wa serikali za mitaa in 2 yrs time watatoa hukumu inayostahili kwa wote waliodhulumu kura za wananchi na itakapofika 2015 itakuwa ni climax ya hukumu hiyo
 
Kwanza nakupengeza sana MMK kwa hoja yako. Ni hoja nzuri sana ambayo inatakiwa kuangaliwa vizuri. Kwa upande wa CHADEMA ni turufu kwani wataweza kujitetea na kueleza kwanini hawamtambui na pia CCM itabidi waonyeshe nikwa jinsi gani huyu RAIS WAO ameshinda kihalali.

Pili ikitokea CCM wakafanya hivyo mlango mwingine wa Demokrasia utakuwa umefunguliwa Tz. Na nadhani itapelekea MAHAKAMA ZETU sasa zitoe haki ya kweli siyo ujanja ujanja.
 

Unachosema ni kweli kwa upande fulani. Alichojaribu kuibua huyu MMK ni kuwa kama Cpt. Chiligati aliona kuna kifungu kilivunjwa waende mahamani kufungua kesi ya kikatiba kuwalazimisha CDM.

Pia kama umefuatilia Police wamezuia CDM kufanya mikutano yoyote ya hadhara mpaka hapo khali itakapo tulia. Hali gani mbaya wao ndiyo wanajua. Labda mpaka wamtambue JK.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…