CCM ijifunze toka Kenya. Nguvu ya dola haiwezi tumika kuishinda nguvu ya umma

CCM ijifunze toka Kenya. Nguvu ya dola haiwezi tumika kuishinda nguvu ya umma

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Ni dhahiri sasa kuwa maandamano ya Gen.Z kule Kenya hayawezi tena kutulizwa na Polisi au Jeshi maana kitakacho tokea ni mauaji ya Raia ya kutisha na hilo haliwezi kukubalika duniani pote.

Umma wa Kenya umeamua kupitia vijana wasio na ajira na hata wenye nazo bila kuongozwa na chama chochote cha siasa au makundi ya kikabila au kidini njia ambayo huwa inaishia kuwagombanisha wanaopinga mambo ya hovyo ya serikali.

CCM inakawaida kutumia vyombo vya dola kuzuia harakati zite za kuikosoa. watu watapigwa, kukamatwa, kutekwa na hata kupotezwa lakini wajue nguvu ya umma ikijiunga pamoja bila kutumia vyama, dini au ukabila basi hakuna yeyote wa kuwazuia.

Ni ngumu kwa CCM kulitambua hilo la NGUVU YA UMMA haishindwi kitu, kwa sababu wana kiburi cha uzima ila siku Watanganyika wakiamka IMEKWISHA.
 
Viongozi wengi wakishatoka madarakani ndio wanaona hatari zilizopo.
 

Attachments

  • VID-20240630-WA0002.mp4
    5.4 MB
Waendelee kuandamana...Lakini uporaji na uharibifu wa mali za raia wenzao kwa kisingizio cha kupinga mswada wa sheria ni uharamia na ujambazi usiokubalika katika utawala wa haki unaozingatia sheria!
 
Ni dhahiri sasa kuwa maandamano ya Gen.Z kule Kenya hayawezi tena kutulizwa na Polisi au Jeshi maana kitakacho tokea ni mauaji ya Raia ya kutisha na hilo haliwezi kukubalika duniani pote.
Hapa ndiyo utaona umuhimu wa kulea na kukuza vyama vya siasa. Hawa Gen Z wangekuwa chini ya mwavuli wa chama cha kisiasa ingekuwa ni rahisi kuwatuliza kupitia kiongozi wa chama chao. Lkn wao wanaongozwa na hasira zao tu.

CCM, kwenye maandamano ya Kenya kuna masomo mengi
 
Wanajua sana, ndiyo maana wako karibu na polisi, majeshi. Wanachotakiwa kujua tu, wananchi ni wengi kuliko vyombo vya usalama. Wananchi wakichoka, hakuna namna ya kuwatuliza.
 
Nguvu ya umma ipi kaka unayoiongelea?? Kama ni hii hii ya wabongo sidhani...
 
Nguvu ya umma ipi kaka unayoiongelea?? Kama ni hii hii ya wabongo sidhani...
Mkuu hata Kenya lilikuwepo hilo, akijitokeza mtu kushawishi wafanye hivi wengine wanampinga eti huyo kabila fulani au dini fulani.
Sasa vijana Gen.Z wameamua hakuna cha kabila wala dini ni Kenya tuu.
Na wetu wakiacha huo ufala basi kwisha kazi
 
Back
Top Bottom