Ndombwindo
JF-Expert Member
- Nov 23, 2013
- 1,387
- 2,085
Moja kwa moja kwenye mada bila kupoteza muda, ukiangalia namna nchi yetu iliyovyoendeshwa kuanzia 2005 awamu ya Kikwete mpaka 2015, na baadae 2015 mpaka 2020 awamu ya Magufuli utagundua kitu hapo.
Hulka za kiuongozi alizokuwa nazo Kikwete ziliruhusu wananchi kuwa wazi na uhuru katika kuwasilisha hoja na hisia zao binafsi (Being outside of the closet). Watanzania wengi waliweza kutoa hisia zao za moyoni kuwa chama hakifai. Kikwete hakuwa na namna maana hulka yake ndio ilimtaka hivyo kuwa mtazamaji tu na ndipo tulipofunuliwa kuwa Mkapa na Mwinyi walilazimika kuingilia kati kunusuru jahazi lao la CCM kutozama kutokana na wimbi zito la vuguvugu la wananchi. Kwa wakati huo Raia shida yao kuu ikiwa ni kuiondoa CCM madarakani bila kujali ni nani ataingia baada ya hapo na ndio maana Mbowe akaona fursa ya Lowassa.
Magufuli kwa upande wake alijua hii hasira na kiu ya wananchi, katika kuhakikisha anarejesha ushawishi ambao ulipotea kwa kiwango cha hali ya juu aliwahusisha wananchi kila jambo kwa undani wake na kufanya maamuzi hadharani ili kurudisha trust iliyokuwa imepotea kabisa. Inashangaza kuona Nape kwa mfano au Kinana wakisifiwa kwa utumishi wao uliotukuka ingali chama kidogo kiwafie mikonoji, unless otherwise tuwe tunaongelea utayari wao wa kuishi wakiwa upinzani hapo tutakuwa tumewatendea haki, lakini still ndio hao hao waliokuwa wakijinasibu kwa bao la mkono mithiri ya mkongwe Maradona.
Magufuli kapambania legacy ya Mwalimu Nyerere kiasi cha kufanya uchaguzi 2020 kutokuwa na kashkash za 2015 kabisa. Si ajabu kuwaona CCM tarehe 14 October wakijikuta wapo Chato badala ya Butiama, tunaweza kuwabeza tuwezavyo lakini wanajua namna walivyonasuliwa kwenye tundu la choo na Marehemu Dr. John Magufuli. Pia ninauhakika wanaichungulia 2025 na wasijue watasimamia kuti gani endapo chombo kitakwenda hali jojo hapa katikati.
Namna gani Magu alitumia kuwanasua ni suala jingine, hata hivyo it had to be the hard way with due considerations. Mama yetu kwa sasa analijua hili vizuri maana na yeye ni part ya CCM, karata zipo mkononi na uamuzi ni wake kutoa joka mapema au kulibakiza ndani akisubiria timing. Time will tell the tale.
Imeisha hiyo.