CHIPESI NAMISUKU
Member
- Oct 7, 2019
- 51
- 157
Nimekuwa na Interested sana na Siasa za Jimbo la Tarime vijijini kwa Sasa kuliko majimbo Mengine. Hii ni baada ya Naibu Waziri Tamisemi kuonyesha Nia ya kulitaka hili Jimbo kwa udi na Uvumba.
Nini nakiona Tarime vijijini.
Kuna Kosa kubwa la kiufundi linafanyika kwa chama changu NDANI ya Jimbo hili. Kitendo Cha kumruhusu Waitara kufanya vurugu za Moja kwa Moja za kampeni NDANI ya Jimbo hili Chadema haiathiriki kama CCM itakavyoathirika.. Kosa tulilolifanya kwenye Jimbo hili 2015 linaweza kujirudia tena na CCM ikapasuka vibaya Sana Tarime... Kwanini nasema hivyo?
Kuna mtu anaitwa John Gimunta, John Gimunta yeye ni mzaliwa wa kata ya Nyamwaga. Ni mwana CCM na alikuwa mwekahazina wa chama miaka ya nyuma
Mwaka 2015 alikuwa kwenye kambi ya mgombea Kangoe ila dakika za mwisho kwenye kura za maoni akaamua na yeye kugombea.
Ilileta kizaazaa sana, yeye ni koo ya wairege Koo hii ya Waigere ni wengi kwenye jimbo la Tarime vijijini. Ni utaratibu usio Rasmi kuwa Tarime kura hipigwa kwa koo kama koo yako ni ndogo kushinda ni kazi kwelikweli.
Baada ya yeye kujitosa kugombea alianguka kwenye kura za maoni ikatokea ugomvi kati yake na Kangoe ugomvi mkubwa sana.
Mwisho wa siku Gimunta aliamua kukaa pembeni bila kumsapoti Kangoe, inasemekana aliapa kuwa Kangoe hawezi shinda yeye akiwa hai. Mwisho wa siku inasemekna alimuunga mkono Heche indirect pamoja na wafusi wake yeye akiwa kiungo muhimu kuhakikisha Kangoe hapati ubunge.
Inasemekana alitoa taarifa za mikakati ya kampeni na mbinu zote za ccm kwa chadema mwisho wa siku heche akashinda chama kikagawanyika yakatoke makundi ndani ya chama Gimunta akaonekana alikishika chama miguu kisishinde ubunge aliyekuwa katibu mkuu CCM Kinana akasema wote waliosababisha chama kushindwa wafukuzwe.
Kwa kuwa Gimunta ananetwork kubwa alijitetea na akasalia kwenye chama Baada ya hapo kambi ya Kangoe imeendelea kumlaumu kuwa yeye aliwanyima ushindi.
Kuelekea 2020 Gimunta alikuwa amejipanga haswa lakini hesabu zake zinaonekana kuchakachuliwa na Ujio wa Waitara na siasa anazofanya waitara ndani ya jimbo Hilo. Hapa natabiri mpasuko mkubwa Sana Kama Viongozi wa Chama hawatamdhibiti Waitara.
Kwa jinsi ambavyo Waitara anafanya Siasa zake ni Kama katumwa na Viongozi wa juu, yaani ana Baraka zote na kwa jinsi anavyoongea ni Kama tayari ameshashinda kura za maoni. Nitaadharishe kuwa huyu Gimunta na wenzake Kama wakiamua kumwaga mboga Hali itakuwa tete Sana hapa.
Ni vizuri Hawa wahamiaji waliokuja ndani ya chama kuwa na nidhamu na waliokipigania chama usiku na mchana kipindi kile Lowassa alivyoamua kutuzungusha mikono kwa kauli Mbiu yake ya mabadiliko.
KUHUSU HECHE.
Kuna uwezekana mkubwa heche asigombee Tarime Vijijini kwa kuwa anatoka Sirari kata ambayo nadhani soon inaweza hamishiwa jimbo la Tarime mjini. Tukumbuke kuwa mpasuko ndani ya CCM ndio uliompa Heche Ubunge. Vinginevyo hapa asingelishinda kutokana na factor ya Koo ambayo nimeizungumza hapo juu.
Inasemekana Heche anaeleweka zaidi Tarime mjini na kiuhalisia Chadema imekuwa ikifanya vizuri zaidi kwenye miji kuliko vijijini. Hii ni factor inayomvuta zaidi kusogea mjini. Heche anajua fika kuwa Koo yake ya wasiwa kule Tarime vijijini ni ngumu kutoboa hivyo asilimia zankuondoka hapa Ni zaidi ya 80.
Chadema Tarime vijijini wanaweza kumsimamish Moses Misiwa Diwani wa Nyamwga na M/kiti wa Halmashauri. Hata hivyo Kuna uwezekano vurugu anazofanya waitara kwa sasa ndani ya Jimbo Hilo likawapatia Chadema mgombea na actually atakuwa Gimunta. Kama Hali ikiwa hivyo Jimbo hili linaweza kurudi Chadema kwa uzembe wetu wenyewe.
GIMUNTA NI MAESTRO WA SIASA ZA TARIME VIJIJINI.
Wakati wa uchaguzi ndani ya CCM Gimunta alimuunga mkono Mgombea aliyeitwa Thobius Raya. Mwisho wa Siku Raya hakushinda Watu walijua ndio mwisho wa Gimunta. Baada tu ya uchaguzi Gimunta alienda kwa Mwenyekiti mpya wa Mkoa ambaye alikuwa hamuungi mkono Sameul Kiboye na kumuomba msamaha na kuahidi kushirikiana naye.
Ndio maana Mwenyekiti wa Mkoa ndugu Sameul Kiboye amewahi kumuita Waitara kwenye kamati ya MAADILI kuhusu kuanza kampeni mapema.
MWISHO.
Tayari Waitara kashaipasua CCM Tarime vijijin UVCCM wameakubeba mabegi ya Waitara. Tukumbuke Waitara alivyoitwa kwenye kamati ya MAADILI ya Mkoa alisindikizwa na Mwenyekiti wa UVCCM akiwa Kama bodyguard wake. Hivyo UVCCM ipo kwa Waitara huku Mwenyekiti wa CHAMA akiwa kwa Gimunta. Kazi ipo hapa.
Kangoe yeye ameamua kunyoosha mikono na kwasasa anapambana mwanawe awe Mbunge Tarime mjini.
All in all CHAMA kisifumbie macho rafu hizi. Zipo kwenye majimbo mengi tu siku za Usoni tutajadili Jimbo la Moshi Vijijini....