Mfikirishi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 8,939
- 10,403
Hili genge liitwalo ccm limefanikiwa kutugawa na sasa tumegawanyika vipande vipande. Kuna ambao wanaona nguo, tshirts, kofia, khanga, lift, chakula na fadhila nyingine ni muhimu sana kwao kwa sasa kuliko hata ahadi na ilani ya uchaguzi.
Kuna ambao mikopo midogo midogo, bendera na mabango ni muhimu sana kwao kwa sasa.
Wachache sana wanafikiria kuhusu:
1. Mafao ya wafanyakazi na kikokotoo cha kikatili kilichowekwa na wakatili
2. Mishahara ya wafanyakazi (kwa miaka 5 sasa haijaongezwa)
3. Makato ya kikatili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu
4. Mazingira magumu ya sekta binafsi
5. Ajira zinazotolewa kibaguzi
6. Ukandamizaji, uminywaji wa uhuru na haki ya kuishi, kupata habari na kutoa maoni
7. Udhalilishaji na ubaguzi wa wazi wazi...
Wametugawa na sisi tumekubali kugawanyika!! Wengi wameyasahau maslahi mapana ya taifa ketu...
Kama kawaida. ccm watajitangaza washindi. Wananchi watawavumilia. Na viongozi wa ccm watatenda kwa jinsi walivyozoea kutenda miaka nenda rudi...
Akili kubwa itaacha akili ndogo ziongoze...
Madhara yake Tanzania itabaki pale pale bila kupiga hatua zozote kimaendeleo na ushindani wa kimataifa...!!