CCM ilihusika kifo cha Wangwe?



Hapana ccm ni chama makini kama kilivyo chadema cuf nk Ila kuna watu ndani ya vyama hivyo kuna mifisadi tu .

Huwezi sema chadema ama SLAA ama ZITTO ndio kaanzisha hii move nenda nyuma kidogo uone nani alisababisha IDD SIMBA kujiuzulu,nani alisababisha Mbilinyi kama sikosei waziri wa fedha kujiuzulu na kwa sababu zipi?

Nakumbuka enzi hizo ilikuwa ni SKENDO akina Dr SLAA wao wameiita MAFISADI.Huwezi kabisa ku hadaa watu kwa kusema uvumbuzi wa uovu umeanzishwa na chadema .Sema kweli hili la EPA ndilo limeshkiliwa bango na SLAA.

Hizi juhudi ktk hili kuna jamaa wanalichukulia ili kupata umaarufu kisiasa kitu ambacho kipo tu enzi na enzi.

Hili la Tarime ccm kushindwa wala msilichukulie eti ndio mwanzo wa ukombonzi NEVER tumeona akina MREMA wakibebwa ,gari lao likisukumwa .tuambieni ukweli wakati wa MREMA na saizi CHADEMA ni wakati upi watanzania walipenda upinzani??

Pia tuambiane wakati Mrema ana wabwaga CCM temeke napo tutasema vipi?

Tatizo letu tunapenda kuzidaganya akili zetu kwa vitu vidogo kuwa vikubwa .
Ukombozi unahitajika LAkini si kwa viongozi wa vyma vilivyopo
 
damu yako ewe CHACHA WANGWE NA IWE JUU YAKO WEWE ROSTAM AZIZ, YUSUF MANJI, MAKAMBA, LOWASA, NK, NA VIZAZI VYENU VYOTE
 

Ulichoandika hapo ni playbook ya ccm..No doubt ni mazingira yaliyowafanya wabweteke....Kuweza kujustify kuwa eti hakuna viongozi wazuri kwenye upinzani simply kwasababu ya mifano uliyoitolea.

Lakini trust me kama hawa watu wakija pamoja na kuchapa kampeni makini...This time ccm mtabwagwa.

Siasa zinabadilika ndugu yangu na uchumi wa dunia unakoelekea ni wazi upepo unafavor mabadiliko.

Watu washachoshwa duniani kote...Wamechoshwa na ufisadi kiasi cha kwamba ile michezo ya kisiasa ya zamani ambayo mingi ni michafu ita backfire vibaya na mambo yanaweza yakawa si mazuri to the status quo.

Mkamap ulichosema ndio udhaifu ambao wamekuwa wakiutumia ccm...Je will it work this time around?

It remained to be seen...One thing for sure is PEOPLE ARE TIRED WITH THE SAME OL POLITICS.
 


Jmushi
Wewe subiri tu ikifika 2010 utaona jinsi wapinzani wanavyotengana ,Saizi mimi naamini CUF na CHADEMA wanapigiana timing tu kwamba wapo pamoja.

Itakapofika 2010 hawa jamaa watapigana vijembe wao kwa wao na ndio utakapoona watanzania tulivyo.

Leo CHADEMA na CUF wanaelewana kwa sababu CUF hawakusimamisha mgombea wao Tarime, akina Mbatia na Mrema ni wafuasi wa ccm kwa vile walisimamisha wagombea wao.

Leo mtanipinga sana ktk hili lakini Jmushi subiri mda ufike ndio utaona ni nini wana siasa wetu wanatafuta
 
Mbatia used to be a good politician sijui nini kimembadilisha huyu mtu..Nafikiri most of it is jokeying for power.
Mrema alisimamisha mgombea wake Tarime?
 

Hapo sasa ndio tamu ya siasa!!!!!!!
 
Kama ni kweli Wangwe aliuwawa na hao watu basi kazi ipo.
Nilishasema huko nyuma kuwa Usalama wa Taifa umegawanyika...Ila nawaombea wale wazalendo washinde...Assuming wapo, Maana tunataka nothing but the truth.
Mazingira ya kifo cha Wangwe yalibeba dhana kubwa zaidi ya jimbo la Tarime...Na ndio maana nikasema kuwa wananchi walio wengi walikuwa wakisubiri matokeo ya huko kwani aliyemwua Wangwe(Kama aliuwawa) Ndiye aliyeshindwa...Na vita ya Wangwe ni ya upinzani...Upinzani umepoteza mpiganaji.
Kwa mantiki hiyo basi wananchi tutaendelea kuwapima kutokana na sanduku la kura.
 
Mod aangalie sana hawa watu awape flag fulani ili tukijua comments imetoka kwa mtu fulani tujue lengo lake ni lipi hata kabl ay akusoma comments

Mod DON'T

JF is where we dare to speak openly!!!


Acha tuwasikilize tujue ujinga wao!!!!
 
Mbatia used to be a good politician sijui nini kimembadilisha huyu mtu..Nafikiri most of it is jokeying for power.
Mrema alisimamisha mgombea wake Tarime?

Mrema na mbatia ni ilikuwa sawa na cuf na chadema upo?
 
Mgirima unaweza kutueleza ni kwa kivipi habari hii ime expire kwa standard yoyote ile? I mean in whatever means and forms or even terms.
Uko free hapo kutumia vigezo vyovyote unavyovitaka ili kunishawishi ama kuonyesha ushahidi kuwa ime "Expire"


Nadhani sisi ni watu wazima na haihitaji kuwa na dregee mbili au masters kujua kuwa wanaotumwa na mafisadi kujibu mashambulizi dhidi yao ndani ya JF ni wengi kuliko tunavyodhani. Sasa kama kweli sio kuzima ufisadi ni nini mtu naposema hoja ya kifo cha Wangwe kime expire?Wanataka tusizungumzie tena kwani ukweli unadhihirika kidogo kidogo nani hasa aliehusika na kifo kile! Ingekuwa Chadema wamepoteza kwenye uchaguzi Mdogo wa Tarime leo tungekuwa tunachangia kitu kingine kabisa kuwa Chadema ndio waliosuka mipango na kumuua Wangwe at the same time wasingewachukulia hatua viongozi wa juu wa Chadema maana kwa kufanya hivyo ungekuja kujulikana ukweli wenyewe na wao hawataki hivyo!

Mafisadi mmeshinda some how kufungia MwanaHalisi lakini mjue kuna kina Kubenea wengi sana tofauti ya kubenea wa MwanaHalisi ni kuwa anatumia kalamu kuwachapa Mafisadi na hao Kubenea wengine wanatumia JF kuwachapa Mafisadi na Kubenea waliobakia wanatumia mawe Kupopoa misafara ya mafisadi na watetea mafisadi!

Angalieni msije mkawafungia
Watanzania wote kuzungumza! Maaana tulipofika ni kubaya!
 
Wakili,

Waswahili husema lisemwalo lipo, kama halipo laja.

Ukiangalia hiyo listi ya watetezi na walinzi wa mafisadi, hata Rais wetu yupokatika kundi hili na linakuja swali kubwa iweje yeye kama Rais, Amiri Jeshi mkuu na Mwenyekiti wa Chama Tawala awe chini ya shinikizo la hawa Wahujumu maarufu kama Mafisadi?

Wale wote walio viongozi wa ama CCM au Serikali wanawaogopea nini hawa Mafisadi? Ni lini tutapata Gorbachev wetu tuondokane na huu upuuzi wa kutawaliwa na "Wazungu Weusi"?

Hapa ndipo utaona kuwa Azimio la Arusha na miiko yake ililenga kuondokana na Tanzania kufikia hapa tulipo!
 

Malunde,

JamiiForum ina demokrasia ingawa mara nyingine huingia madoa. Msiwaogope wala kutaka hawa walinzi wa mafisadi humu ndani wawekewe mihuri kwenye paji la nyuso zao.

Waacheni wawe huru kama wale wanaopinga Ufisadi na ni hoja zinazotolewa ziwe vipimo vya kujua Uzalendo wetu.
 

Mkuu umenena, nami ninakuunga mkono na ........
 


Ukiwa unatakiwa ndani ya chama hata ukiua utabakia ndani ya chama!na ikitokea kuna watu wanataka wakuwajibishe wakubwa ndani ya chama watamtetea "mwenzetu" ila ukiwa hutakiwi na ikionekana kama wewe u kikwazo kwa maslahi yao hata kama hauna hizo skendo unazosema utaundiwa! Unakumbuka yaliyomkuta aliye wahi kuwa mkuu wa mkoa wa Tanga, Mkurugenzi mkuu wa usalama wa Taifa na mbunge wa Makete Dr Hans Kitine?Watu walio ona mbali (Sumaye na kundi lake) waliona kuwa angekuwa ni tishio kwao ndio maana wakaunda mkakati na kufukua "maiti" iliyo kufa tangu alipo kuwa mkuu wa mkoa wa Tanga! na akaachia ngazi! Na tunawajua wengi ambao wamefanya maovu yasiyoelezeka yanayochangia ugumu wa maisha tulionao lakini wanadunda ndani ya chama kwenye CC NEC na kamati mbalimbali!Chenge aliyekuwa AG wa serikali ya awamu ya tatu ndie aliefanikisha mikataba ya ubinafsishaji wa NBC na mashirika mengi tu kwa maslahi yake na ya mabwana zake ataendelea kuwepo CCM na ili mjue hilo ndio maana aliteuliwa kwenye tume ya kufatilia mkataba wa UVCCM. Mkiambiwa CCM ina wenyewe mjue ni kina nani!sio wewe wala kina Idd Simba!
 

Hapo awali nilisema kimamlaka akitoka Mungu ni Rais wa nchi yeye ndio anaeteua mawaziri na yeye ndie anaefire mawaziri. Lakini huyu anajua kuteua tu ikitokea tatizo anawaundia tume! Hao Mafisadi wanakuwa wananguvu kwasababu wao ndio waliemuweka hapo alipo!Hawezi kusema kitu zaidi ya kucheka cheka tu wakati anajua yeye ndie yupo hatarini zaidi kwa bahati nzuri dalili ameziona alipokuwa mbeya. Akiendela tusijeshangaa akaja kuoga mvua ya mawe na mavi!Muda anao anaweza kubadilisha hali na watu wakarudisha imani kwake unless awe hana uwezo wa kuona maandishi ukutani!
 


Hata CHADEMA ina wenyewe mkiambiwa hamtaki kuliona hilo.

Nikuulize maswali mawili tu ukiyajibu tutaendelea vizuri.

1.Kwanini marehemu wangwe alisimamishwa umakamu m/kiti chadema?

2. Na baada ya kifo chake risala ya chadema ilisema nini kuhusu marehemu wangwe?
 


Hiyo risala I real dont know nataka kukumbusha kuwa kabla ya kifo chake kulikuwa na harakati za yeye Wangwe kuhamia CCM na waraka wake ulitumwa kwa Fax a day before the scene. Fax ilitumwa kutoka CCM makao makuu dodoma ofisi ya katibu mkuu kwa uhakika zaidi wasiliana na Makamba atakumegea na sie utujuze.

Hiyo sababu ni muendelezo wa propaganda za CCM na Marehemu alikuwa akitumiwa. Mie nitakuomba ujaze makabila ya viongozi wa Chadema katika nafasi zilizo achwa n a mikoa wanaotokea.then tutaenda sawa.

1. Freeman Mbowe _____________________
2.Dr Wilbrod Slaa _____________________
3.Zito Z. Kabwe _____________________
4.Tundu Lisu _____________________
5.John Mnyika _____________________

Huu sio wakati wa siasa za magogoni mkuu.

PS.

I declare my interst on Chadema.

Mimi si mwanachama wa Chadema sina kadi ya uanachama wa chama chochote ila ni mtu mwenye kupenda siasa za upande wa upinzani na ninavifeel vyama viwili tu hapa Tanzania navyo ni CUF na Chadema na mie si mchagga wala mpemba shauri yenu msiotaka kuona na ilihali mana macho!
 
Mushi, kuna njemba zimeibuka siku za karibuni kutetea kwa kila hali uongozi mbovu wa JK, tutakula nao sahani moja maana wakati wa kuendelea kutuzuga na Watanzania kunyamaza kimya umeshapita miaka mingi sana.

Mkuu Bubu, hapa tupo ukurasa mmoja.
 

Mazungumzo ya kushushia kahawa!!
 

Hapana mkuu nani hapa ametaja wachaga mbona unajisitukia mkuu??

Mimi nimekuuliza maswali rahisi kabisa
nipe majibu yake yani
1.chadema walisema nini walipomsimamisha maremu chacha?
2.chadema walisema nini ktk mazishi yake ?very simple.

Majibu yako nitayajibu kutokea chini
5.gw'ana wa mayo
4.anatoka singinda sijui kabila lake
3.anatoka kigoma sijui kabila lake
2.sijui kabila lake
1. Mmachame

Harafu ccm wakaamua kumuwahi mwanachama wao mpya mtegemewa kwa kumuua ama chadema ndio walimuwahi kabla hajahama?

Na wewe jibu maswali yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…