Natoa tu angalizo kwamba hili taifa la Wamachinga limetengenezwa na ilani ya CCM huku Wakuu wa Wilaya na Mikoa wakishindana kutoa kwa wingi Vitambulisho vya Mjasiriamali.
Ghafla tena Wakuu wa Wilaya wale wale wanaanza kuwakana wamachinga kwamba wanafanya biashara barabarani na maeneo yasiyoruhusiwa.
Angalizo langu ni kuwa hawa wamachinga, bodaboda na bajaji limeshakuwa kundi kubwa lililooteshwa kama "uyoga" hivyo linahitaji akili kubwa kulidhibiti.
Wakati wanapewa vitambulisho kwa lazima ilijulikana kabisa kwamba wapo barabarani, tusisahau hilo.
Kazi Iendelee!